Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya: Bayern kutupa ndoano kwa Guehi Januari
Bayern Munich wanapanga kufanya mazungumzo na beki wa England, Marc Guehi, mwanzoni mwa Januari wakati ambao mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaweza kusaini mkataba wa awali na klabu yoyote ya nje, kutokana na mkataba wake na Crystal Palace kumalizika majira ya kiangazi. (Sky Sports Germany)
Tottenham wanatarajia kumuuza kiungo Yves Bissouma mwezi Januari, lakini kutokana na mkataba wake kumalizka majira ya kiangazi, wanaweza kutumia kipengele cha kumuongezea mwaka mmoja endapo watashindwa kumpata mnunuzi. (The Times)
Aston Villa wameiambia Liverpool kuwa wanataka kumrudisha kiungo wa England U-21 Harvey Elliot mwezi Januari. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa kwa mkopo Villa tangu majira ya kiangazi.(Teamtalk)
Arsenal wanaonyesha nia ya muda mrefu ya kuwasajili winga wa Real Madrid na Brazil Rodrygo (24) pamoja na winga wa AC Milan na Ureno Rafael Leao (26), ingawa kwa sasa hawajatilia mkazo kumsajili mshambuliaji mpya. (Caughtoffside)
Kamishna wa ligi kuu ya Marekani (MLS), Don Garber, amesema kuwa ligi hiyo iTAmpokea Mohamed Salah "kwa mikono miwili" endapo mchezaji huyo wa Misri mwenye miaka 33 ataamua kuondoka Liverpool. (Fox Sports)
Mshambuliaji wa Real Madrid Gonzalo Garcia, mwenye miaka 21, anawindwa na Stuttgart ya Ujerumani, ingawa wanaelewa kuwa dili hilo litakuwa gumu kutekeleza (Sky Sports Germany)
Manchester United hawana nia ya kumsajili beki wa zamani wa Hispania Sergio Ramos, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Monterrey ya Mexico (ESPN)
Bournemouth wanamfikiria winga wa FC Basel, Philip Otele, 26, kama chaguo mbadala la kuziba nafasi ya Antoine Semenyo. (Teamtalk)