Tetesi za soka Jumamosi:Palace wamtaka Johnson kutoka Spurs

Muda wa kusoma: Dakika 2

Mlinzi wa Tottenham Brennan Johnson yuko kwenye orodha ya wachezaji wanaoweza kusajiliwa na Crystal Palace mwezi Januari, huku Eagles wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales, 24, kusaidia katika juhudi zao za kufuzu Ligi ya Mabingwa. (Telegraph)

Tottenham wako tayari kuvunja mfumo wao wa mishahara ili kumsajili winga wa Bournemouth na Ghana Antoine Semenyo, 25, mbele ya Manchester City na Liverpool. (Teamtalk)

Chelsea wanaibuka kama wagombea wakuu katika kinyang'anyiro cha kiungo wa kati wa AZ Alkmaar Kees Smit, 19, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi pia akiwa kwenye rada za Newcastle, Manchester United na Tottenham. (The I)

Kuvutiwa kwa Newcastle na beki wa Ufaransa wa Toulouse, Dayann Methalie, 19, kunaweza kuashiria mwisho wa muda wa beki wa Uswisi Fabian Schar mwenye umri wa miaka 33 katika klabu hiyo huku mkataba wake ukiisha msimu ujao wa joto. (Football Insider)

Mshambuliaji wa West Ham Niclas Fullkrug ni mojawapo ya majina ambayo AC Milan itazingatia katika dirisha la uhamisho la Januari huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 32, akitaka kuondoka Uwanja wa London. (Gazzetta dello Sport)

Crystal Palace inamtaka mlinzi wa kulia wa Bayern Munich Sacha Boey, 25, ambaye anatarajiwa kuondoka kwenye timu hiyo ya Bundesliga mwezi Januari. (Fabrizio Romano)

West Ham, Lazio na AC Milan zote zinamtaka mshambuliaji wa Italia na Sassuolo Andrea Pinamonti, 26 (Calciomercato)

Kiungo wa kati wa Everton James Garner anapendwa na Nottingham Forest ingawa uhamisho wa Januari kwa Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 24 hauwezekani ikizingatiwa kuwa amekuwa akianza mara kwa mara katika kikosi cha Toffees. (Mail)

Chelsea na Manchester United zinaharakisha juhudi za kumsajili kiungo wa Sunderland na DR Congo Noah Sadiki, 20, baada ya mwanzo wake mzuri katika soka la Uingereza. (Football Insider)