Elon Musk: Jinsi mtu tajiri zaidi duniani alivyonunua Twitter

Elon Musk

Chanzo cha picha, Reuters

Ilikuwa jioni tulivu mwishoni mwa Machi huko San Jose.

Mkutano ulioandaliwa kwa haraka ulikuwa umepangwa katika Airbnb ili kumkaribisha mtu tajiri zaidi duniani.

Mkutano huo ulikuwa wa hadhi ya juu kwa Twitter.

Hivi karibuni Elon Musk alikuwa mwanahisa mkubwa zaidi wa Twitter.

Sasa kulikuwa na mazungumzo kwamba anataka kujiunga na bodi ya kampuni.

Wakati mwenyekiti wa Twitter, Bret Taylor, alipowasili katika ukumbi huo haikuwa kile alichokuwa akitarajia.

Hii "inaongoza kwa sehemu ya ajabu ambayo nimewahi kufanya mkutano hivi karibuni", inasemekana alimtumia ujumbe Bw Musk.

"Nadhani walikuwa wakitafuta Airbnb karibu na uwanja wa ndege na kuna matrekta na punda," alimwambia.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hata hivyo, mkutano ulifanyika vizuri. Siku chache baadaye ilitangazwa kuwa Bw Musk atajiunga na bodi ya Twitter.

Huo ulikuwa mwanzo tu. Miezi sita iliyofuata ingeshuhudia moja ya mikataba ya kichaa zaidi, isiyo ya kawaida katika historia ya Silicon Valley.

Mwanzoni mwa Aprili, Bw Musk alionekana kufurahishwa na msimamo wake wa bodi kwenye Twitter, akitweet mara kwa mara kuhusu jinsi kampuni inaweza kubadilika.

Mnamo tarehe 14 Aprili, bilionea huyo alisema hadharani kwamba alitaka kununua Twitter - kufuli, hisa na pipa. Alitoa $44bn (£38bn) kwa Twitter katika kuipokea au kuiacha.

Bodi ya Twitter hapo awali ilikataa ofa hiyo, hata ikaunda kifungu cha "kidonge cha sumu" ili kujaribu kumzuia Bw Musk kuinunua kampuni hiyo kwa lazima.

Kisha akabadili moyo (sio mara ya kwanza katika hadithi hii). Bodi ya Twitter baada ya kutafakari iliamua mpango huo na mnamo Aprili 25, Twitter ilitangaza kuwa wamekubali ofa hiyo.

"Yessss" Bw Musk alitweet.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 1

Bw Musk alidai kuwa Twitter ilikuwa imepotea njia.

Alisema Twitter mara nyingi ilizuia hotuba na, kama "ukumbi wa jiji" duniani, ilihitaji kuweka uhuru wa kujieleza zaidi ya yote.

Alisema hakujali kuhusu "uchumi hata kidogo" katika mahojiano katika mkutano wa TED2022 huko Vancouver, Canada.

Hiyo ilikuwa bahati, kwa sababu wiki na miezi baada ya mpango huo hisa za teknolojia zilishuka.

Thamani ya Twitter pia ilipungua. Hivi karibuni, wachambuzi wengi walianza kuhoji ikiwa Bw Musk alikuwa amelipa zaidi kwa Twitter.

Alianza kuuliza hadharani maswali tofauti - kuna akaunti ngapi za kweli kwenye Twitter?

Bilionea huyo - aliyeorodheshwa na Forbes na Bloomberg kama mtu tajiri zaidi duniani, mwenye utajiri wa takriban dola bilioni 250 sawa na (£216bn) - kwa miaka mingi alikuwa akilalamika kuhusu idadi ya akaunti zisizo halisi kwenye jukwaa hilo.

Baada ya ofa yake kukubaliwa, aliuliza mara kwa mara Twitter kutoa data kuhusu watumiaji wangapi halisi.

Wasimamizi wa Twitter walitoa takwimu zilizokuwa chini ya 5% ya watumiaji halisi wa kila siku, kulingana na makadirio kutoka kwa sampuli za akaunti, zilikuwa feki.

