Mafanikio ya Trump Gaza na kushindwa kwa Biden

Trump yuko upande wa kushoto na mgongo wake kwenye kamera, akitazama kulia kuelekea Netanyahu ambaye pia ameweka mgongo wake kwenye lenzi, akitazama kushoto kuelekea Trump. Wanaume wote wana suti nyeusi na mashati nyeupe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bega kwa bega - Trump na Netanyahu
    • Author, Anthony Zurcher
    • Nafasi, Mwandishi America Kaskazini
    • Author, Tom Bateman
    • Nafasi, Mwandishi wa Masuala ya Kigeni
  • Muda wa kusoma: Dakika 8

Wakati huo, shambulio la anga la Israel dhidi ya timu ya mazungumzo ya Hamas nchini Qatar lilionekana kama sababu nyingine ambayo ingesukuma matarajio ya amani kwenda mbali zaidi.

Shambulio la Septemba 9 lilikiuka uhuru wa mshirika wa Marekani na kuhatarisha kuzidisha mzozo huo kuwa vita vya eneo zima.

Diplomasia ilionekana kama imeporomoka kabisa.

Badala yake iligeuka kuwa wakati muhimu ambao umesababisha mpango, uliotangazwa na Rais Donald Trump, kuwaachilia mateka wote waliosalia.

Hili ni lengo ambalo yeye, na Rais Joe Biden kabla yake, walikuwa wametafuta kwa karibu miaka miwili.

Ingawa hii ni hatua ya kwanza tu kuelekea amani ya kudumu, bado kuna mazungumzo kuhusu kuondoa silaha kwaHamas, uongozi wa Gaza, na kuondoka kabisa kwa Israel katika eneo hilo.

Lakini ikiwa makubaliano haya yatadumu, yanaweza kuwa mafanikio makubwa ya Trump katika muhula wake wa pili ambayo Biden na timu yake ya kidiplomasia hawakuweza kufanikisha.

Mtindo wa kipekee wa Trump na uhusiano muhimu na Israeli na ulimwengu wa Kiarabu unaonekana kuchangia mafanikio haya.

Lakini, kama ilivyo kwa mafanikio mengi ya kidiplomasia, pia kulikuwa na sababu zilizokuwa zikichangia nje ya udhibiti wa viongozi hawa wawili.

Uhusiano wa karibu ambao Biden hakuwahi kuwa nao

Hadharani, Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wote wanatabasamu mara kwa mara.

Trump anapenda kusema kuwa Israel haina rafiki bora, na Netanyahu amemtaja Trump kama "mshirika mkuu zaidi wa Israel kuwahi kuwepo katika Ikulu ya White House". Na maneno haya ya upendo yameambatana na vitendo.

Wakati wa muhula wake wa kwanza wa urais, Trump alihamisha ubalozi wa Marekani nchini Israel kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem na kuachana na msimamo wa Marekani uliodumu kwa muda mrefu kuwa makazi ya Waisraeli katika Ukingo wa Magharibi wa Palestina ni kinyume cha sheria, msimamo huo ukiwa ni kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Wakati Israel ilipoanza mashambulizi yake ya anga dhidi ya Iran mwezi Juni, Trump aliwaamuru washambuliaji wa Marekani kulenga vituo vya kurutubisha nyuklia vya taifa hilo kwa mabomu yake ya kawaida yenye nguvu zaidi.

Woman holding flower seems overcome with emotion, as crowds behind wave USA and Israel flags

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waisraeli wakipeperusha bendera na wamarekani baada ya habari za makubaliano hayo

Maandamano hayo ya hadhara yaliyoungwa mkono huenda yalimpa Trump nafasi ya kutoa shinikizo zaidi kwa Israel nyuma ya pazia.

Kwa mujibu wa ripoti, mpatanishi wa Trump, Steve Witkoff, alimshinda Netanyahu mwishoni mwa 2024 na kukubali kusitishwa kwa mapigano kwa muda ili kuachiliwa kwa baadhi ya mateka.

Wakati Israel ilipoanzisha mashambulizi dhidi ya majeshi ya Syria mwezi Julai, ikiwa ni pamoja na kulipua kanisa la kwa mabomu, Trump alimshinikiza Netanyahu kubadili mwelekeo.

Trump alionyesha kiwango cha mapenzi na shinikizo kwa waziri mkuu wa Israel jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa, anasema Aaron David Miller wa Shirika la kimataifa la Carnegie. "Hakuna mfano wa rais wa Marekani kumwambia waziri mkuu wa Israel kwamba itabidi utii au sivyo."

Historia ya kibiashara ilisaidia kupata uungwaji mkono Ghuba

Shambulio la kombora la Israel lilolenga mji wa Doha, ambalo liliua raia mmoja wa Qatar likishindwa kuua afisa yeyote wa Hamas, lilimfanya Trump kutoa onyo kali kwa Netanyahu,kuwa Vita vilipaswa kusitishwa.

