Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, Arsenal imeweka rehani ubingwa wa ligi kuu?
Baada ya Arsenal kupoteza uongozi wa mabao mawili na hatimae kukubali sare ya mabao mawili dhidi ya klabu iliyopo mkiani katika ligi kuu ya England (EPL), Wolves, swali la kuhusu iwapo Arsenal wana ari ya kumaliza ukame wa miaka 22 wa kushinda kombe la ligi kuu linabaki tena midomoni mwa watu.
Kwa mara ya kwanza msimu huu kwa kweli, kinyanganyiro cha kuwania ubingwa hakipo tena mikononi mwa Mikel Arteta na kikosi chake.
Iwapo Manchester City, walio nyuma kwa alama tano katika nafasi ya pili watashinda mechi zao 12 zilizosalia, ikiwemo mchezo wao wa nyumbani Etihad dhidi ya Arsenal, basi watamaliza kileleni katika ligi.
Hata hivyo, mtazamo huo huo unaweza kuzungumziwa kwa Arsenal pia, waliobakisha mechi 11, iwapo wakishinda mechi zao zote 11 ikiwemo ya Aprili dhidi ya City watabeba kombe.
Ila, baada ya kupoteza alama nne muhimu katika sare mbili mfululizo dhidi ya Brentford na Wolves, wako hatarini kuandamwa na jinamizi la masaibu yao ya zaidi ya miaka 20.
Washika bunduki hao wa London (The Gunners), wamemaliza mara tatu katika nafasi ya pili, mara mbili nyuma ya timu ya Pep Guardiola, huu ni ukumbusho unaojirudia mara kwa mara.
Aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal, Alan Smith, alikiri kuwa "neno 'chupa' litatumika sana katika siku chache zijazo." Kwa maana ya kushindwa 'kizembe'.
Mambo yalianza kunoga kabisa wakati Piero Hincapie alipofunga bao lake la kwanza kwa klabu hiyo katika dakika ya 56, likiwa la pili kwa arsenal waliotangulia mapema kwa bao la dakika ya tano lililofungwa na Bukayo Saka.
Lakini Gunners walikosa udhibiti na makali ya kumaliza mchezo dhidi ya Wolves, timu ambayo walikuwa wamepoteza mechi zao tisa zilizopita wakikodolea kushuka Daraja .
Wenyeji walionyesha ukakamavu wa kupambana na kurejea mchezoni, huku shuti kali kutoka umbali wa yadi 20 la Hugo Bueno likiwapa matumaini. Kisha, katika dakika ya nne ya muda wa nyongeza, Tom Edozie mwenye umri wa miaka 19 aliyeingia kutoka benchi kwa mechi yake ya kwanza katika kikosi cha wakubwa alitumia makosa ya maelewano kati ya wachezaji wa Arsenal, David Raya na Gabriel, na shuti lake likaingia wavuni baada ya kumgonga Riccardo Calafiori, na kuleta bao la kusawazisha la kusisimua na la ndoto.
Mechi mbili zijazo, Arsenal watakabiliana na mahasimu wao Tottenham Hotspur katika debi la London kabla ya kuvurugana na Chelsea, na kuyumba huku kwao kumewadia wakati muhimu sana katika msimu.
'Kwa hakika leo tulistahili kichapo'
Arteta anajua kuwa kikosi chake kitakabiliwa na lawama na kusundugwa.
'chochote tukachoambiwa ,tutakikubali'alisema. 'Tutaipokea risasi yoyote ,kwa sababu tulicheza chini ya viwango kabisa'
'Kila kitakachosemwa ,itakuwa sahihi kwa sababu hatukuwajibika.Jibu ni kucheza vizuri siku ya jumapili'
'nimesikitishwa sana na matokeo bila shaka na jinsi mechi ilivyoisha ,tutajilaumu wenyewe'
'katika kipindi cha pili,hatukuonyesha makali yetu kabisa yanayohitajika katika ligi hii.nimevunjika moyo kwa kweli,tutazungumza kuhusu tunavyohisi ila si kwa sasa'
'Ukifikia viwango hivi na ukiwa unaongoza ligi ,unakubali kashfa hizi,leo tunastahili kashfa'
Kocha wa Wolves Rob Edwards alisema'katika dakika ya kwanza tu,tulijua wana shinikizo kubwa, tukatumia fursa hiyo.
