Ni nani hugharamia mavazi ya viongozi wa dunia na wenzi wao?

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Ido Vock
- Nafasi, BBC News
- Muda wa kusoma: Dakika 5
Sir Keir Starmer na mkewe Victoria walikubali michango ya nguo ili wawe na "muonekana mzuri" kuiwakilisha Uingereza, David Lammy amesema.
Alipoulizwa kuhusu michango hiyo, waziri huyo wa mambo ya nje alipendekeza mataifa mengine yalikuwa na bajeti kubwa ya mavazi ya viongozi inazofadhiliwa na walipa kodi.
Lammy alikuwa akijibu ripoti kwamba huenda Sir Keir alivunja sheria za bunge kwa kutotangaza hadharani nguo ambazo mkewe alinunuliwa na mfadhili wa chama cha Labour Lord Waheed Alli.
Aliiambia Sunday with Laura Kuenssberg: "Marais wa Marekani na wake wa rais wana bajeti kubwa, inayofadhiliwa na walipa kodi, ili waonekane vyema zaidi kwa niaba ya raia wa Marekani."
Kwa kweli, mke wa rais wa Marekani hana bajeti maalum ya mavazi - na wengi wao wamelalamikia gharama ya mtindo wa mavazi katika Ikulu ya White.
Marupurupu kwa rais - sio mke wake
Katika baadhi ya mataifa, walipa kodi huchangia gharama ya maisha ya viongozi wao - ambayo inaweza kujumuisha mavazi.
Marais wa Marekani wana bajeti ya takriban dola 50,000, ambayo inaweza kutumiwa kununua mavazi na vifaa vingine kando ma mshahara wa kila mwaka wa dola 400,000.
Lakini mke wa rais wa Marekani - hapokei mshahara wa kila mwaka au bajeti ya gharama zisizobadilika, ingawa wamelipa wafanyikazi na ofisi.
Hii ni licha ya kwamba mitindo wa mke wa rais wa Marekani hufuatiliwa kwa karibu.
Mifano mashuhuri ni pamoja na koti la Melania Trump la mwanamitindo Zara lililoandikwa “I REALLY DON’T CARE, DO U?”, alipotembelea kituo cha wahamiaji, na vazi jekundu la kuvutia la mbunifu wa mitindo Alexander McQueen lililovaliwa na Michelle Obama alipokutana na Rais wa zamani wa China Hu Jintao. .

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Baadhi ya wake wa rais wamesema kwamba, kwa ujumla, walitarajiwa kulipia nguo zao wenyewe.
Mke wa George W Bush, Laura Bush aliandika katika kumbukumbu yake ya 2010 kwamba "alishangazwa na idadi kubwa ya nguo za wabunifu wa mitindo ambazo nilitarajiwa kununua ... ili kukidhi matarajio ya mtindo Mke wa Rais".
"Baada ya mwaka wetu wa kwanza katika Ikulu ya White House, mhasibu wetu alimwambia George, 'Inagharimu sana kuwa rais,' na alikuwa akiangazia hasa nguo zangu," Bi Bush aliandika.
Afisa wa habari wa Michelle Obama, Joanna Rosholm, aliiambia CNBC mnamo 2014: "Bi Obama anagharamia mavazi yake."
Wake wa marais wa Marekani wanaweza pia kupokea nguo kama zawadi, mara nyingi kwa niaba ya serikali.
Baadhi ya wabunifu wa mitindo wanavutiwa umaarufa wanaopata zinaz nguo zao zinapovaliwa na mke wa rais.
Kwa kuwa bei za nguo za wabunifu wa mitindo zinaweza kufika maelfu dola kwa urahisi, michango ndiyo njia pekee ya wakazi wa Ikulu wasio na utajiri mkubw wanaweza kuvaa nguo za wabunifu nyota.
"Kwa hafla rasmi yenye umuhimu kwa umma au wa kihistoria, kama vile ziara ya serikali, nguo za mke wa rais zinaweza kutolewa kama zawadi na mbunifu na kukubaliwa kwa niaba ya serikali ya Marekani," Bi Rosholm alisema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Jumba la Makumbusho la Smithsonian linaorodhesha vazi ambalo mke wa rais wa sasa Jill Biden alivaa wakati wa kuapishwa kwa mumewe 2021 kama mchango wa mbunifu Alexandria O'Neil "kwa heshima ya mwanamke wa rais Jill Biden" - ishara kwa alimwazima na mbunifu wa mitindo.
Lakini mtangulizi wake Melania Trump, ambaye utajiri wa mumewe ulimfanya kuwa rais tajiri zaidi katika historia, alinunua mavazi yake ya siku ya kuapishwa kwa mumewe kutoka kwa Hervé Pierre.
Nchini Uingereza, Sarah Brown, mke wa waziri mkuu wa zamani Gordon Brown, amezungumza kuhusu ugumu wa kupokea zawadi - ikiwa ni pamoja na nguo - akiwa Downing Street.
"Ninapogundua haraka," aliandika katika kitabu chake cha 2011 Behind the Black Door, "hakuna uhaba wa wabunifu na wauzaji ambao watakupa nguo za bure.
“Hata hivyo, kuna sheria nyingi zinazoongoza kile ambacho wabunge (na wenzi wao) wanaweza kufanya kwa zawadi za bure – bila kusahau kipengele cha maadili cha kutumia nafasi yako kunyakua takrima.
Suluhisho alielezea: " Washauri wa afisi ya waziri mkuu na wanafaa kubuni njia ambayo itamridhisha kila mtu. Naweza kununua nguo zozote ambazo ninayotaka.
"Nguo au vito vyovyote vinavyotolewa bure, ninaweza 'kukodisha' kwa takriban asilimia 10 ya thamani yake kisha niirudishe."
Nchi zingine zinafanyaje?
Wake wa viongozi wa ulimwengu mahali pengine kwa ujumla huonekana kutegemea michango ya mitindo ya mavazi yao.
Brigitte Macron wa Ufaransa hana bajeti ya nguo inayofadhiliwa na serikali na anaaminika hukopeshwa na chapa maarufu ya mitindo ya Paris kama vile Louis Vuitton.
Kulingana na kitabu cha 2019 cha Madame La Présidente, ofisi yake huweka rekodi ya nguo ambazo amepewa na ambazo ni zake mwenyewe.
Lakini mume wake, Rais Emmanuel Macron, amekosolewa kwa matumizi yake mabaya ya pesa. Mwaka huu, gazeti moja lilifichua kwamba ofisi yake ilihifadhi kiti cha kiwango cha biashara kwenye ndege kutoka Paris hadi Brazil ili kusafirisha tu suti zake mbili, kwa gharama ya karibu euro 3,380.
Nchini Ujerumani, mawaziri walikosolewa kwa kutumia €450,000 kwa watengezaji nywele, wasanii wa vipodozi na wapiga picha katika miezi sita ya kwanza ya 2023, ingawa haionekani kuwa na hazina maalum ya mavazi.
Alipoulizwa kuhusu matamshi ya Lammy, msemaji wa Ofisi ya Mambo ya Nje alikataa kutoa maoni zaidi.
Downing Street ilisema kuhusu tamko la Sir Keir la michango ya nguo: "Tulitafuta ushauri kutoka kwa mamlaka juu ya kuja ofisini.
"Tuliamini tumekuwa tukizingatia, hata hivyo, kufuatia kuhojiwa zaidi mwezi huu, tumetangaza vitu zaidi."
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi na kuhaririwa na Yusuf Jumah












