Ni kwanini Ubelgiji ilitunza jino la dhahamu la shujaa wa Afrika?

Patrice Lumumba led Congo to independence

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Patrice Lumumba aliiongoza Congo kupata uhuru

Jino lililovikwa taji la dhahabu ndio masalia pekee ya shujaa wa uhuru wa Congo Patrice Lumumba.

 Alipigwa risasi na kikosi cha kufyatua risasi mwaka 1961 kikiungwa mkono kimya kimya na utawala wa ukoloni wa Kibelgiji, mwili wake ulizikwa katika kaburi fupi, lilichimbwa na kusafirishwa kilomita 200 (maili 125 ), akazikwa tena, akafufuliwa na halafu akakatwa vipande vipande na hatimaye kuyeyushwa kwa asidi.

 Kamishna wa polisi wa Ubelgiji, Gerard Soete, ambaye alisimamia na kushiriki katika kuangamiza mabaki alichukua jino, alikiri baadaye.

 Pia alizungumzia kuhusu jino la pili na vidole viwili vya maiti, lakini hivi havikupatiana.

 Imepangwa sasa kwamba jino lake litarejeshwa kwa familia yake katika sherehe itakayofanyika katika mji mkuu wa Ubelgiji Brussels.

 Soete ambaye alitunza vipande vya mwili ilielezea pia kuhusu tabia ya maafisa wa kikoloni wa Ulaya ya kurejesha masalia ya mwili nyumbani baada ya miongono kama kipindi cha kukumbuka kuwa kila mtu lazima atakufa.

 Lakini pia hatua hiyo ni udhalilishaji wa mwisho wa mwanaume ambaye Ubelgiji ulimchukuliwa kama adui.

 Soete, ambaye alionekana katika makala mwaka 1999, alilielezea jino na vidole alivyovichukua kama "aina ya nyara ya uwindaji". Lugha inayoonyesha kwamba kwa polisi huyo Mbelgiji, Lumumba- ambaye alikuwa anaheshimiwa kote barani Afrika kama sauti inayoongoza ya ukombozi wa Waafrika – alikuwa binadamu wa kudharauliwa.

 Kwa binti yake Lumumba, Juliana, swali analojiuliza ni iwapo waliomuua walikuwa binamu au la. "Unahitaji kiwango gani cha chuki kufanya unyama kiasi hicho?" anauliza.

"Hii inatukumbusha kile kilichotokea kwa Wanazi, kuchukua vipande vya miili ya watu - na uhalifu dhidi ya binadamu," aliiambia BBC.

Jino

Chanzo cha picha, JELLE VERMEERSCH

Maelezo ya picha, Binti yake Gerard Soete alionyesha jino, katika boksi lililofungwa kwa kufuli, kwa mpigapicha katiak mwaka 2016
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Lumumba alikuwa amepanda cheo na kuwa Waziri mkuu akiwa na umri wa miaka 34. Alichaguliwa katika siku za mwisho za utawala wa kikoloni, aliongoza baraza la mawaziri la taifa jipya huru.

 Juni 1960, wakati wa kukabidhiana mamlaka, Mfalme wa Ubelgiji Baudouin aliusifu utawala wa ukoloni na alizungumzia kuhusu babu yake, Léopold II, kama "mstaarabu" wa nchi.

 Hakusema lolote kuhusu mamilioni waliokufa au ambao waliofanyiwa ukatili chini ya utawala wake wakati huo wa kilichoitwa taifa huru la Congo Congo, kama mali yake ya kibinafsi.

 Kushindwa huku kukiri yaliyopita kulitawa miaka ya Ubelgiji kushindwa kukubali yaliyotokea, ambapo sasa ndio imeanza kukubali baada ya kuelewa kwamba Lumumba hakuwa msiri sana.

 Katika hotuba ambayo haikupangwa katika mpango rasmi, Waziri mkuu alizungumzia kuhusujinsi Wacongo wanavyoumizwa na ghasia na kudhalilishwa.

