Kwanini vikosi vya Urusi vimeondoka Kherson, eneo ambalo waliliteka kutoka kwa Ukraine?

.

Chanzo cha picha, ANADOLU

Maelezo ya picha, Shambulizi la wanajeshi wa Ukraine Kherson

Siku ya Jumatano , mamlaka ya Urusi ilitangaza rasmi kusalimu amri mjini Kherson , ‘ikitangaza kuondoa vikosi vyake’.

Jeshi la Urusi linajiondoa polepole katika mji iliouteka, ambao Ukraine imekuwa ikijaribu kuukomboa tangu mwisho wa msimu wa joto.

Hiki ndio kituo kii cha kijimbo pekee ambacho Urusi ilikuwa imekiteka tangu kuanza kwa uvamizi nchini Ukraine .

BBC inazungumzia kuhusu kile kilichotokea , pengine kushindwa pakubwa kwa vikosi vya Urusi tangu uvamizi wake na kile kinachoendelea katika upande wa kulia wa ukingo wa mto Dnieper.

Tarehe 9 Novemba , habari za runinga ya taifa zilianza na ripoti ya komando wa kundi la wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine , Sergei Surovikin , kwa Waziri wa Ulinzi nchini humo Sergei Shoigu .

Jenerali mwenye kimo kirefu aliyekasirika akiwa amevalia magwanda ya kijeshi alisimama na kijiti alichokuwa akiotesha ramani .

Baada ya kuonesha jinsi jeshi la Urusi lilivyofanikiwa katika vita hivyo, Shoigu aliangazia mada kuu na kuuliza kuhusu Kherson.

Muelekeo wa Kherson ni kwamba tunajilinda , lakini ina ubaya wake, Waziri huyo alisena.

Kulingana na jibu la jenerali Surovikin, ilikuwa wazi ni wakati wa jeshi la Urusi kuondoka katika mji huo iliouteka mwanzoni mwa uvamizi huo.

Zaidi ya mwezi mmoja uliopita Kremlin iliandaa sherehe za kuweka makubaliano ya maeneo yaliotekwa na Urusi wakati wa vita hivyo ikiwemo jimbo la Kherson.

Baada ya sherehe hiyo rais Putin alisema kwamba wakaazi wa eneo la Kherson sasa watakuwa raia wa Urusi maisha .

 Wanajeshi wachache wa Urusi walisalia

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ukombozi wa Kherson ulikuwa lengo kuu la jeshi la Ukraine tangu mwanzo wa vita hivyo .

Haiwezekani kufikiria kwamba mji wa Kherson utasalia na maadui zetu. Hii ni muhimu, mshauri wa afisi ya rais wa Ukraine aliambia BBC katikati ya mwezi Agosti.

Mashambulizi kusini mwa taifa yalitangazwa mjini Kyiv katika msimu wote wa joto.

Mwezi Julai jeshi la Ukraine lilianza kutekeleza mashambulizi ya kila siku katika daraja muhimu la kimkakati linalounganisha kulia na kushoto mwa ukingo wa mto Dnieper katika jimbo la Kherson.

Ni kupitia daraja hilo ambapo vikosi vya Urusi vilikuwa vikipata silaha. Lakini kutokana na mashambulizi ikiwemo yale ya kutumia silaha ya HIMARS – madaraja ya Kakhovka na Antonovsky yalikuwa hayapitiki

Wanajeshi wa Urusi walilazimika kutumia feri , lakini uvukaji wa feri pia ulishambuliwa mara kwa mara hali iliosababisha matatizo makubwa ya kimkakati. Mwisho wa mwezi Agosti , mashambulizi upande wa kusini yalianza.

Mamlaka ya Urusi na maafisa waliokuwa wakikalia eneo hilo waliitaja operesheni hiyo kuwa bandia .Uongozi wa jeshi ulisema kwamba jaribio la kushambulia lilishindwa kufaulu na kwamba jeshi la Ukraine lilipata kipigo.

Lakini ukweli ni kwamba , hali ambayo jeshi la Urusi ilijipata haikuwa nzuri kabisa.

Huku wakikabiliwa na mashambulizi upande wa kusini , Jeshi la Ukraine lilielekea katika jimbo la Kharkiv, na kukomboa Balakleyah , Kupyansk na Izyum ambayo ilikuwa imekaliwa tangu msimu wa baridi , wataalamu walielezea BBC kwamba vitendo vya mjini Kherson vinaweza kutumika Pamoja na vitu vingine kuwa mpango wa kuelekea mashariki.

Meli ya mwisho

.

Chanzo cha picha, SERGEI BOBYLEV and TASS

Maelezo ya picha, Moja ya meli za magari zilizobeba wenyeji wa Kherson kutoka ukingo wa kulia wa mto Dnieper kwenda kushoto.

Mnamo tarehe 7 mwezi novemba , mfanyakazi mmoja wa nyumba ya wazee alimshawishi ajuza wa miaka 83 Alevtina Ivanoma , ambaye amekuwa akiishi katika nyumba hiyo kuondoka na kuelekea katika eneo la Krasnoder.

''Ni mwanamke mwenye nguvu, anapiga kelele, anashikilia kitanda anasema haendi kokote, lakini tunahitaji kufunga'' , alisema Svetlina mwenye umri wa miaka hamsini – aliyeomba jina lake kutotajwa na BBC kwasababu ya masuala ya usalama.

Anasema kwamba yeye mwenyewe yuko Krasnoder pamoja na wadi yake na wafanyakazi wote wa nyumba hiyo ya wazee. Lakini anaongezea kwamba sio wenzake wote walioondoka katika mji huo.

