Mchezaji aliyechukua nafasi ya Cristiano Ronaldo - Goncalo Ramos ni nani?

.

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Ureno Goncalo Ramos?

Kabla ya kuanza kwa mechi, mazungumzo yote yalikuwa juu ya Cristiano Ronaldo kuachwa nje. Kufikia wakati wa kupulizwa kipenga cha mwisho , watu waote walikuwa wakimzungumzia Goncalo Ramos.

Kamera zielekezwa kwa mtu mwenye rekodi ya mfungaji bora wa muda wote wa Ureno, ambaye hisia zake za kubadilishwa wakati wa mechi ya awali ya taifa lake zilimkasirisha meneja Fernando Santos, alipochukua nafasi yake miongoni mwa wachezaji wa akiba katika mechi ya hatua ya 16 bora dhidi ya Uswizi kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar. .

Benchi hilo lilizungukwa na wapiga picha waliokuwa na hamu ya kupiga picha ya Ronaldo ambaye hajaridhika, hayupo kwenye kikosi cha kwanza cha Ureno kwenye michuano mikubwa kwa mara ya kwanza tangu 2008.

Lakini umakini ulibadilika na kuwa uwanjani, kwani mbadala wake mwenye umri wa miaka 21 alinyakua nafasi yake kwa kufunga hat-trick katika matokeo ya ushindi wa 6-1.

Utangulizi wa Kombe la Dunia wa kukumbuka

Kocha wa Ureno Santos alipochukua uamuzi wa kumweka Ronaldo kwenye benchi kwenye mechi hiyo, hakuwa na matumaini ya matokeo bora.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 1

Fowadi huyo wa Benfica alihitaji dakika 17 tu kujitangaza akiwa Qatar alipogusa mpira mara moja kabla ya kupiga mpira uliompita kipa wa Uswizi, Yann Sommer .

Muda mfupi baada ya kipindi cha mapumziko alifunga bao la pili, akipenya kwenye lango na kukutana na krosi ya chini ya Diogo Dalot ambapo alifanya matokeo kuwa 3-0.

Pasi ya bila kuangalia ilimfikia Raphael Guerreiro, kabla ya Ramos kufunga goli lake la tatu – ikiwa hatrick ya kwanza katika Kombe hili la Dunia.

Alibadilishwa baada ya dakika 74, alimaliza mechi akiwa amepiga mashuti mengi zaidi (sita), mashuti yaliyolenga lango (matano) na miguso kwenye eneo la hatari (sita), pamoja na mabao yake matatu kutoka kwa mabao yaliyotarajiwa ya 1.28.

Wakati Ramos akitolewa, kipa wa zamani wa Uingereza Robert Green alisema kwenye BBC Radio 5 Live: "Hilo lilikuwa jambo la kustaajabisha na Goncalo Ramos. Uchezaji wa Kombe la Dunia hadi sasa, pamoja na kila kitu kilichoendelea."

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 2

Ramos ni nani?

Wakati Ronaldo, akiwa na mabao manane ya Kombe la Dunia, bado hajafunga katika mechi sita za mtoano kwa Ureno kwenye michuano hiyo, Ramos tayari ana matatu.

Ramos, ambaye aliimarika kupitia mfumo wa vijana wa Benfica, alikuwa ameichezea Ureno jumla ya dakika 33 katika mechi tatu alizoichezea nchi yake kabla ya kukutana na Uswizi siku ya Jumanne.

Hilo lilijumuisha bao moja katika mechi ya kirafiki la dakika 23 dhidi ya Nigeria mnamo Novemba, kabla ya dakika mbili na dakika nane katika mechi za kundi dhidi ya Ghana na Uruguay mtawalia.

Kisha akabaki kama mchezaji ambaye hakutumika wakati ambapo Ureno iliopoteza dhidi ya Korea Kusini tayari ilikuwa imefuzu.

Hatahivyo, baada ya kuichezea timu yake 7kwa mara ya kwanza katika hatua ya mtoano ya kombe la Dunia, alionesha mchezo ambao ulimfanya kuonekana kwamba amekuwa akifanya hivyo kwa miaka mingi.

Nini kinafuata kwa Ronaldo?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Alipoulizwa kuhusu Ronaldo baada ya mechi kukamilika, Ramos alisema: "Cristiano Ronaldo anazungumza nami na kila mtu katika timu. Yeye ni kiongozi wetu na daima anajaribu kusaidia."

Mwisho wa mfululizo wa mechi 31 za mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid, Juventus na Manchester United kuanzishwa kwenye michuano mikubwa nchini mwake ulikuwa habari kuu.

Kwa kuzingatia ushawishi wa Ramos, hakuna uhakika kwamba Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 atarejesha nafasi yake ya kuanza dhidi ya Morocco Jumamosi.

Kocha wa Ureno, Santos alisema "hakupenda" jinsi Ronaldo alivyochukulia baada ya kubadilishwa baada ya dakika 65 za kushindwa na Korea Kusini katika mchezo wa mwisho wa kundi, ambao ulilinganishwa na jinsi muda wake wa kucheza Manchester United ulimalizika ghafla mwezi uliopita.

Mshindi huyo mara tano wa Ballon d'Or alikana kuelekeza hasira kwa kocha wake lakini, hata hivyo, alijikuta miongoni mwa wachezaji wa akiba dhidi ya Uswizi.

Baada ya kuwa mwanamume wa kwanza kufunga katika Fainali tano za Kombe la Dunia mapema katika michuano hiyo, kiwango cha mchezo wake kitamlazimu Ronaldo kukubali jukumu lisilo la kawaida kwa nchi yake.

Akiongea kwenye ITV, mshambuliaji wa zamani wa England Ian Wright alisema: "Hii ni timu ambayo inaweza kufika mbali na Ronaldo bado anaweza kuchangia.

"Iwapo ataelewa kinachoendelea , anaweza kuishia kuwafungia bao la ushindi kwenye fainali."