Ajuza wa Kiafrika mwenye miwani mikubwa na mtindo wa mavazi wa kipekee

Chanzo cha picha, Luxury media Zambia
Bibi mmoja katika maeneo ya vijijini nchini Zambia amekuwa mwanamitindo na mwenye hisia za mtandao, baada ya kukubali kucheza na mavazi yake kwa kuyavaa kwa njia tofauti tofauti na kubadilishana mavazi na mjukuu wake ambaye ni mwanamitindo.
Margret Chola, ambaye ana miaka takriban 80 na ushee, anajulikana kama "Legendary Glamma" - na anapendwa na wafuasi 225,000 wa Instagram kwa picha zake za kushangaza.
"Ninahisi tofauti, najihisi mtu mpya na hai katika nguo hizi, kwa njia ambayo sijawahi kuhisi hapo awali," Bi Chola ameiambia BBC. "Ninahisi kama ninaweza kushinda ulimwengu!"
Msururu wa mtindo wake wa mavazi wa Granny Series ulibuniwa mnamo 2023 na mjukuu wake Diana Kaumba, ambaye ni mwanamitindo ambaye yuko New York City.

Chanzo cha picha, Luxury Media Zambi
Alikuja na wazo hilo wakati alipozuru Zambia katika kumbukumbu ya mwaka wa pili tangu kifo cha baba yake - mtu ambaye anasema alihamasisha shauku yake ya mitindo kwasababu kila wakati alikuwa amevaa vizuri.
Wakati wa ziara hiyo Bi Kaumba hakuwa amevaa mavazi yake yote yaliyoandaliwa kwa uangalifu, kwa hivyo alimuuliza bibi yake - au "Mbuya" kwa lugha ya Bemba - ikiwa angependa kujaribu mavazi yake.
"Sikuwa nafanya chochote wakati huo, kwahivyo nilisema tu: 'Sawa. Ikiwa ndivyo unavyotaka kufanya - kwa nini usifanye?'" bibi Chola alisema.
"Utanikosa wakati nitakufa na angalau kwa njia hii utakuwa unanikumbuka."

Chanzo cha picha, Luxury Media Zambia
Bi Kaumba alivalia nguo ya juu ya Mbuya na "chitenge" - kipande cha kitambaa chenye muundo kilichofungwa kiunoni. Na vazi la kwanza la Mbuya lilikuwa vazi la rangi ya fedha.
"Nilidhani itakuwa vizuri kumvalisha Mbuya mtindo wa hali ya juu na kisha kumpiga picha akiwa katika makazi yake ya asili," Bi Kaumba ameiambia BBC.
Mazingira hayo ya asili ni ya shambani katika kijiji kilichopo maili 10 , kaskazini mwa mji mkuu wa Zambia, Lusaka.
Mara nyingi Bibi Chola hupigwa picha za mavazi yake yote ya kuvutia nje - na mara kwa mara huwa ameketi kwenye kiti cha mbao cha kifahari au amejilaza kwenye sofa lake la ngozi.

Chanzo cha picha, Luxury Media Zambia
Upande wa nyuma kuna majengo ya matofali yaliyo wazi na paa za chuma, mashamba yenye mazao, miti ya maembe na mazao ya mahindi.
"Nilikuwa na wasiwasi sana nilipochapisha picha hiyo ya kwanza kwenye mtandano. Niliacha simu yangu kwa dakika 10 na katika dakika hizo 10 kulikuwa na watu 1,000 (likes) walioipenda ," anasema Bi Kaumba.
"Nilishangaa sana. Maoni yalikuwa mengi na watu walikuwa wakiomba nitume picha zaidi."
Ilikuwa Aprili 2024 ambapo Msururu wa Granny ulipoanza - baada ya Bi Kaumba kuchapisha mfululizo wa picha za bibi yake akiwa amevalia nguo nyekundu ya Adidas, mikufu kadhaa ya dhahabu, na taji la vito vya kupendeza.
"Ilinishangaza kusikia kwamba watu wengi duniani kote wananipenda," Bi Chola ambaye hajui umri wake halisi kwa sababu hana cheti cha kuzaliwa anasema.