 Katika hotuba hiyo iliyotolewa kwa misemo ya kusikitisha, iliyokatishwa na makofi na hadhira iliyosimama kumshukuru alipoikamilisha alipoelezea "utumwa wa udhalilishaji ambao tumewekewa kwa nguvu".

 Wabelgiji walipigwa na butwaa, kulingana na msomi Ludo De Witte, ambaye aliandika makala ulioelezea ushahidi wa mauaji yake.

 Sijawahi kumsikia kabla Mwafrika mweusi akidiriki kuongea kama hivi mbele ya Wazungu. Waziri mkuu ambaye De Witte anasema alikuwa ameelezewa kama mwizi ambaye hakusoma katika vyombo vya habari vya ubelgiji, alionekana kama alikuwa akimuaibisha mfalme na maafisa wengine wa Ubelgiji.

Patrice Lumumba (Kulia) na mshirika wake Joseph Okito (Kushoto) walikamatwa Disemba 1960

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Patrice Lumumba (Kulia) na mshirika wake Joseph Okito (Kushoto) walikamatwa Disemba 1960

Baadhi wamesema kuwa kwa hotuba zake Lumumba alisaini waranti ya kifo chake mwenyewe, lakini mwaka mmoja baada ya mauaji yake uligubikwa na Vita Baridi na utashi wa Wabelgiji wa kuendelea kuidhibiti nchi.

 Wamarekani pia walipanga kifo chake kwasababu ya uwezekano kubadilika kuelekea Muungano wa Usovieti na upinzani wake usioshawishika dhidi ya ukoloni ,huku afisa wa Uingereza aliandika waraka uliopendekeza kwamba kumuua lilikwa ni chaguo lao.

 Hatahivyo, ilionekana kulikuwa na suala la chuki ya kibinafsi kwa jinsi Lumumba alivyodhalilishwa na kutafutwa.

 Kuangamizwa kabisa kwa mwili, pamoja na njia ya kupoteza ushahidi, inaonekana juhudi za kumfuta Lumumba katika kumbukumbu. Hakutakuwa na kumbukumbu, jambo linalopelekea uwezekano wa karibu kukana kwamba aliishi kabisa. Haikutosha tu kumzika.

Lakini bado anakumbukwa

Sio jambo dogo kwa binti yake Juliana – muendeshaji wa kampeni ya kutaka jino la Waziri mkuu lirejeshwe nyumani, ambaye amesafiri hadi Brassels kulipokea.

 Alikumbuka wakati wa utoto wake. Akiwa mdogo zaidi kati ya watoto wa Lumumba, na msichana wake pekee, alisema alikuwa karibu sana na baba yake.

 Bi Lumumba alikuwa "chini ya umri wa miaka mitano" alipokuwa Waziri mkuu. Anakumbuka aliporuhusiwa kuwa katika ofisi ya baba yake "kuketi tu na kumuangalia baba yangu alipokuwa akifanya kazi. Kwangu mimi alikuwa ni baba."

Lakini anatambua kuwa baba yake "ni wa nchi, kwasabau alifariki kwa ajili ya Congo…na kwa maadili yake na kwa Imani yake ya utu wa watu wa Afrika".

 Anakiri kwamba kukabidhiwa jino nchini Ubelgiji na kulileta katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo ni ishara "kwasababu kile kilichobakia hakitoshi kusema kweli. Lakini lazima aje nchini mwake ambako damu yake ilimwagika."

Jino lake litatembezwa katika maeneo ya nchi kabla ya kuzikwa katika mji mkuu Kinshasa.

 Kwa miaka mingi, hatahivyo, familia ya Lumumba haikufahamu ni nini hasa kilichotokea kwa baba yao kutokana na ukimya uliozingira kifo chake.

Safari ya Lumumba kuanzia kuwa Waziri mkuu hadi kuwa muhanga wa mauaji ilichukua chini ya miezi saba.

 Mazishi ya jino la Lumumba-yamepangwa kufanyika kuambatana na maadhimisho ya miaka 61 ya hotuba maarufu ya uhuru ya Lumumba - itakayotoa fursa ya kukumbuka yaliyotokea miaka iliyopita