Tetesi za soka Ulaya: Mourinho hamuhitaji Cristiano Ronaldo Fenerbahce

Muda wa kusoma: Dakika 2

Jose Mourinho amefutilia mbali uwezekano wa nyota wa Ureno wa Al-Nassr Cristiano Ronaldo, 39, kujiunga naye Fenerbahce, akisema timu yake tayari ina washambuliaji watatu wazuri. (Goal)

William Saliba yuko tayari kuweka mustakabali wake wa muda mrefu kwa Arsenal licha ya beki huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 kuwa mlengwa namba moja wa Real Madrid. (Sun)

West Ham itamfikiria kocha wa Middlesbrough Michael Carrick iwapo watamtimua meneja wa sasa Julen Lopetegui. (Daily Mirror), nje

Arsenal wanatazamiwa kukataa ofa za Januari kwa beki wa kati wa Poland Jakub Kiwior huku Napoli, AC Milan na Juventus zikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Daily Mirror)

Meneja wa Crystal Palace Oliver Glasner amefutilia mbali uwezekano wa kumrudisha fowadi Mfaransa Odsonne Edouard, 26, kutoka Leicester anakocheza kwa mkopo. (Talksport)

Mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 25, ambaye yuko kwa mkopo Galatasaray, ana nia ya kuungana na mkurugenzi wa zamani wa michezo wa klabu hiyo Cristiano Giuntoli, Juventus. (Il Mattino)

Mlinzi wa Manchester United na Argentina Lisandro Martinez, 26, yuko kwenye rada za Real Madrid huku mabingwa hao wa Ulaya wakitathmini uwezekano wa mabeki wapya wa kati. (TBR Football)

West Ham wanafikiria kumnunua mlinzi wa Chelsea Tosin Adarabioyo kwa mkopo Januari 27. (Footmercato)

Chelsea na Arsenal ziko mbioni kumsajili beki wa Brazil mwenye umri wa miaka 19 Vitor Reis kutoka Palmeiras. (Florian Plettenberg)

Paris St-Germain wanafikiria kumnasa mshambuliaji wa Sporting raia wa Sweden Viktor Gyokeres, huku Arsenal, Chelsea na Manchester United pia wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Fichajes)