Chanzo cha picha, Luxury Media Zambia
"Sikujua kama ningeweza kufanya hivyo katika umri huu."
Bi Chola anavaa nguo ambazo ni mchanganyiko wa rangi mahiri, muundo na mitindo.
Kuanzia jezi ya soka ya Marekani ya kijani, pamoja na magauni yenye rangi nyekundu aliyoyageuza kuwa kama sketi - katika rangi za bendera ya Zambia vazi alilovaa kutoa heshima kwa miaka 60 ya uhuru, hadi blauzi yenye rangi ya bluu, nyeusi na kijani iliyokatwa juu, na kukamilisha kwa mkufu wa nyoka wa dhahabu na bangili.

Chanzo cha picha, Luxury Media Zambia
"Sikuwahi kuvaa jinzi au wigi kabla - kwahivyo nilikuwa na furaha, na nilikuwa nikicheza."
Bi Kaumba, ambaye amekuwa mchapakazi tangu mwaka 2012, anasema kuwa bibi yake ana "ujasiri, neema - na alikuwa na muonekano wa kupendeza sana kwa kila picha".
Muonekano wote unaonyesha uzuri wake wa juu ya kidevu ambao unaonyesha furaha yake ya ujasiri, na ubora wa mchanganyiko wa rangi za mavazi yake.
Kinachoonekana zaidi kuvutia macho ni miwani yake mikubwa ya jua, kofia zenye ukubwa wa kupindukia, mikufu, bangili, pete, glavu, mifuko, na wigi zenye mvuto.
Ushawishi huo umetoka moja kwa moja kutoka kwa bibi yake, ambaye "daima amekuwa mpenzi wa lulu na bangili".
Katika eneo moja la kucheza linaloitwa GOAT, Bi Chola anaonekana akiwa na mbuzi ambaye amepambwa kwa lulu anazozipenda Bi Mbuya.

Chanzo cha picha, Luxury Media Zambia
Vito vingine pia vinaonyesha ubinadamu na hadithi ya maisha ya Chola.
Katika baadhi ya picha Mbuya anaonekana akishikilia redio yake anayoipenda ambayo huibeba karibu siku nzima na kulala nayo.
Au anashikilia "ibende" - fimbo ndefu ya mbao ambayo kwa miaka mingi amekuwa akitumia kutwanga mtama, mihogo au mahindi.
Anavuta kiko au kushikilia kikombe cha chuma kilichojaa chai, na kuning'inia kando ya mkono wa kiti ni "mbaula" au jiko la la mkaa ambalo Wazambia hutumia mara nyingi kupika – hasa wakati ambapo nchi inakabiliwa na kupunguzwa kwa uhaba wa umeme.

Chanzo cha picha, Luxury Media Zambia
Bi Kaumba ana matumaini kwamba mfululizo wa Granny utaangazia kwamba wazee bado wana mengi ya kukushirikisha jamii - na kufanya kumbukumbu na ni njia muhimu ya "kuacha muongozo kwa kizazi kijacho".
"Usiwapuuze, wapende mpaka mwisho kwasababu kumbuka tutakuwa kama wao siku moja."
Kutokana na kupigwa picha kwa Mbuya, Bi Kaumba ameajiriwa na wajukuu wanne kuwavalisha bibi zao - wenye umri kati ya miaka 70 na 96.
Bi Kaumba ana matumaini kwamba mfululizo wa Granny utaangazia kwamba wazee bado wana mengi ya kukushirikisha jamii - na kuweka njia muhimu ya "kuacha kumbukumbu kwa kizazi kijacho".
"Usiwapuuze, wapende mpaka mwisho kwasababu kumbuka tutakuwa kama wao siku moja."
Kutokana na kupigwa picha kwa Mbuya, Bi Kaumba ameajiriwa na wajukuu wanne kuwavalisha bibi zao - wenye umri kati ya miaka 70 na 96.

Chanzo cha picha, Luxury Media Zambia
Bi Chola alilelewa na babu na babu yake, akaenda shuleni hadi alipokuwa na umri wa miaka 12 au 13 kisha, kwa sababu za kiuchumi, akalazimishwa kuolewa na mwanamume mwenye umri wa miaka 30.
Alikuwa na watoto watatu, akaishia kunywa pombe kupita kiasi na hatimaye kutoroka ndoa.

Chanzo cha picha, Margret Chola alilazimika kuacha shule akiwa na umri wa miaka 12 au 13
Kiwewe hicho bado kinamsumbua - lakini umaarufu wake wa ulimwengu usiotarajiwa unampa sababu mpya ya kuishi.
"Sasa ninaweza kuamka nikijua kuwa watu duniani kote wanapenda kuniona," Chola anasema.
End of Unaweza pia kusoma:
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