Trump aliipa Israel uhuru mkubwa katika operesheni yake katika eneo la Gaza.

Aliunga mkono kampeni ya Israel dhidi ya Iran kwa kutumia nguvu za kijeshi za Marekani.

Lakini shambulio dhidi ya Qatar lilikuwa jambo tofauti kabisa, lililomsogeza karibu na msimamo wa Waarabu kuhusu mbinu bora kabisa ya kumaliza vita.

Maafisa kadhaa katika utawala wa Trump wameiambia CBS, mshirika wa BBC nchini Marekani, kuwa hili lililikuwa jambo muhimu lililomsukuma rais kutumia shinikizo la hali ya juu kufanikisha makubaliano ya amani.

Syrian President Ahmed al-Sharaa walks on red carpet after disembarking a plane in Doha ahead of an emergency Arab-Islamic leaders' summit

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mkutano wa dharura wa kilele wa mataifa ya kiarabu ulifanyika mjini Doha baada ya shambulio hilo
Unaweza pia kusoma
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Uhusiano wa karibu wa rais huyu wa Marekani na mataifa ya Ghuba umeandikwa vyema. Ana shughuli za kibiashara na Qatar na UAE. Alianza mihula yake yote miwili ya urais kwa ziara za kiserikali nchini Saudi Arabia. Mwaka huu, pia alizuru huko Doha na Abu Dhabi.

Mpango wake wa mkataba wa Abraham, ambao ulirekebisha uhusiano kati ya Israel na mataifa kadhaa ya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na UAE, ulikuwa mafanikio makubwa zaidi ya kidiplomasia katika muhula wake wa kwanza.

Muda aliotumia katika miji mikuu ya Ghuba ya kiarabu mapema mwaka huu ulisaidia kubadili mawazo yake, anasema Ed Husain wa Baraza la Mahusiano ya kimataifa.

Rais wa Marekani hakuitembelea Israel katikaziara hii ya Mashariki ya Kati lakini alitembelea UAE, Saudi Arabia na Qatar ambako alisikia wito wa mara kwa mara wa kusitisha vita.

Chini ya mwezi mmoja tangu shambulio hilo la Israeli huko Doha, Trump alikaa karibu na Netanyahu akiipigia simu Qatar kuomba msamaha.

Na baadaye siku hiyo, kiongozi huyo wa Israel alitia saini mpango wa amani wa Trump wenye hoja 20 za Gaza - ambao pia ulikuwa na uungwaji mkono wa mataifa muhimu ya Kiislamu katika eneo hilo.

Ikiwa uhusiano wa Trump na Netanyahu ulimpa nafasi ya kuihimiza Israel kufikia makubaliano, basi historia yake na viongozi wa Kiislamu huenda ilimsaidia kufanikisha uungwaji mkono huo, na kuwasaidia kuwashawishi Hamas kukubali mpango huo.

"Mojawapo ya mambo ambayo yalitokea wazi ni kwamba Rais Trump alipata ushawishi kwa Waisraeli, na kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa Hamas," anasema Jon Alterman kutoka Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa (CSIS).

"Hilo lilileta utofauti. Uwezo wake wa kufanya hivi kwa wakati wake, na kutotii matakwa ya wapiganaji limekuwa tatizo ambalo marais wengi waliopita wamepambana nalo, na anaonekana kufanya kwa mafanikio kiasi."

Ukweli kwamba Trump ni maarufu zaidi nchini Israeli kuliko Netanyahu mwenyewe ilikuwa na manufaa ambayo alitumia kunufaisha upande wake, anaongeza.

Sasa Israel imejitolea kuwaachilia zaidi ya Wapalestina 1,000 wanaoshikiliwa katika magereza ya Israel na imekubali kujiondoa kwa sehemu kutoka Gaza.

Hamas itawaachilia mateka wote waliosalia, walio hai na waliokufa, waliochukuliwa wakati wa shambulio la awali la Oktoba 7 la Hamas, ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya Waisraeli 1,200.

Kumalizika kwa vita hivyo ambavyo vimesababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Gaza na vifo vya Wapalestina zaidi ya 67,000 sasa ni jambo linalofikirika.

Ushawishi wa Ulaya

Lawama za kimataifa dhidi ya Israel juu ya hatua zake huko Gaza pia zililemea fikra za Trump.

Masharti ya ardhini hayajawahi kutokea katika suala la uharibifu na maafa ya kibinadamu kwa Wapalestina.

Katika miezi ya hivi karibuni serikali ya Netanyahu iliendelea kushuhudia kutengwa kimataifa.

