Matokeo 10 ya kushangaza katika historia ya kombe la Dunia

Saudi Arabia iliwashangaza wengi katika kombe la Kombe la Dunia walipotoka nyuma na kuwaduwaza washindi mara mbili Argentina katika mechi ya kwanza ya Kundi C iliyofanyika Lusail.

Ikiwa ya 51 katika orodha ya dunia , Saudia ingeshindwa katika kipindi cha kwanza cha mchezo baada ya Lionel Messi kufungua mlango wa mabao kupitia mkwaju wa penalty kabla ya magoli mengine matatu kiudaiwa kuwa ya kuotea.

Lakini Saudia ilibadilisha mchezo katika kipindi cha pili ndani ya dakika 10 za kwanza ambapo saleh Al Shehri alisawazisha na baadaye salem Al Dawsari kufunga bao la ushindi , bao lililozua sherehe kubwa katika uwanja huo.

Matukio haya mnakuba ya kushangaza huifanya michunao ya kombe la Dunia kuwa maalum.

Lakini je matokeo hayo ya Saudia dhidi ya Argentina yanalinganishwa vipi na matokeo mengine makubwakatika historia ya michunao hiyo?

Watangazaji wa BBC Gary Lineker, Alan Shearer na Micah Richards walijadili mada hii kwenye kipindi chaMechi ya Siku.

Korea Kusini 2-1 Italy 2002 (Richards: 7, Shearer: 10)

Ndoto ya Korea Kusini iliowasaidia kufuzu nusu fainali ya Kombe la Dunia 2002 ilijumuisha ushindi wa 2-1 dhidi ya Italia katika hatua ya 16 bora.

Ahn Jung-hwan - ambaye, kwa bahati mbaya, alitumia misimu miwili iliyopita kwa mkopo katika timu ya Italia Perugia – alifunga bao la dhahabu katika muda wa nyongeza na kuwaondoa nyota wa Azzurri waliokuwa na Gianluigi Buffon, Paolo Maldini na Alessandro del Piero.

Lineker: Ilikuwa ni mshtuko mkubwa na ulikuwa mchezo wa ajabu. Korea Kusini imeimarika na huo ukawa mwanzo wake. Licha ya timu kuwa na nguvu kiasi gani, kuna sababu isiyojulikana kila wakati.

Thamani ya goli ni kubwa sana na umati unaweza kuliunga mkono na kuipa timu kitu cha kung'ang'ania.

Richards: Huo ulikuwa mshtuko mkubwa wakati huo ingawa Korea Kusini ilikuwa timu nzuri.

Uholanzi 5-1 Uhispania 2014 (Richards: 10, Shearer: 7)

Utetezi wa Kombe la Dunia wa Uhispania ulianza kwa njia mbaya walipochapwa 5-1 na Uholanzi katika mchezo wao wa ufunguzi wa makundi wa michuano ya 2014 nchini Brazil, na kuwaruhusu Waholanzi hao kulipiza kisasi kwa kushindwa kwao katika fainali ya 2010.

Pia ilikuwa tofauti kubwa zaidi ya mabao kwa bingwa mtetezi kuahi kupoteza katika Kombe la Dunia.

Shearer: Uhispania pia walipoteza mchezo wao uliofuata na wakatolewa nje baada ya kuingia kwenye dimba wakiwa washikiliaji.

Lineker: Uholanzi ndio kwanza waliicharaza Uhispania siku hiyo na unafikiria 'nini kiliwapata?'

Ujerumani Mashariki 1-0 Ujerumani Magharibi 1974 (Richards: 6, Shearer: 9)

Kikosi cha Ujerumani Magharibi kinachoongozwa na nahodha Franz Beckenbauer na chenye mshambuliaji mahiri Gerd Muller kilipewa nafasi kubwa dhidi ya Ujerumani Mashariki, haswa kwa vile walikuwa pia wenyeji wa Kombe la Dunia na mabingwa wa Ulaya.

Lakini bao la dakika za mwisho la Jurgen Sparwasser lilihitimisha ushindi mnono kwa Ujerumani Mashariki na kuhakikisha wanaongoza kundi mbele ya wapinzani wao.

Lineker: Ujerumani Magharibi ilikuwa na nguvu nyingi siku hizo. Ilikuwa ni jambo la kushangaza kwa sababu wenyeji waliishia kushinda Kombe la Dunia mwaka huo.

Senegal 1-0 Ufaransa 2002 (Richards: 4, Shearer: 8)

Mechi nyingine ya ufunguzi wa mashindano hayo ilikuwa ile ya kichapo cha kushangaza dhidi ya mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia.

Bao la Papa Bouba Diop lilitosha kwa washiriki wa kwanza wa Kombe la Dunia Senegal kuwashtua mabingwa watetezi Ufaransa katika mchezo wa kwanza wa Korea/Japan 2002.

Senegal wangetinga robo fainali, lakini matokeo mabaya ya Les Bleus yaliifanya kumaliza chini ya kundi lao wakiwa na pointi moja pekee katika mechi tatu.

