Tetesi za Soka Ulaya Jumapili: Nani kumrithi Salah Liverpool?

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool wamempa beki wa kulia wa Uingereza na anayelengwa na Real Madrid Trent Alexander-Arnold, 26, mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya £78m. (Mirror).
Kwa upande mwingine, Liverpool wanamtaka winga wa Bayern Munich na Ujerumani Leroy Sane, 28, kuchukua nafasi ya fowadi wa Misri Mohamed Salah, 32. (Fichajes), Salah aliweka wazi katika mahojiano maalum kuwa ataondoka Liverpool mwisho wa msimu wa 2024/2025.
Paris St-Germain iko tayari kufanya mazungumzo na Aston Villa kuhusu dili la kubadilishana fedha na wachezaji likiwemo fowadi wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, na mshambuliaji wa Colombia Jhon Duran, 21. (Football Insider).
Napoli wameanza mazungumzo na Liverpool na wakala wa Federico Chiesa ili kupata mkopo wa miezi sita kwa winga huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 27. (Footmercato)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa Uholanzi Joshua Zirkzee anataka kuondoka Manchester United, huku Juventus ikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Gazzetta dello Sport),
Mshambulizi wa United na England Marcus Rashford, 27, amevutiwa na klabu ya Ligi Kuu ya Soka Seattle Sounders. (Teamtalk).
Wolves wanakaribia kurefusha kandarasi ya fowadi wa Brazil Matheus Cunha licha ya kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 analengwa na Arsenal Januari. (Eduardo Burgos, Diario AS).
Brighton wametoa ofa ya takriban pauni milioni 23 kumnunua beki wa Palmeiras Vitor Reis, 18, huku klabu hiyo ikitarajia kuleta nyongeza katika dirisha la uhamisho la Januari. (Mail).

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City wanatayarisha ofa kwa mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Omar Marmoush, 25, huku wakitaka kuzishinda Arsenal, Tottenham na Liverpool ili kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri. (Footmercato - kwa Kifaransa)
Beki wa kushoto wa Manchester United Tyrell Malacia, 25, analengwa na klabu ya Italia Juventus katika uhamisho wa kushtukiza. Mholanzi huyo anaonekana kama mbadala wa mlinzi mwenye uzoefu wa Brazil Danilo, 33. (Daily Star)
Real Betis wako kwenye mazungumzo ya juu zaidi ya kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Stefan Bajcetic, 20, kwa mkataba wa mkopo kutoka Liverpool. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Crystal Palace Muingereza Jadan Raymond, 21, analengwa na Dundee na Colchester United katika dirisha la uhamisho la mwezi huu. (Football Insider)
Bournemouth wamekubali dili la kumsajili beki wa kushoto wa Argentina Julio Soler, 19, kutoka Lanus kwa mkataba wa takriban pauni milioni 12. (Uriel Lugt)
Ipswich Town imekubali dili la kumsajili beki Ben Godfrey kwa mkopo kutoka Atalanta. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anasemekana kukamilisha sehemu ya kwanza ya matibabu yake siku ya Jumamosi. (Fabrizio Romano)
Imetafsiriwa na Munira Hussein