Wakati Israel ikichukua udhibiti wa kijeshi wa usambazaji wa chakula kwa Wapalestina na kisha kutangaza shambulio lililopangwa kwenye mji wa Gaza, nchi kadhaa kubwa za Ulaya, zikiongozwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ziliamua kuwa haziwezi kuunga mkono msimamo wa Washington unaokosa usawa linapokuja suala la Israeli.

Women and children peer out of the window of a stone building. There are rugs draped over the window and hanging from the ceiling.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wapalestina wakichungulia dirishani huko Gaza baada ya tangazo la kusitisha mapigano

Mgawanyiko wa kihistoria ulifuata kati ya Wamarekani na washirika wa Ulaya lilipokuja suala la vipengele muhimu vya diplomasia na mustakabali wa mzozo wa Israel na Palestina.

Utawala wa Trump uliikashifu Ufaransa iliposema itatambua taifa la Palestina, hatua iliyofuatiwa na Uingereza.

Walikuwa wakijaribu kuiweka hai dhana ya suluhisho la mataifa mawili, lakini zaidi ya hapo walilenga kuyatenga makundi ya msimamo mkali pande zote mbili na kufufua njia ya kidiplomasia kuelekea mustakabali wa pamoja kati ya Waisraeli na Wapalestina.

Lakini Macron alikuwa makini katika kuwaingiza Wasaudia kwa ajili ya mpango wake wa amani.

Hatimaye,rais huyo wa Marekani Donald Trump alikabiliana na muungano wa umoja wa Ulaya na mataifa ya Kiarabu kwa upande mmoja, dhidi ya wazalendo wa Israel na mrengo wa kulia kuhusu maono ya muda mrefu kwa watu wa eneo la Gaza.

Alifanya uamuzi wa kuwapendelea marafiki zake wa Ghuba.

Unaweza pia kusoma

Mgawanyiko wa kihistoria ulifuata kati ya Wamarekani na washirika wa Ulaya lilipokuja suala la vipengele muhimu vya diplomasia na mustakabali wa mzozo wa Israel na Palestina.

Utawala wa Trump uliikashifu Ufaransa iliposema itatambua taifa la Palestina, hatua iliyofuatiwa na Uingereza.

Walikuwa wakijaribu kuiweka hai dhana ya suluhisho la mataifa mawili, lakini zaidi ya hapo walilenga kuyatenga makundi ya msimamo mkali pande zote mbili na kufufua njia ya kidiplomasia kuelekea mustakabali wa pamoja kati ya Waisraeli na Wapalestina.

Lakini Macron alikuwa makini katika kuwaingiza Wasaudia kwa ajili ya mpango wake wa amani.

Hatimaye,rais huyo wa Marekani Donald Trump alikabiliana na muungano wa umoja wa Ulaya na mataifa ya Kiarabu kwa upande mmoja, dhidi ya wazalendo wa Israel na mrengo wa kulia kuhusu maono ya muda mrefu kwa watu wa eneo la Gaza.

Alifanya uamuzi wa kuwapendelea marafiki zake wa Ghuba.

Mbinu ya kipekee ya Trump

Mtindo wa kipekee wa Trump bado una shangaza. Mbwembwe au maneno makali, lakini baadaye hubadilika na kuwa wa kawaida zaidi.

Katika muhula wake wa kwanza, kauli zake kali na vitisho vya "moto na ghadhabu" vilionekana kuisababishia Marekani ijaribu kuingia vitani na Korea Kaskazini.

Badala yake, alijihusisha moja kwa moja kwenye mazungumzo ya amani.

Trump alianza muhula wake wa pili kwa pendekezo lililoshngaza kwamba Wapalestina walazimishwe kuhama Gaza ili eneo hilo libadilishwe kuwa sehemu ya kimataifa ya kitalii.

Viongozi wa Kiislamu walikasirika sana. Mabalozi wa zamani waliobobea katika masuala ya Mashariki ya Kati walishangazwa kwa hatua hiyo.

Hata hivyo, mpango wa amani wa Trump wa vipengele 20 hauko mbali sana na aina ya makubaliano ambayo Biden angeweza kufanya, na ambayo washirika wa Marekani wamekuwa wakiyaunga mkono kwa muda mrefu.

Trump ametumia mbinu isiyo ya kawaida kuyapata matokeo ya kawaida.

Imekuwa vurugu. Si sawa na vile diplomasia inavyofundishwa katika vyuo vikuu vya Ivy League.

Hata hivyo, walau katika tukio hili na kwa wakati huu, imeonekana kuleta mafanio.

Kesho Kamati ya Nobel itatangaza mshindi wa Tuzo ya Amani ya mwaka huu.

Ingawa hakuna uwezekano mkubwa kuwa Trump atashinda tuzo hiyo, wazo hilo halionekani kuwa la kushangaza kama lilivyokuwa wiki chache zilizopita.

Ripoti ya ziada na Kayla Epstein.

Unaweza pia kusoma

Imetafsiriwa na Martha Saranga