Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 08.12.2022

Chanzo cha picha, Getty Images
Winga wa PSV na Uholanzi Cody Gakpo, 23, anasema "angefikiria" kuhusu kujiunga na Manchester United, lakini hajawasiliana na klabu hiyo ya Ligi ya Premia. (NRC - in Dutch)
Tottenham na Liverpool wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Morocco Sofyan Amrabat, 26, kutoka Fiorentina dirisha la uhamisho litakapofunguliwa Januari. (90min)

Chanzo cha picha, Getty Images
AC Milan wanaweza kuwa tayari kushindana na Barcelona kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Brazil Gabriel Martinelli, 21, iwapo wataamua kumuuza winga wa Ureno Rafael Leao, 23, mwezi Januari. (Calciomercato - in Italian)
Arsenal huenda ikalazimika kuahirisha mpango wao wa kumnunua winga wa Shakhtar Donetsk na Ukraine Mykhailo Mudryk, 21, baada ya kuumia kwa mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 27, anasema angependa kucheza katika Ligi ya Premia. Mkataba wa mchezaji huyo anayelengwa na Manchester United katika klabu ya Juventus unamalizika mwaka wa 2023. (Express)
Bayern Munich wanatazamia kumpa mshambuliaji wa Ujerumani Jamal Musiala, 19, mkataba mpya. (Bild - in German)
Marseille wanataka kumsajili mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 30, kutoka Crystal Palace mkataba wake utakapokamilika 2023. (90min)

Chanzo cha picha, Reuters
Meneja Eddie Howe anasema Kanuni za Udhibiti wa Matumizi yaani financial fair play (FFP) huenda ikapunguza matumizi ya Newcastle katika dirisha la uhamisho la Januari. (Mail)
Roma wako kwenye mazungumzo ya kina na wakala wa mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay, 28, kuhusu kuhama kutoka Barcelona.(Sport - in Spanish)

Chanzo cha picha, BBC Sport
Atletico Madrid wako tayari kusikiliza ofa kwa mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 23, ambaye anataka kuondoka katika klabu hiyo. (TVE, via Mail)
West Ham wanataka kusajili mshambuliaji mpya katika dirisha la uhamisho la Januari. (Sun)
Meneja wa timu ya taifa ya wanaume ya Marekani Gregg Berhalter atafanya mazungumzo kuhusu mkataba mpya. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi wa akademi ya Arsenal Per Mertesacker anaweza kuajiriwa na chama cha soka cha Ujerumani kuwa mkurugenzi wao mpya wa michezo. (Sky Germany, via Mail)
Arsenal, Barcelona na Paris St-Germain wana nia ya kumsajili winga wa Palmeiras na Brazil Estevao Willian mwenye umri wa miaka 15. (Goal)