Scotland 3-2 Uholanzi 1978 (Richards: 9, Shearer: 3)

Archie Gemmill alifunga moja ya mabao mazuri zaidi kuwahi kutokea katika Kombe la Dunia na kuisaidia Scotland kuishangaza Uholanzi kwenye Kombe la Dunia la 1978 nchini Argentina.

Huku Scotland ikiwa tayari inaongoza 2-1 na dakika 20 zilizosalia, Gemmill aliwachanganya walinzi watatu wa Uholanzi kabla ya kuinua mpira kwa utulivu juu ya kipa Jan Jongbloed na kuingia wavuni.

Shearer: Ninakumbuka bao hilo, aliwakata mabeki na kuingia upande wa kulia kabla ya kufunga. Scotland walikuwa na wachezaji wazuri katika kipindi hicho na timu hiyo ya Uholanzi ilifika fainali.

Uhispania 0-1 Uswizi 2010 (Richards: 8, Shearer: 4)

Uhispania ilifika kwenye Kombe la Dunia la 2010 kama mabingwa wa Ulaya na vipenzi vyake vya michuano hiyo, lakini mchuano wao ulianza vibaya zaidi Afrika Kusini walipoteleza na kuchapwa 1-0 na Uswizi bao lililofungwa na kiungo wa zamani wa Manchester City, Gelson Fernandes.

Marekani 1-0 Uingereza 1950 (Richards: 1, Shearer: 6)

England iliwasili Brazil kwa Kombe la Dunia la 1950 kama moja ya vivutio vya mashindano hayo na ilitarajiwa kupunga upepo na timu ya Marekani ilioshirikisha wachezajiwachanga na wasio na uzoefu wa kitaaluma.

Lakini Joe Gaetjens mzaliwa wa Haiti, mwanafunzi wa uhasibu ambaye pia aliosha vyombo katika mkahawa wa Brooklyn, alifunga bao la pekee na kuipatia ushindi ambao haukutarajiwa timu yake.

Lineker: Ilikuwa ni huzuni kubwa. England ilikuwa na wachezaji wazuri kama vile Billy Wright, Stan Mortensen na Tom Finney. Uingereza ilirudi nyumbani ikiwa na aibu kubwa.

Shearer: USA hawakuwa na uwezo wa kushiunda mechi hiyo lakini waliishinda England na wachezaji hao wote.

Argentina 0-1 Cameroon 1990 (Richards: 2, Shearer: 5)

Miaka minne baada ya Diego Maradona kuwapatia msukumo wa ushindi wao wa ajabu wa Kombe la Dunia nchini Mexico, Argentina walishtushwa na Cameroon katika mechi ya ufunguzi ya Italia '90 kwenye uwanja wa San Siro wa Milan.

Bao la kichwa la Francois Omam-Biyik kipindi cha pili lilitosha kuwpatia ushindi Cameroon ambao hawakutarajiwa kupata matokeo kama hayo ambapo Andre Kana-Biyik na Benjamin Massing walitolewa nje kwa kadi nyekundu.

Shearer: Huo ulikuwa muujiza wa Milan.

Lineker: Cameroon walikuwa timu ya soka ya kifahari. Walicheza soka maridadi na walikuwa na akili katika uchezaji wao.

Uhispania 0-1 Ireland ya Kaskazini 1982 (Richards: 5, Shearer: 1)

Wachache waliipa Ireland Kaskazini nafasi ya kujshinda walipochuana na wenyeji Uhispania katika mechi yao ya mwisho ya kundi, wakihitaji ushindi ili kufuzu kwa hatua inayofuata.

Lakini bao la Gerry Armstrong mwanzoni mwa kipindi cha pili liliwapatia ushindi mmoja mkubwa zaidi, jambo la kushangaza zaidi walicheza sehemu kubwa ya kipindi cha pili wakiwa na wachezaji 10 baada ya Mal Donaghy kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Shearer: Ilikuwa ni ajabu kuona Ireland Kaskazini ikishiinda Uhispania. Walicheza na wachezaji 10 kwa nusu saa.

Lineker: Kwa Gerry Armstrong ilikuwa ni wakati wa kubadilisha maisha. Baada ya hapo alihamia Uhispania na kuwa mchambuzi wa Uhispania. Akizungumzia kuhusu lengo moja la kubadilisha maisha yako.

Italia 0-1 Korea Kaskazini 1966 (Richards: 3, Shearer: 2)

Italia, ambao walikuwa miongoni mwa waliopendekezwa kwa Kombe la Dunia la 1966, walifika Ayresome Park huko Middlesbrough wakihitaji sare tu dhidi ya washiriki wa kwanza wa michuano hiyo Korea Kaskazini ili kufuzu robo fainali. Lakini bao kutoka kwa Pak Doo-ik liliifanya Korea Kaskazini kufuzu huku Azzurri ya Itali ikifunga virago na kwenda nyumbani mapema .