Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, kuna njia yoyote ya Salah na Liverpool kuelewana?
Yatasalia kuwa moja ya mahojiano makali zaidi katika enzi ya Ligi Kuu.
Mchezaji wa Liverpool Mohamed Salah aliwashangaza watu wengi Jumamosi jioni alipodai kuwa uhusiano wake na meneja Arne Slot "ulivunjika".
Mmisri huyo, ambaye bila shaka ni mmoja wa wachezaji wakubwa wa Ligi ya Premia, alimuwekea shinikizo kocha Slot baada ya kutumikia mechi ya tatu mfululizo kwenye benchi la wachezaji wa akiba, huku Liverpool ikiruhusu leeds kutoka nyuma mara mbili katika sare ya 3-3 .
Madai kama vile 'ametupwa chini ya basi' na kwamba kuna 'mtu hakumtaka katika klabu' hiyo huenda ni jambo la mwisho ambalo Slot alitaka kusikia likiwekwa hadharani, hasa baada ya mchezo mbaya ambao umewaacha mabingwa hao wakiwa nafasi ya tisa kwenye Ligi Kuu.
Lakini sasa ipi hatima ya Salah Liverpool? Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alitia saini mkataba mpya wa miaka miwili tu mwezi Aprili lakini alikiri Jumamosi kuwa hakuwa na uhakika kama aliichezea klabu hiyo mechi yake ya mwisho.
BBC Sport inaangazia kwa undani kile kinachoendelea karibu na mchezaji huyo ambaye amefunga mabao 250 katika mechi 420 za Liverpool.
'Uhusiano wa Salah na Slot bila shaka umevunjika'
Salah mara chache huzungumza na vyombo vya habari lakini anapozungumza huwa ni kwa sababu ana jambo muhimu la kusema.
Hatua hiyo ilipata kiwango kipya kufuatia matamshi yake ya siku ya Jumamosi.
Alipokutana na vyombo vya habari katika barabara ya makutano ya Elland, alikuwa wazi kwa wanahabari kwamba alitaka kuzungumza nao.
Haijulikani ikiwa hii ilikuwa kwa sababu ya mafadhaika alioyopitia ama ilikuwa kitu alichokipanga.
Maoni yake yalienea ulimwenguni kwa haraka na kumweka kocha mkuu wa Liverpool Slot chini ya shinikizo.
Siku ya Jumapili, baadaye, kulikuwa na dalili ndogo kwamba kulikuwa na majuto yoyote au kurudi nyuma kutokana na kile ambacho Salah alikisema.
Vyanzo vinavyofahamu hali hiyo viliiambia BBC Sport kwamba uhusiano wa Salah na Slot umevunjika rasmi.
Alisema haoni mustakabali wa Liverpool na Slot kama meneja wake.
Hayo ni mabadiliko makubwa kutokana na hali ilivyokuwa miezi minane iliopita baada ya timu hiyo kushinda taji la ligi kuu muda mfupi tu baada ya kandarasi mpya na nono kutangazwa.
Vyanzo vya habari vinasema kwamba Salah pia amekerwa na hisia kwamba wachambuzi na wachezaji wa zamani wanatoa simulizi kwamba yeye ni moja ya sababu kuu za Liverpool kuhangaika msimu huu.
Salah anasemekana kuhisi kwamba Slot ameathiriwa na maoni hayo ya vyombo vya habari - lakini bila yeye uwanjani Reds bila shaka haijakuwa na kiwango kizuri cha mchezo.
Imedaiwa kwamba Salah anahisi mbinu tofauti msimu huu inayoendeshwa kulingana na mahitaji ya wachezaji wapya haimfai.
Vyanzo hivyo vilivyokerwa pia vilisema ni kiasi gani Salah anaipenda Liverpool na jinsi kiwango cha chini cha timu hiyo na jinsi alivyofadhaiswa na kiwacho.
BBC Sport iliambiwa Jumamosi kwamba Liverpool wana nia ya wazi kuhusu mustakabali wa Salah huku klabu ya Saudia ikimhitaji. Al-Hilal, inayosimamiwa na Simone Inzaghi, inafahamika kuwa miongoni mwa timu zinazomuhitaji.
Inaaminika kuwa bado hakujakuwa na mazungumzo madhubuti. Kwa sasa, inaonekana Salah anaweka wazi chaguzi zake, na ni wakati wa shughuli nyingi kwake na jukumu la Kombe la Mataifa ya Afrika linalotarajiwa Jumatatu 15 Desemba.
Kipi kitarajiwe?
Mashabiki wa Liverpool - na ulimwengu wa kandanda kwa ujumla - watasubiri kujua kile kitakachofuata .
