Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumanne 21.11.23
Chelsea wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney, 27, kwa pesa nyingi katika kipindi cha dirisha la usajili la Januari. (Football.London)
Chelsea, Manchester City, Manchester United na Newcastle United zote zilituma wawakilishi kumtazama winga wa Napoli Khvicha Kvaratskhelia, 22, wakati wa kushindwa kwao 3-1 na Uhispania Jumapili. (90min)
Arsenal na Manchester United ni miongoni mwa vilabu vinavyotarajiwa kuonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Brazil Marcos Leonardo, 20, ambaye wakala wake anasema atataka kuondoka Santos Januari. (Evening Standard)
Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, anasema "kutakuwa na wakati wa kuzungumza" kuhusu mustakabali wake wa Paris St-Germain anapojiandaa kuingia miezi ya mwisho ya mkataba wake na klabu hiyo ya Ligue 1. (Telefoot, via Mail)
Benfica hawana mpango wa kuingia kwenye mazungumzo juu ya kiungo wa kati wa Ureno Joao Neves, 19, ambaye amekuwa akifuatiliwa na Manchester United, akiwa na kipengele cha kumnunua cha £105m. (Fabrizio Romano)
Bayern Munich wanaweza kufikiria kumnunua beki wa kati wa Manchester United na Ufaransa Raphael Varane, 30. (Sky Germany - in German)
Liverpool haitakubali ofa kwa winga wa Colombia Luis Diaz, 26, licha ya ripoti nchini Uhispania kwamba wanaweza kuidhinisha makubaliano ya kubadilishana na Barcelona kumnunua mshambuliaji wa Brazil Raphinha, 26. (Football Insider)
Meneja wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso hana kipengele cha kuuzwa katika mkataba wake kinachomruhusu kujiunga na moja ya timu zake za zamani, Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo amesema, huku kukiwa na ripoti kwamba Mhispania huyo, 41, anaweza kuhamia Liverpool, Real Madrid au Bayern Munich. (Talksport)
Tottenham wako tayari kuwapa Roma £26m kwa ajili ya kiungo wa kati wa Italia Bryan Cristante, 28. (Tuttomercatoweb, via Teamtalk)
Tottenham hawajafurahishwa na madai ya Everton kwamba kukataa kwao kulipa pauni milioni 80 kumnunua mshambuliaji wa Brazil Richarlison, 26, kulisababisha The Toffees kukiuka kanuni za matumizi ya fedha za Premier League. (Mail)
Manchester United wanapanga kuchukua nafasi ya mkurugenzi wa soka John Murtough kama sehemu ya mabadiliko makubwa yatakayoambatana na uwekezaji wa Sir Jim Ratcliffe katika klabu hiyo. (MEN)
West Ham inasemekana kuwa na hasira huku kukiwa na hofu kwamba Michail Antonio amepata jeraha la muda mrefu akiwa na timu ya taifa ya Jamaica. (Telegraph - subscription required)
Mkurugenzi wa Girona Quique Carcel anasema klabu hiyo ingetamani kumsajili tena kiungo wa kati wa Uhispania Oriol Romeu, 32, kutoka Barcelona. (90min)
Imetafsiriwa na Asha Juma na kuhaririwa na Seif Abdalla