Tutarajie nini katika michezo ya Afrika katika mwaka 2025?

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Emmanuel Wanyonyi anatarajia kuvunja rekodi ya dunia ya mita 800 mwaka wa 2025, huku wachezaji wa mpira wa vikapu wa wanawake wa Nigeria na wanasoka wa Afrika Kusini wakitetea mataji yao ya bara.
Muda wa kusoma: Dakika 6

Emmanuel Wanyonyi ana matumaini ya kuvunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 800 mwaka 2025, huku wachezaji wa mpira wa kikapu wa Nigeria na wanasoka wa Afrika Kusini wakitetea mataji yao ya bara.

Mwaka mpya unapoanza, huja na ahadi za mafanikio ya wanariadha wa Afrika.

Mataji ya michezo ya bara la Afrika yanasubiriwa katika soka la wanaume na wanawake mwaka 2025, huku Rwanda ikiwa tayari kuwa mwenyeji wa baadhi ya waendesha baiskeli bora duniani.

Wanariadha wa Afrika wanatafuta kuvunja rekodi za zamani, wakati vipaji vipya vitapata fursa ya kujithihirisha kwenye jukwaa la dunia.

Hii ni kalenda yako ya mapema kulingana uchanganuzi wa BBC Sport Africa kuhusu baadhi ya tarehe muhimu za matukio ya kimichezo barani Afrika katika miezi 12 ijayo.

Unaweza pia kusoma:

Joto la kandanda Afrika Kaskazini

Macho yote yatakuwa Morocco wakati ufalme huo ukiandaa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (AFCON), sawa na wanaume (AFCON) na Kombe la Dunia la Wanawake wenye chini ya umri wa miaka 17.

Baada ya kucheleweshwa kutokana na michezo ya Olimpiki, AFCON ya Wanawake ya 2024 itafanyika kuanzia Julai 5 hadi 26.

Afrika Kusini itatetea taji hilo wakati mara ya mwisho Morocco na Zambia zote zinawania taji lao la kwanza la bara na Nigeria wanapania kulinyakua taji hilo. Botswana na Tanzania zitacheza mechi yao ya pili tu katika fainali hizo.

Kwa wanaume, kutakuwa na karibu mwaka kamili wa kutarajia kabla ya AFCON ya 2025, ambayo itaanza Disemba 21 na kumalizika Januari 18, 2026.

Ivory Coast wanasafiri kwenda Afrika Kaskazini kama mabingwa watetezi lakini shinikizo litakuwa kwa wenyeji ikizingatiwa kuwa Atlas Lions ndio timu iliyoshika nafasi ya juu zaidi barani Afrika na kutwaa taji lao pekee mwaka 1976.

Mashindano ya Kombe la Dunia

g

Chanzo cha picha, SUDAN FA

Maelezo ya picha, Wachezaji wa Sudan wamefuzu kwa AFCON 2025 licha ya athari za vita vya wenyewe kwa wenyewe na bado wanapigania nafasi katika Kombe la Dunia la 2026.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Miezi 12 ijayo itakuwa muhimu kwa soka la bara kwani michuano ya Mataifa ya Afrika (1-28 Februari), mashindano ya wachezaji wanaocheza katika nchi zao, yatapima maendeleo ya wenyeji wenza Kenya, Tanzania na Uganda katika maandalizi yao ya AFCON 2027.

Baada ya hapo, ushindani utaongezeka na kuwa moja ya timu tisa za Afrika zilizohakikishiwa nafasi katika Kombe la Dunia la FIFA la 2026.

Comoro, Rwanda na Sudan - zote tatu zikiwa juu ya jedwali - zinafuatilia kile ambacho kitakuwa mechi ya kwanza ya kihistoria katika fainali.

Mechi za mchujo mwezi Novemba zitapeleka taifa jingine la Afrika katika raundi ya kufuzu kwa bara la Afrika mwaka 2026 kwa ajili ya kupata nafasi ya mwisho ya kufuzu kwa timu 48.

Katika mchezo wa klabu, uzinduzi wa timu 32 za Kombe la Dunia la Klabu la FIFA (Juni 15-Julai 13) utachezwa nchini Marekani, na Al Ahly, Wydad Casablanca, Mamelodi Sundowns na Esperance Tunis watajaribu kuwatoa uzito wa Ulaya na Amerika Kusini.

Ligi ya soka barani Afrika inatarajiwa kurejea na muundo mpana, wakati Ushelisheli itakuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la Soka la Ufukweni (Mei 1 hadi 11) kwa mara ya kwanza barani Afrika.

Mashindano ya Riadha ya Dunia

Baada ya mashindano ya ndani ya dunia na ya kupokezana vijiti, mkutano mkubwa wa riadha wa mwaka utafanyika Japan huku Tokyo ikiwa inaandaa Mashindano ya Riadha ya Dunia (tarehe 13 hadi 21 Septemba).