HiliIlionekana kumkasirisha Bw Musk. Baada ya mazungumzo marefu ya Twitter kutoka kwa Bw Agrawal, akielezea jinsi kampuni hiyo ilivyofikia idadi hiyo, Bw Musk alijibu kwa emoji ya kinyesi.

Elon Musk's

Chanzo cha picha, Getty Images

Mpango huo ulikuwa ukisambaratika. Sio kwamba haikutarajiwa kabisa, mnamo tarehe 8 Julai, Bw Musk alitangaza kuwa anataka kujiondoa kwenye mpango huo

Je, alikuwa akijaribu kupata bei nzuri kutoka kwa kampuni au alimaanisha kweli kujiondoa? Ilikuwa vigumu kubaini.

Twitter haikutaka kabisa kusikia mchezo huo. Ilidai kuwa makubaliano ya Bw Musk ya kununua kampuni hiyo yalikuwa ya lazima kisheria na hakuwa nachaguo la kutengua mpango huo.

Huku pande zote mbili zikijihami kwa mawakili wa ngazi ya juu waliolipwa donge nono, tarehe ya mahakama iliwekwa mjini Delaware, tarehe 17 Oktoba kuamua iwapo Bw Musk atalazimishwa kununua kampuni hiyo.

Katika nyaraka za mahakama, Twitter ilisema kuwa ilikuwa imempa taarifa za kutosha kuhusu idadi ya watumiaji halisi iliyokuwa nayo.

Bw Musk alisema Twitter huenda ina watumiaji hewa wengi kuliko ilivyodai hadharani, na hata kuishutumu kampuni hiyo kwa udanganyifu.

Ukosoaji huo wa umma ulikuwa ikiathiri Twitter. Sehemu kubwa ya mapato ya Twitter yanatokana na matangazo na watangazaji walianza kushangaa ni matangazo mangapi yaliyokuwa yakionyeshwa kwa watu watumiaji halisi.

Mchakato huo ulisumbua sana katika Makao Makuu ya Twitter pia.

Baadhi ya wafanyakazi walifurahia wazo la Bw Musk kuwa Mkurugenzi Mtendaji wao.

Wengi kwa faragha - na wengine hadharani - walisema ununuzi wake utakuwa janga kwa udhibiti wa maudhui na malengo mapana ya kampuni.

Bw Musk, Twitter, hakimu na waandishi wa habari, wote walikuwa wakijiandaa kwa kile kilichoonekana kama kesi ya kuepukika mahakamani wakati mabadiliko mengine ya ajabu yalipotokea.

Baada ya kutoa kila aina ya madai dhidi ya Twitter, Bw Musk ghafla alitangaza mpango huo umeanza tena. "Kununua Twitter ni kuongeza kasi ya kuunda X, programu ya kila kitu," alisema.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 2

Ni nini ilimfanya abadili mawazo yake? Labda alifikiri atapoteza kesi yake mahakamani.

Siku chache kabla ya kutangaza uamuzi huo, alitarajiwa kutia saini makubaliano ya nje ya mahakama na mawakili wa Twitter.

Labda alitaka kuepuka maswali ambayo yangekuwa ya kuchosha na yanayoweza kufichua. Kwa sababu yoyote, unaweza kuona kwa nini Twitter haikukimbilia kusherehekea ushindi dhidi ya Musk hasa baada ya ''kuumwa na nyoka mara mbili''.... ndio maana ilikaa kimya yote haya yakifanyika.

Bw Taylor alituma ujumbe wa Twitter kuwa kampuni hiyo "imejitolea kufunga shughuli ya bei na masharti waliyokubaliana na Bw Musk".

Twitter pia iliomba kesi hiyo iahirishwe, sio kufutwa. Mawakili wa Bw Musk walijibu kwamba Twitter "haitakubali ndiyo kuwa jibu".

Bw Musk alikuwa na hadi saa tisa ya tarehe 28 Oktoba kutoa pesa.

Mabilioni yalitolewa na marafiki zake matajiri na benki. Iliyobaki, kutoka kwa Bw Musk, kwa kuuza baadhi ya hisa zake huko Tesla.

Makubaliano ambayo nyakati fulani yalionekana kuwa magumu, yasiyowezekana kuvunjika, sasa yamekamilika.