Arsenal vs Liverpool: Je, Gunners wanaingia kwenye mechi wakiwa chini ya Liverpool? Na je, Salah atatamba leo?

Muda wa kusoma: Dakika 7

Bado ni mapema katika msimu wa ligii kuu ya England wa 2024/25, lakini Arsenal watakapochuana na Liverpool Jumapili hii, wengi wanahisi kwamba mechi hiyo itakuwa na uzito mkubwa kwenye kinyang’anyiro cha ushindi wa taji la ligi hiyo.

Liverpool almaarufu kama The Reds wako nambari mbili kwenye jedwali ya ligi hiyo wakiwa na alama 21, pointi nne juu ya Arsenal almaarufu The Gunners. Ikiwa Liverpool watashinda, watapanda kileleni na kukiacha kikosi cha Mikel Arteta kwa alama saba chini yao.

Takwimu muhimu ni zipi, na mechi hiyo itakayosakatwa kwenye uga wa Emirates itashindiwa wapi? BBC Sports inaangazia hilo.

Je, Arsenal wanapaswa kuwa na wasiwasi kuhusu Liverpool?

Arsenal wakiwa na baadhi ya wachezaji wenye majeraha na timu ya Liverpool kuwa katika fomu nzuri, mlinzi wa timu ya Mancehster City Nedum Onuoha anaamini kwamba Arsenal wanaingia kwenye mechi hii wakiwa chini ya Liverpool, ila anaamini pia kwamba ni nafasi ambayo huenda ikawafaa.

“Je, Mikel Arteta anapaswa kuwa na waiswasi? Sidhani anapaswa kuhisi hivyo,” alisema kwenye kipindi cha Plane Premier League podcast.

“Ninadhani anaelewa umuhimu wa mwanzo wa msimu, lakini anaelewa zaidi umuhimu wa jinsi ya kumaliza vyema msimu.

“Masikitiko ya kushindwa na Bournemouth yatakuwa makubwa, lakini timu zenye wachezaji na wakufunzi wazuri – mimi huwafurahia sana baada ya wao kushindwa.

“Kwamba watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Liverpool, na katika hali ngumu ya wao kuhisi kuwa chini ya wapinzani wao wakiwa nyumbani – ninadhani inawafaa kwani ni hali ambayo wanapaswa kuwa kwa sasa.

“Mashabiki watalikubali hilo, wachezaji pia, na wakiweza kupata ushindi itakuwa imewapiga jeki na kuwapa motisha ambao hawakuhisi wanauhitaji kwa sasa, lakini hatua hiyo itakapokuja itakuwa asilimia mia.”

Liverpool wamepoteza mechi moja msimu huu – walipofungwa bao moja kwa nunge na Nottingham Forest – na kushinda mechi zote zilizofuatia.

Meneja wa zamani wa Chelsea na Brighton Grahama Potter anaamini kwamba utabiri wa Arne Slot umekuwa jambo kuu kwa fomu njema wanayoonyesha Liverpool.

“Alichokifanya ni kuhakikisha kwamba Liverpool ipo imara na dhabiti,” amesema Potter.

“Mchezo wao umabadilika hatua kwa hatua – wanajikusanya na kuendelea mbele kwa sasa. Itakuwa muhimu sana kuona ikiwa watadumisha hali hiyo.”

Kuhusu mechi ya Jumapili, Potter ameongezea kwamba,” Ninahisi watatoka sare.”

Je Arsenal wataanza kwa kasi tena?

Mechi huenda ikawa ngumu kwa Arsenal ila wanatabia ya kuanza kwa kasi dhidi ya The Reds – katika mechi nne za awali za ligi kuu ya England kati ya The Gunners dhidi ya The reds, Arsenal wamefunga bao za mapema katika dakika 15 za kwanza.

Katika mechi hizo, nusu yazo Arsenal wamenyakuwa alama zote tatu, na walishinda mchuano wa hivi maajuzi dhidi ya Liverpool mnamo Februari kwa mabao 3-1 baada ya Bukayo Saka kufunga bao la mapema kwenye dakika ya 14.

Lakini japo wamefanikiwa kufunga mabao ya mapema dhidi ya Liverpool kwenye mechi za hivi maajuzi, hawajakuwa na haraka iyo hiyo kuzuia mabao msimu huu.

Wamefunga mabao 15 katika mechi 8 za Ligi kuu ya England, lakini zote hizo hazijafungwa kwenye dakika 15 za mwanzo wa mechi.

Ulinzi wa Liverpool ni dhabiti na itakuwa kibarua kigumu kuuvunja

Mwanzo wa mechi kwa kasi dhidi ya Liverpool kunaweza kuwa rahisi kimatamshi wala sio kwa vitendo, huku Arne Slot akiwa amefanya mabadiliko ya kutajika kwenye safu ya ulinzi ya The Reds.

Japo vikosi vya Liverpool alivyosimamia Jurgen Klopp vilicheza mchezo mkali wa kutafuta kufunga mabao zaidi, Slot ana utulivu kiasi na hali hiyo imechangia wao kufungwa mabao matatu pekee na kutofungwa hata bao moja kwenye mechi tano katika mechi nane – nusu ya idadi hii wameweza kutimiza katika msimu uliopita.