Meli ya mwisho ilisafiri kutoka ukingo wa kulia wa mto Dnieper kwenda kushoto saa 12 jioni mnamo Novemba 7.

Kabla ya hii, uhamishaji wa wale wanaotaka kuondoka katika jiji lililokaliwa ulipitia hatua tofauti: mwanzoni, mamlaka ilikataa uwezekano, kisha wakatangaza uondoaji wa hiari wa watu wote wanaokuja kwa madhumuni ya usalama, ifikapo Novemba 6, mamlaka ya uvamizi iliahidi kuifanya iwe ya lazima.

Licha ya hayo, hata uwezekano wa kusalimisha mji ulikataliwa. "Hakuna mtu atakayesalimisha jiji la Kirusi. Warusi hawajisalimishi!" - aliahidi mkuu wa Utawala wa kijeshi wa Kherson Alexander Kobets katika pongezi zake za Siku ya Umoja wa Kitaifa mnamo Novemba 4.

Uongozi uliokalia mkoa wa Kherson mwishoni mwa Oktoba uliliacha jiji hilo na kuelekea mashariki.

Viongozi walilalamika mara kwa mara sio tu juu ya mashambulizi ya kukera ya Vikosi vya Ukraine, hatua iliolifanya jeshi la Urusi kurudi nyuma bali juu ya hatua za raia katika maeneo yaliyokaliwa ya mikoa ya Zaporozhye na Kherson, ambao walifanya majaribio ya mauaji (pamoja na yaliyofanikiwa) dhidi ya maafisa kadhaa wa "tawala" zinazounga mkono Urusi .

"Mikakati hatari"

.

Chanzo cha picha, Vladmiri Bondarenko

Maelezo ya picha, Kirill Stremousov

Kabla ya uvamizi wa Urusi, Kirill Stremousov hakufurahia umaarufu maalum nje ya Ukraine, na hata katika Ukraine yenyewe.

Mzaliwa wa mkoa wa Donetsk, katika miaka ya 2000 alifanya kazi katika Kamati ya Uvuvi ya Kiev, kisha akahamia Kherson.

Akiwa huko Stremousov alifanya kazi pamoja na mashirika yanayoiunga mkono Urusi yanayohusiana na rais wa zamani wa Ukraine Viktor Yanukovych na mwandani mkuu wa rais Putin Viktor Medvedchuk.

Alijaribu bila mafanikio kuchaguliwa kama naibu na meya wa Kherson; alikuwa mmoja wa viongozi wa harakati ya Kiukreni dhidi ya chanjo ya Covid-19, na hapo awali aliongoza semina juu ya dawa mbadala

Mwanzoni mwa uvamizi wa Urusi, Stremousov alitangaza kuundwa kwa "kamati ya wokovu kwa amani na utulivu", ambayo ilitakiwa kuanzisha "uhusiano wa kibiashara, kiuchumi na kijamii na kitamaduni" na Urusi, na mwishoni mwa Aprili. tayari alijiunga na "utawala" wa mkoa wa Kherson katika nafasi ya naibu mtendaji mkuu.

Volodymyr Saldo, meya wa zamani wa Kherson na naibu wa watu wa Rada ya Verkhovna ya Ukraine kutoka Chama cha Mikoa cha Yanukovych, akawa bosi wake.

Tangu Agosti, Stremousov ameshikilia kuwa anapokea vitisho kila siku, na kumekuwa na majaribio ya mara kwa mara juu ya maisha yake. Mnamo Novemba 9, alikufa katika ajali karibu na Genichesk - angalau, toleo hili lilienezwa na mamlaka ya Kherson.

Baadhi ya raia wa Ukraine walichukua hili kwa mashaka - Yuriy Sobolevsky, naibu mkuu wa Baraza la Mkoa wa Kherson, alipendekeza kwamba kifo cha Kirill Stremousov kinaweza kuonyeshwa.

Chanzo cha habari cha RIA Novosti kinadai kuwa mhusika wa ajali hiyo ambayo Stremousov alifariki inadaiwa kuwa ni "dereva wa lori ambaye alifanya ujanja hatari," na dereva wa afisa huyo anadaiwa kushindwa kulimudu.

Picha na video kutoka eneo la ajali zinaonyesha kwamba gari la kivita la Stremousov lilipata uharibifu mkubwa

Maafisa wa Urusi waliitikia kifo cha Stremousov kwa kujizuia siku nzima. Ilipofikia Usiku alipewa tuzo ya Ujasiri na Vladimir Putin, ambaye kwa siku nzima hakusema neno juu ya kifo chake au kujisalimisha kwa kherson.

Je Urusi itachukua hatua gani?

.

Chanzo cha picha, RUSSIA DEFENCE MINISTRY

Jeshi la Urusi tangu mwanzo wa uvamizi lilijaribu kusonga mbele hadi Odessa na Nikolaev.

Katika tukio la upotezaji wa daraja la ukingo wa kulia wa mto Dnieper, haitawezekana kufanya hivi baada ya tukio hili jipya kwani wanajeshi watalazimika kuvuka mto tena ili kuyafikia maeneo hayo – hali ambayo kwa sasa haiwezekani.

Je, mazungumzo yanawezekana?

Agizo la Shoigu la kuondoka mjini Kherson pia linazua maswali zaidi ya kimataifa - kwa mfano, je, mafanikio ya Waukraine yanaweza kuleta amani karibu?

Saa chache kabla ya tangazo rasmi la kujiondoa kwa Kherson, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi Maria Zakharova alisema kuwa Urusi bado iko tayari kufanya mazungumzo na Ukraine - "kwa kuzingatia hali halisi inayojitokeza kwa sasa." Kauli yake, kwa kuzingatia tu "ukweli" huo, ilivutia umakini mwingi.