Kombe la Dunia 2022: Je Morocco inaweza kuipatia ushindi Afrika?

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika msururu wa barua zetu kutoka kwa waandishi wa Afrika mwandishi wa habari Maher Mezahi anaangalia fursa ya ushindi wa Kombe la Dunia , na hatimaye kutimimizwa kwa ubashiri wa Pele.

Sherehe kubwa zaidi duniani ilifanyika katika uwanja wa Education City mjini Doha Jumanne usiku wakati Morocco ilipoishinda Uhispania katika awamu ya 16 ya michuano ya Kombe la Dunia la Fifa 2022 Fifa .

 Wengi wa umati wa mashabiki 44,000 waligubikwa na hisia baada ya mlinzi wa Morocco Achraf Hakimi kuipatia ushindi kwa mkwaju wa penati.

 Wamorocco walimwagika kwenye mitaa ya miji ya Casablanca, Rabat, Marrakesh, na kila mji mkuu wa Ulaya Magharibi kusherehekea ushindi huo.

Hata mfalme Mohamed VI alijiunga na umati wa watu waliokuwa wakisherehekea.

 Baada ya timu kudensi , kukumbatiana na kulia katika chumba cha kuvaa, kocha Walid Regragui alitangaza tangazo muhimu sana katika mkutano na wandishi wa habari.

"Katika wakati mmoja barani Afrika, tunapaswa kuwa na matamanio na ni kwanini tusishinde Kombe la Dunia, hata kama itakuwa vigumu," alisema.

Sio kwamba tu alipata mafanikio katika bara, baada ya kuifunza timu ya soka ya nyumbani nchini Morocco tu, bali alikuwa ni sehemu ya uzinduzi wa darasa la makocha la Caf la mwaka 2018 -kikundi cha kwanza kabisa cha makocha waliopata diploma ya kwanza ya juu zaidi ya soka katika bara la Afrika.

Anawakilisha kila kitu sahihi katika soka la Afrika: Ni kijana, mwenye ujuzi, asiye na uoga na Mwana Afrika anayeipenda kwa moyo wake wote.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kocha mkuu wa Morocco Walid Regragui amekuwa kiongozi bora kwa timu yake.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Aliou Cissé wa senegal, Djamel Belmadi wa Algeria, Radhi Jaidi wa Tunisia na Benni McCarthy wa Afrika Kusini ni mifano mingine ya makocha wapya wa Afrika wa aina yake.

Sio jambo la ajabu kwamba Kome la Dunia 2022 , ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mataifa ya Afrika kulikuwa na makocha wa kiafrika kuongoza timu zao.

Lakini Regragui yuko sahihi? Afrika inapaswa kujiuliza yenyewe iwapo inaweza kushinda Kombe la Dunia?

Kama mwandishi wa habari wa soka wa Kiafrika, mara nyingi huwa ninakuwa na hofu wiki moja kabla ya Makombe ya Dunia kwasababu, bila kushindwa, walau chombokimoja cha habari kitaniuliza kuhusu ubashiri wa Pele wa miaka ya 1970 kwamba timu ya Afrika inaweza kushinda shindao hilo kabla ya mwaka 2000.

 Miaka ya nyuma, nilikuwa nikijibu kuwa Pele alisema mambo mengi ambayo sio lazima kwamba yalikuwa na maana sana, na inaishia hapo.

Mwaka huu hatahivyo, ninaweza kuangalia upya tena jibu langu.

 Mwezi Novemba, tangazo la rais wa shirikisho la soka la Cameroon Samuel Eto'o kwamba alitarajia Cameroon iichape Morocco katika fainali za mataifa ya Afrika.

 Mara moja alidhihakiwa mtandaoni, hasa na raia wenzake wa Cameroon, lakini kauli yake ilinipa wazo tofauti – iliyonifaya kuwa mdadisi zaidi.

 "Ni nini kilizuia timu ya Afrika kushinda Kombe la Dunia katika miaka iliyopita?" Nilijiuliza.

Tatizo lilianza na ukoloni katika bara.

Kwa bahati mbaya ukweli ni kwamba katika makombe yote saba ya dunia yaliyofanyika kuanzia 1930 hadi 1962, ni Misri pekee iliyoliwakilisha bara katika mwaka 1934.

 Hilo ni sehemu ya ukatili wa kikoloni wa bara uliofanywa na mataifa ya Ulaya magharibi, na pia ni kutokana na wakuu wa zamani wa Fifa waliokataa kuipatia Afrika nafasi ya moja kwa moja katika shindano , hata mataifa ambayo yalikuwa yamepata uhuru.