Kwa jumla, Liverpool wanafungwa mabao 0.38 kwa kila mechi kwenya kampeni yao msimu huu, ikilinganishwa na mabao 1.08 msimu uliopita.

Inaweza kutajwa kwamba matokao mazuri ya Liverpool yanatokana kwa kiasi kikubwa na orodha ya mechi walizocheza, na timu walizokabiliana nazo ambazo zipo chini kwenye jedwali.

Lakini wikendi iliyopita, walikabiliana na Chelsea ambao fomu yao ni nzuri na kupita mtihani huo kwa tundu la sindani walipowaadhibu mabao 2 kwa moja, hali inayoashiria kwamba wamejiandaa kwa mechi ngumu zinazokuja.

Changamoto ya ulinzi kwa 'The Gunners'

Kwa uhakika, kuna njia ndefu inayoangaziwa mbele kabla ya taji la Ligi kuu ya England kuamuliwa, ila kwa The Gunners, wanajipata katika hali inayokuwa mtihani mkubwa kwao kwenye msimu huu.

Arteta amekumbwa na changamoto ya wachezaji wenye majeraha – Kapteni/Kinara Martin Odegaard hajacheza tangu Arsenal kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Brighton mwishoni mwa Agosti baada ya kupata jeraha la mguuni akiichezea timu ya taifa ya Norway.

Bukayo Saka amekosa mechi mbili zilizopita akiuguza jeraha kwenye goti alilolipata akiichezea timu ya taifa ya England, huku Mlinzi Riccardo Calafiori akijikwaa mguuni kwenye mechi ya ligi kuu ya mabingwa wa ulaya walipoishinnda Shaktar Donetsk ya Ukraine.

Kukanyanga mambo, Arsenal hawana mlinzi William Saliba aliyepata kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Bournemouth na takwimu zinaashiria kwamba hili huenda likawa tatizo kubwa kwao.

The Gunners, wana nafasi za ushindi asilimia 74 wakiwa na mlinzi huyo, ilikinganishwa na asilimia 45.5 wakiwa hawana Saliba uwanjani.

JEWDALI

Rekodi ya Arsenal tangu mwanzo wa msimu wa 2022-23 kwenye Ligi Kuu ya England.

Michuano Wakiwa na Saliba Bila ya Saliba

Mechi 73 11

Ushundi kwa asilimia (%) 74 45.5

Alama kwa mechi 2.4 1.6

Mabao kwa mechi 0.8 1.6

xG dhidi ya kila mechi 0.8 1.4

Chanzo: Opta

Masuala ya Ulinzi yana maana kwamba Jakub Kiwior huenda akajumuishwa kama beki wa kati cha kati akiwa na Gabriel huku Myles Lewis - Skelly mwenye umri wa miaka 18 ambaye aliingia katika nafasi ya Calafiori mapema wiki hii akiwa chaguo jingine.

“Ni jambo muhimu kwa sababu Arsenal inakumbwa na wakati wa kwanza katika muda mrefu ambapo kikosi chake hakiko thabiti huku wachezaji wakuu wakiwa nje,’ amesema Potter kwenye kipindi cha Planet Premier League.

“Itakuwa muhimu kuona jinsi watakabiliana na changamoto hiyo.”

The Gunners watafurahi, angalau kuwa Gabriel Martinelli atakuwa katika fomu nzuri ya kucheza.

Amehusika kwenye kuchangia kufungwa kwa mabao mengi dhidi ya Liverpool (mabao 7 – matano, na kuchangia kufungwa kwa mawili) kuliko mechi dhidi ya timu nyingine tangu kuwasili kwake Arsenal mnamo 2019.

Salah anawiri na kung’aa tena

Mohammed Salah ni mwenye umri wa miaka 32, lakini amekuwa kiungo muhimu kabisa kwenye kikosi cha ushambulizi cha Liverpool.

Alifunga bao kwenye mechi ya wiki iliyopita dhidi ya Chelsea na kuchangia kufungwa kwa bao la Curtis Jones la ushindi.

Ni Erling Haaland, Bryana Mbeumo na Cole Palmer wamefunga mabao zaidi, huku Saka akichangia kufungwa kwa mabao zaidi.

Na dhidi ya timu kubwa sita, Salah huwajibika na kufanya vyema kwenye mechi hizo.

Mshambulizi huyo kutoka Misri, ana jumla ya mabao 61 na kuchangia kufungwa mabao 72 katika mechi alizocheza dhidi ya Arsenal, Chelsea, mancehster City, Manchester United na Tottenham.

Ni mchezaji Alan Shearer pekee mwenye idadi kubwa kwenye mechi za ligi kuu ya England dhidi ya timu hizo - kwa pamoja na Liverpool akiwa na mabao 75 na kuchangia mengine 129.

Imetafsiriwa na Laillah Mohammed na kuhaririwa na Asha Juma