Na hawatakuwa na muda mrefu sana kwasababu Jumatatu inaweza kuwa siku muhimu.
The Reds wanatarajiwa kushiriki mazoezi ya wazi Jumatatu asubuhi, kabla ya mechi muhimu ya Jumanne ya Ligi ya Mabingwa huko Inter Milan, kwa hivyo macho yote yatatazama ikiwa Salah atahudhuria.
Bado hatujasikia kutoka kwa Liverpool, lakini swali kubwa litakuwa je, Salah atasafiri na kikosi kwenda Milan baada ya mazoezi ya wazi?
Slot anatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza tangu mahojiano ya Salah yalipoanza Jumatatu usiku, na yote yakilenga kuwa kwenye uhusiano wao.
Je alishangazwa na mahojiano hayo? Je, kuna njia ya kurudi nyuma kwa Salah? Je, bado yuko kwenye mipango yake ya Jumanne usiku? Maswali yote kwa Slot itabidi yatoke huko Milan.
Siku moja baadaye, Liverpool watakuwa wakikabiliana na Inter Milan wakisaka ushindi ili kuwarudisha katika nafasi ya nane bora ya Ligi ya Mabingwa - lakini je, Salah atahusika?
The Reds kisha watamenyana na Brighton uwanjani Anfield Jumamosi, mechi ya mwisho ya Salah kabla ya kujiunga na Misri Jumatatu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika.
Ikiwa Salah atakuwa Anfield kwa sasa haijulikani na, kama yuko, mwitikio wa wafuasi dhidi ya hasira yake itakuwa ya kuvutia sana.
Chochote kitakachotokea, siku saba zijazo zitakuwa nzuri haswa kuhusu mustakabali wake wa Liverpool
'Ni makosa kutoka kwa Salah' - Maoni
Kipa wa zamani wa England Rob Green, aliiambia BBC Radio 5 Live:
Yeye huzungumza tu wakati yanapokwenda vibaya upande wake au iwapo mambo hayaendi kulingana na mahitaji yake .Amefanya hivyo mara chache baada ya michezo na nadhani anapaswa kuambiwa.
Lakini anachofanya ni kumpa Arne Slot bao la wazi sasa na chochote anachotaka kufanya. Kwa Sasa, Afcon inakuja na matamshi yake ni aina ya zawadi kwa Slot kusema hakuna mtu mkubwa kuliko klabu, ondoka.
Au anaweza kumrudisha kikosini, amuuguze tena kwenye timu lakini afanye hivyo kwa kauli yake.
Presha imeisha kabisa kwa Arne Slot sasa, kweli ni makosa kutoka kwa Mo Salah kwa sababu kiuhalisia sare (ya Leeds) na ugumu walionao msimu huu, angekaa kimya tu kwa sababu presha inazidi, kila mechi ambayo huchezeshwi.
Huu ni wakati wa Slot kuamua sasa. Kwangu mimi, Salah ni mchezaji bora wa muda wote kwa Liverpool, kwa kila kitu alichokifanya. Sasa unasema utaondoka wakati fulani. Huenda ikawa sasa, Januari anaweza kuja na kusema ni bora kwa pande zote mbili kuachana - haitanishangaza kama hilo lingetokea.
Kipa wa zamani wa Newcastle na Man City, Shay Given, aliambia BBC Mechi Bora ya Siku:
Nilimuhisi Mo Salah kidogo. Wakati mtu anaweka kipaza sauti mbele yako, ni wakati wa kukatisha tamaa kwa mchezaji wa akiba kutocheza, haswa mchezaji wa kiwango chake.
Jambo la kushangaza ambalo lilinitoka kwenye ukurasa wangu ni kwa nini Arne Slot hajampeleka ofisini mwake na kufanya mazungumzo naye ? Huyu jamaa ni mchezaji wa ajabu.
Najua pengine Mo amekasirika na kwenye baridi kali hakupaswa kusema baadhi ya mambo hayo, lakini sisi tumekuwepo, huchezi, una hasira na kuchanganyikiwa na timu haichezi vyema. Mo Salah amesema mwenyewe anajihisi kama mbuzi wa Azazeli.
Kiungo wa zamani wa Ujerumani na Aston Villa Thomas Hitzlsperger, kwenye Mechi Bora ya Siku ya BBC:
Nadhani alichosema alikuwa amekipanga lakini zaidi kilijaa hisia zake.
Wanachotakiwa kufanya ni kukaa chini na kusemezana maana bado haijaisha.
Wote wanahitaji kukusanyika na kusema tunaweza kupata hili sawa. Uharibifu umefanyika lakini bado nadhani kuna wakati wa kurekebisha lakini wanapaswa kufanya hivyo haraka.