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Afrika imepokea mashindano ya Kombe la Dunia mara moja – katika Afrika Kusini mwaka 2010.

Katika mwaka 1966, bara la Afrika lilisusia Kombe la dunia nchini Uingereza ili kutuma ujumbe kwa Fifa kwamba inataka kupewa nafasi katika shindano hilo, nafasi ambayo iliipata katika mwaka 1970.

 Kwa kipindi cha miongo mitatu iliyofuata, timu za Afrika ziliweza vyema kuonyesha ushindi, ukiwemo ushindi wa Algeria dhidi ya Ujerumani Magharibi, Morocco dhidi ya Ureno na Cameroon dhidi ya Argentina.

Licha ya hili, Fifa iliendelea kujivuta, na kuyapatia mataifa mwawili ya Kiafrika nafasi mbili tu pekee katika mwaka 1982, nafasi tatu mwaka 1994, na nafasi tano katika mwaka 1998.

Kwahiyo sababu moja kuhusu ni kwanini bado Afrika haijashinda Kombe la dunia ni kwamba imeshiriki mashindano hayo mara chache.

Baadhi wanaweza kuzungumzia matokeo mabaya katika kipindi cha miaka 12 iliyopita, lakini ni nani alisema kwamba kuongezwa kwa ushiriki kungepelekea kuongezeka kwa ushindani na mafanikio?

Pesa ya ushindi kwa kushiriki katika Kobe la Dunia ingeingizwa katika soka la mashinani kote barani Afrika , na kuboresha kwa kiasi kikubwa ubora wa mchezo.

 Karibu karne moja baada ya kuzinduliwa kwa Kombe la Dunia nchini Uruguay, hatimaye Afrika itapewa fursa zaidi, wakati itakapopewa nafasi 9.5 katika mwaka 2026.

Kombe la Dunia la mwaka 2022 pia limetuonyesha kwamba ukosefu wa uwakilishwaji, sio tu kwa nafasi za kufuzu, lakini pia katika haki ya kupokea shindano, unaweza kuwa na ushawishi wa hali ya juu kimchezo.

 Korea Kusini ilifikia nusu fainali mwaka 2002 wakati ilipopokea mashindano hayo na , huku Black Stars wa Ghana wakiondolewa kwa mikwaju ya penati katika nusu fainali mwaka 2010 katika mashindano ya kwanza ya Kombe la Dunia la Afrika yaliyofanyika nchini Afrika Kusini.

 Si jambo la ajabu kwamba timu hizi mbili za Asia na Afrika zilifanya vyema zaidi kuliko miaka yote wakati mabara yao yalipopokea shindano?

 Kombe la dunia la 2022 limetuonyesha kuwa jibu ni : huenda sio.

Nchi tatu za Asia zilifuzu kwa awamu za mchujo mwaka huu, na Kombe la Dunia la Qatar, limekuwa shindano lenye mafanikio makubwa sana kuwahi kushuhudiwa Afrika.

 Jumla ya pointi 24 kwa ujumla katika mechi za makundi 15 zilivunja rekodi ya awali ya pointi 15 katika Kombe la Dunia la mwaka 2002.

G

Chanzo cha picha, Maher Mezai

Maelezo ya picha, Morocco inaamini kwamba wana dakika 270 kabla ya kuwa washindi wa dunia. Huenda umefika muda pia kwetu kuwaamini ", anasema mwandishi Maher Mezai

Cameroon ilikuwa ni nchi ya kwanza ya Afrika kuichapa Brazil katika Kombe la Dunia, Tunia ilipata ushindi dhidi ya Ufaransa, na Morocco ikawa nchi ya kwanza ya Afrika kushinda katika kundi, ikiwa na pointi zake saba.

 Kuona mashabiki - Wasaudia, Wamorocco na Watunisia Saudia wakishangilia ushindi wa timu zao limekuwa ni jambo la kufurahisha.

 La kufurahisha zaidi katika "kero za Kombe la Dunia" litakuwa ni iwapo Morocco itaweza kutekeleza maneno ya kocha wao Regragui kivitendo na kushinda shindano.

Ukiangalia jinsi safu yao ya ulinzi ilivyolinda na jinsi mlinda lango wao Yassine Bono alivyo, kila mara watakuwa na nafasi katika kombe la Dunia.

 Morocco inaamini kuwa wako katika dakika ya 270 kufikia kuwa washindi wa duni. Huenda umefika wakati na sisi pia tuwaamini.