Real Madrid na Man City mashakani? Jinsi Ligi ya Mabingwa Ulaya ilivyo kufikia sasa

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Guardiola na Carlo Ancelotti
Muda wa kusoma: Dakika 4

Je, Manchester City wanaweza kukosa kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa? Na Celtic, Arsenal, Aston Villa na Liverpool zinahitaji nini ili kutinga hatua ya muondoano?

Mechi tatu zimesalia katika awamu mpya ya ligi ya timu 36 ya Ligi ya Mabingwa iliyoboreshwa.

Nane bora watatinga robo fainali kuruka raundi ya muondoano ya awamu mbili.

Lakini, si kila mtu anafurahia muundo mpya wa ligi hiyo. Mabingwa wa Uingereza Manchester City wanajikuta katika nafasi ya 17 baada ya mechi tano.

Na, tukitazama chini zaidi, mabingwa watetezi Real Madrid na Paris St-Germain wanaweza kukosa kabisa katika awamu ya muondoano.

Nani atafuzu kwa awamu ya muondoano?

Hapa kuna ukumbusho kuhusu kile ambacho timu 36 za Awamu ya Ligi zinalenga.

Wale watakaomaliza katika nafasi nane bora watafuzu moja kwa moja hadi makundi ya 16 bora, ambapo watafuzu.

Watasubiri washindi wa mechi nane za mtoano wa mikondo miwili itakayoshirikisha vilabu vilivyoorodheshwa kutoka nambari tisa hadi 24.

Wale watakaomaliza kati ya nafasi ya tisa na 16 watakutana na timu iliyo nafasi ya 17 hadi 24, ikiwa na faida ya kucheza mkondo wa pili nyumbani.

Vilabu vitakavyokuwa nambari 25 kuendelea vitaondolewa na havitapata nafasi ya kushiriki Ligi ya Europa.

Je, ni pointi ngapi zinahitajika kufuzu

Kwa kuzingatia kwamba hili ni toleo jipya la ligi ya mabingwa Ulaya, inabakia kuonekana ni pointi ngapi zitahitajika ili kufikia mwisho wa nane bora, au kuepuka kuondolewa kwenye mashindano.

Kabla ya shindano la msimu huu, Opta ilikokotoa makadirio ya pointi za kila timu na uwezekano wa kusonga mbele .

Waligundua kuwa pointi 16 - uwezekano wa kushinda mara tano na sare moja kutoka kwa mechi nane - zingetoa nafasi ya 98% ya kumaliza katika nane bora.

Wakati huo huo, kufikia pointi 10 - ushindi wa mechi tatu na sare moja, kwa mfano - kunaweza kutoa nafasi ya 99% ya kupata nafasi ya 24 bora.

Hata hivyo, timu yoyote itakayokusanya chini ya pointi tisa itajipata imeondolewa katika mashindano hayo ya Ulaya msimu huu .

Ni klabu zipi zilizo kifua mbele na ni zipi zina kazi ya ziada?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Viongozi Liverpool ndio timu pekee inayojivunia rekodi nzuri baada ya mechi tano na, ikiwa na alama 15, kwa sasa ina uhakika wa angalau nafasi ya kushiriki.

Pengine tayari wana pointi za kutosha kufikia 16 za mwisho, pia. Kulingana Opta, pointi 15 zinatosha kutinga hatua ya nane bora kwa asilimia 73 .

Pointi mbili nyuma ya Liverpool ni Inter Milan, moja ya timu mbili ambazo hazijafungwa pamoja na Atalanta. Mabingwa hao wa Italia wako katika hali nzuri ya kufuzu hatua ya mtoani kama ilivyo kwa Barcelona, ​​Borussia Dortmund na Atalanta, ambao wote wametinga nane bora.

Arsenal wanashika nafasi ya saba baada ya ushindi mnono wa mabao 5-1 ugenini dhidi ya Sporting. Kwa pointi 10, The Gunners kuna uwezekano mkubwa kuwa tayari wanazo pointi za kutosha kwa angalau nafasi ya kushiriki.

Kikosi cha Mikel Arteta kiko kati ya Bayer Leverkusen na Monaco, waliotinga nane bora.

Aston Villa wako nafasi ya tisa kwa alama 10, nyuma ya Arsenal, Leverkusen na Monaco kwa tofauti ya mabao.

Kikosi cha Unai Emery kilianza kampeni yake kwa kushinda mechi tatu lakini tangu hapo kimeshindwa na Club Brugge na kutoka sare na Juventus.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pep Guardiola

Kuna timu nyingi kubwa nne ya nane bora, Bayern Munich ikishika nafasi ya 13, Atletico Madrid nafasi ya 15, AC Milan nafasi ya 16 na Juventus nafasi ya 19.

Labda klabu inayoshangaza zaidi kukosa kasi ni washindi wa 2022-23 Manchester City.

Opta iliwapa vijana wa Pep Guardiola nafasi ya asilimia 24.9 ya kubeba Ligi ya Mabingwa msimu huu mwezi Septemba, lakini City kwa sasa wanajikuta katika nafasi ya 17 wakiwa na pointi nane pekee katika michezo yao mitano.

Kulingana na Opta timu zilizo na alama nane katika hatua hii ziliepuka kuondolewa kwa 16% ya wakati huo.

Wakiwa na pointi tisa walifika raundi iliyofuata kwa 69% ya muda huo na wakiwa na pointi 10 walisonga mbele katika 99% ya kura zilizokamilika.

Pia walio na pointi nane ni mabingwa wa Uskochi Celtic, ambao wanatarajia kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2012-13.

Washindi mara 15 Real Madrid kwa sasa wanashikilia nafasi ya mwisho ya kufuzu katika nafasi ya 24. Los Blancos wana pointi sita pekee, wakiwa wamepoteza mechi tatu kati ya tano.

Paris St-Germain ndio jina kubwa zaidi miongoni mwa timu zitakazoondolewa, wakiwa pointi mbili mbali na Madrid, baada ya kushinda mechi moja pekee ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Imetafsiriwa na Seif Abdalla na kuhaririwa na Ambia Hirsi