Bingwa wa Olimpiki wa Botswana katika mbio za mita 200 Letsile Tebogo anakabiliwa na ushindani mkali katika jitihada zake za kuongeza dhahabu nyingine ya dunia katika ukusanyaji wake wa medali, Faith Kipyegon wa Kenya anaweza kulenga taji la tatu mfululizo la dunia la mita 1500, na mwenzake Emmanuel Wanyonyi ameiambia BBC Sport Africa kuwa analenga kuvunja rekodi ya dunia ya David Rudisha ya mita 800.

Tukizungumzia rekodi, je, huu unaweza kuwa mwaka ambao alama ya saa mbili katika marathon ya wanaume hatimaye imevunjwa katika mashindano ya wazi? Marehemu Kelvin Kiptum alikuwa sekunde 36 tu kutoka kuvunja kizuizi huko Chicago mnamo Oktoba 2023.

Wanariadha wa Afrika Mashariki wanaopigania uhuru wa juu watakuwa na mbio za ziada kuweka rekodi baada ya Sydney (Agosti 31) kuongezwa kwenye orodha ya marathoni kuu.

Wakati huo huo, New Delhi itakuwa mwenyeji wa Mashindano ya Dunia ya Riadha ya walemavu kutoka Septemba 26 hadi Oktoba 5.

Kuna raundi sita za kufuzu zilizobaki, katika miezi ya Machi, Septemba na Oktoba. Washindi wa kundi hilo pekee ndio watakaoshiriki mashindano katika nchi za Canada, Mexico na Marekani.

g

Chanzo cha picha, Golazo

Maelezo ya picha, Waendesha baiskeli wa Eritrea wataendelea na ushindi wao mitaa ya Kigali katika Mashindano ya Dunia yanayofanyika barabarani

Historia pia itaandikishwa wakati Rwanda itakapoandaa mashindano ya dunia ya baiskeli , ambayo yataitembelea Afrika kwa mara ya kwanza tangu yaanzishwe miaka 98 iliyopita.

Kigali ni ukumbi wa mfululizo wa mbio za wiki nzima ( kuanzia tarehe 21 hadi 28 Septemba) na Eritrea itakuwa na matumaini ya kuonyesha utawala wake wa mchezo huo hivi karibuni kwenye hatua ya bara hadi hatua ya kimataifa. Mshindi wa jezi ya kijani ya Tour de France Biniam Girmay anatarajiwa kuwa miongoni mwa washindani.

Mataji ya bara yataandaliwa katika mchezo wa mpira wa kikapu -AfroBasket, huku wanawake wa Nigeria wakielekea Ivory Coast kutetea taji lao kwa mara ya nne (Julai 25 hadi Agosti 3). Senegal na Mali zinatarajiwa kuwa wapinzani wa karibu wa D'Tigress.

Michuano hiyo ya wanaume (itakayofanyika Agosti tarehe 12 hadi 24) inarejea kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2021, huku Angola ikiwa mwenyeji na Tunisia ikipania kutwaa taji la tatu mfululizo.

Mashindano ya Dunia na Uchaguzi

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baada ya kushinda dhahabu katika daraja lake la uzito katika Michezo ya Paris ya 2024, je, mwanariadha wa Misri Rehab Ahmed anaweza kushinda medali katika mashindano ya dunia kwenye ardhi ya nyumbani?

Afrika Kusini ndio wawakilishi pekee wa bara katika Kombe la Dunia la Rugby 2025 litakalofanyika nchini Uingereza (Agosti 22-Septemba 27), lakini Wanawake wa Springbok wanatafuta kupata ushindi wao wa kwanza katika mashindano hayo tangu 2014.

Nchi hiyo pia itashiriki katika Kombe la Dunia la Kriketi ya Wanawake mwezi Septemba, ikitarajia kuboresha matokeo yao ya nusu fainali mawili ya mwisho ya mashindano ya 50.

Guinea itacheza mechi yake ya kwanza katika michuano ya dunia ya mpira wa mikono kwa wanaume (Januari 14-Februari 2) kati ya timu tano za Afrika, wakati mechi hizo upande wa wanawake wanawake zitaanza mwishoni mwa Novemba.

Misri itakuwa mwenyeji wa Mashindano ya Dunia ya Kuinua uzani (Oktoba 11 hadi 18), wakati Tokyo itakuwa mwenyeji wa Olyimpiki ya wasiosikia -Deaflympics mwezi ujao (Novemba 11 hadi 18).

Archery na michezo ya walemavu ya Olyimpiki ya, badminton, mpira wa wavu wa pwani, para-cycling, uzio, para-swimming na volleyball pia itakuwa na michuano ya dunia katika 2025.

Nje ya uwanja, Kirsty Coventry anagombea urais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki - moja ya kazi muhimu zaidi katika michezo.

Raia huyo wa Zimbabwe anatajwa kuwa mtu wa nje katika uchaguzi wa mwezi Mei.

Wakati huo huo, Patrice Motsepe atashuhudia muhula wake wa pili wa miaka minne kama rais wa Shirikisho la Soka la Afrika uliothibitishwa mwezi Machi.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi