Vigodoro: Kwa nini baadhi ya watu Tanzania hupendelea vazi la ndani 'linalokuza' makalio?
Katika kile wanachokiita kujiongezea urembo ili kuonekana mlimbwende zaidi, baadhi ya wanawake jijini Dar es salaam na maeneo mengine ya miji mikuu ya nchi za Afrika Mashahariki wanalazimika kununua nguo za ndani maalumu, zenye kuongeza muonekano wa umbile la mwili, hususani makalio ili yawe na mvuto zaidi.
Nguo hizo za ndani ni maarufu kwa majina yasiyo rasmi ya vigodoro au vijuba.
Mwandishi wa BBC Martha Saranga alifuatilia na kuandaa taarifa ifuatayo.
Video : Eagan Salla