Gunners hawajakuwa katika kiwango chao bora tangu mwanzo wa mwaka 2026 na wameshinda mechi mbili tu kati ya saba za ligi, ushindi huo ukiwa dhidi ya Leeds na Sunderland.
Arteta aliongeza'kuna vitu vya msingi tulipaswa kuvifanya,tulivifanya vibaya,na kuvirudia
'si bora kuhukumu,sote tuna hisi nyingi sana .Ila lazima ukubali lawama kwa kuwa tunastahili.Ni rahisi sana kuzungumza kwa hisia ,na kutoa kauli za kuwaumiza wachezaji.Kila mmoja anajituma hapa'
Ni Crystal Palace na West Ham pekee (zote zikiwa na pointi nane) ambazo zimepoteza pointi nyingi zaidi kutoka katika nafasi za kuongoza kwenye ligi mwaka 2026 kuliko Arsenal (saba), na Gunners sasa wameshindwa kushinda wakiwa mbele katika mechi tatu kati ya tano zao zilizopita za ligi.
Hii pia ilikuwa mara ya kwanza katika historia ya ligi kuu ya Premier kushuhudia timu iliyokuwa mkiani mwa ligi ikizuia kipigo kutoka kwa kiongozi wa ligi licha ya kuanza kuchapwa mabao mawili chini.
'Ni wakati muhimu sana,tena sana na labda kuwe na mabadiliko'Smith alizungumza na Skysports
'Kwa sasa kombe liko mikonononi mwa Manchester City.Na kwa tajriba yao na uzoefu wa Pep Guardiola, City watachangamka sana.Watakuwa wamehisi mchecheto wa Arsenal na wanatazama kwa makini'
'Ukiwa unaongoza kwa magoli mawili dhidi ya timu iliyo mkiani wakiwa alama tisa tu,si jambo zuri kwa timu inayolenga kushinda ligi. Haitaakuwa rahisi kwa Arsenal kukabiliana na presha'
Presha inazidi kuongezeka kwa Arsenal baada ya kutupa uongozi wa amabao mawili dhidi ya Wolves.
'Hatukuwa na kiwango bora'
Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Arsenal imeshindwa kupata ushindi ugenini kwa mara ya kwanza tangu Aprili mwaka 2023 wakiwa ug awa West ham,ukiwa msururu wa mechi 18.
Saka,aliyemaliza ukame wa mabao wa mechi 15 anasema kulikuwa na tofauti kubwa na jinsi walivyocheza.
"Tumekatishwa tamaa, hatusemi mengi ," aliongeza mchezaji huyo wa England. "Tumepoteza viwango vyetu kwa kiasi kikubwa na tumeadhibiwa kwa hilo."
Siku moja tu baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitano, alianzishwa kama mshambuliaji kinara katika nafasi ya Namba 10, lakini alisalia kutazama tu kwa huzuni baada ya kutolewa katika dakika ya 73 akipewa matibabu.
"Tulikuwa butu," Saka aliongeza. "Ni wakati wetu kuchambua utendaji wa mechi chache zilizopita na kutatua matatizo mara moja, ili tuweze kurudi kushinda michezo, kuanza mfululizo na kujenga kasi tena kwa sababu tumeipoteza kidogo sasa hivi."
"Nadhani ni lazima turudi kwenye kiwango chetu. Tufanye mambo ya msingi vizuri kwani tuna ubora wa kutosha katika kikosi kushinda mechi, hasa kwenye michezo ambayo tumekuwa tukipoteza pointi hivi karibuni. Tunahitaji kutatua hilo na hilo ndilo linalojishughulisha sasa hivi."
'Tunastahili kupitia maumivu na kujitafakari '
Kwa kuwa derby ya Kaskazini mwa London inafuata dhidi ya Tottenham Jumapili, Arsenal lazima wajibu haraka.
Spurs watakuwa na Igor Tudor kando ya benchi kuu na wanatarajia aweze kuwapa 'msukumo wa meneja mpya' kuongeza kwa huzuni ya Gunners.
Arteta alikiri: "Tunahitaji kupitia maumivu, kujitifakari na kuelewa kinachohitajika kwenye mchezo Jumapili.
"Kile tunachosema kutoka hapa ni sawa, lakini tunahitaji kuweka yote ndani ya mioyo yetu na kuonyesha makali yetu Jumapili."