Sababu 5 kwa nini Putin hawezi kuamuru shambulizi la nyuklia

Chanzo cha picha, EPA
Najiskia kama ninaangalia filamu ya James Bond.
Mahali fulani karibu na Moscow, Rais wa Urusi yuko jukwaani na anaulizwa kuhusu matokeo ya uharibifu.
Mwanablogu anamkumbusha Putin kuwa alitabiri kuwa baada ya shambulio la nyuklia, Warusi watakwenda peponi.
"Hatuna haraka ya kwenda huko, au sio?" Anamuuliza mwanablogu mwenye matumaini.
Kisha kukawa na muda mrefu wa utulivu usio kawaida. Sekunde saba za ukimya.
"Ukimya wako unaniogopesha", anasema mwanablogu.
"Ilikuwa ndio dhamira yenyewe", Putin alijibu kwa dharau.
Pole kwa kutocheka. Hii si filamu ya Hollywood ambayo ina uhakika wa kuwa na mwisho mwema wa furaha. Matukio ya miezi minane iliyopita ndio mchezo wenyew wa kuigiza ambao umesababisha mateso yasiyoelezeka kwa Ukraine na wengi wanaamini kwamba dunia iko karibu kuingia kwenye mgogoro wa nyuklia kuliko wakati mwingine wowote ule tangu mgogoro wa makombora wa Cuba miaka 60 iliyopita.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Sasa maandishi ya mchezo huu wa kuigiza yanakwenda vipi?
Mengi yanategemea jibu la swali hili: Ni kwa kiasi gani Vladimir Putin yuko tayari kwenda kuhakikisha ushindi au kuepuka kushindwa Ukraine?
Kama wewe utasoma tena hii hotuba kwa taifa lake kuanzia Februari 24, moja yeye alitoa baada ya kuagiza uvamizi wa Ukraine, unaweza kuhitimisha kwamba atafanya chochote kile: "Na sasa baadhi ya maneno muhimu - muhimu sana - kwa wale ambao wanaweza kushawishika kuingilia kile kinachoendelea. Wale wanaojaribu kuingilia kati njia zetu au kutengeneza vitisho kwa nchi yetu na watu wetu wawe macho: Majibu ya Urusi yatakuwa ya haraka na yataleta aina ya matokeo ambayo hawajawahi kushuhudiwa katika historia".
Nje ya Urusi, "matokeo ambayo hujawahi kuyapata katika historia" yalitafsiriwa sana kama mgogoro wa nyuklia. Na katika miezi ifuatayo kelele hizo ziliendelea.
Mwezi Aprili, Rais Putin alitishia kuchukua "mwitikio wa haraka kama mtu angejaribu kuingilia na kutengeneza tishio la kimkakati dhidi ya Urusi. Tuna silaha zote tunazozihitaji kwa ajili ya hili ".
Mwezi Septemba aliongeza jeshi lake. Wiki iliyopita, katika ukumbi wa Valdai Debating, Rais Putin alikuwa akituma ishara mchanganyiko. Alikanusha nia yoyote ya kutumia silaha za nyuklia nchini Ukraine.
"Hatuoni haja. Hakuna haja ya kisiasa wala kijeshi ", alisema.

Chanzo cha picha, EPA
Lakini nyuma ya mjadala uliokuwa ukiendelea ilikuwa ni uvumi tu.
"Kuna hatari kwamba Urusi itatumia silaha za nyuklia. Si dhidi ya Ukraine, lakini dhidi ya Magharibi ", alisema Dmitry Suslov, mwanachama wa Sera ya Mambo ya Nje ya Urusi na Baraza la Ulinzi.
"Kama kombora moja la Marekani litapiga miundo mbinu ya kijeshi ya Urusi, tungefanya jaribio la kihistoria kuelekea Har–Magedoni ya nyuklia. Kwa mujibu wa mafundisho rasmi ya nyuklia ya Urusi, Urusi ingeanzisha shambulizi la kimkakati dhidi ya Marekani na washirika wote wa NATO haraka iwezekanavyo". Mara tu tutakapoona makombora ya Magharibi yakirushwa kwenye eneo letu, bila kujali yana silaha kiasi gani, Bilas haka yoyote, dunia nzima itakufa".
Je hii ni hofu tu? Kabisa.
Au ni maneno yenye ukweli ndani yake?
Sina uhakika sana.
Kuacha kando kule kusalia kimya kwa rais (hakika ilikuwa mchezo wa kuigiza) na maswali yasiyo na majibu ya hivi karibuni ya Urusi, nafkiri haiwezekani kwamba Kremlin ina mipango ya kutumia nguvu ya nyuklia ya vita ya Ukraine hivi sasa.
Hasa kwa kuzingatia sababu hizi nne.
Uchaguzi wa katikati ya muhula wa Marekani.
Huku uchaguzi wa katikati ya muhula ukielekea kufanyika nchini Marekani, chama cha Kremlin kitajua kwamba chama cha Republican kina nafasi ya kushinda udhibiti wa Congress.

Chanzo cha picha, Reuters
Mapema mwezi huu, kiongozi wa wachache wa bunge Kevin McCarthy alionya kuwa wabunge wa chama cha Republican hawatakubali "chochote" tu kwa ajili ya Ukraine kama watarejea kupata wingi wa wabunge.
Huo ni muziki kwa masikio ya Putin.
Ingawa si wazi kama msaada wa Marekani kwa Ukraine utaathirika kwa kiasi kikubwa na ushindi wa Republican, Kremlin itakaribisha nafasi yoyote ya kupunguza msaada wa jeshi la Marekani kwa Kyiv.
2. Majira ya baridi Ulaya
Inaonekana Vladimir Putin anaendelea kufanya hesabu zake, huku Urusi ikikata usambazaji wake wa gesi kwenda Ulaya, na msimu wa baridi hali itakuwa mbaya zaidi katika bara la Ulaya na matatizo ya kupanda kwa gharama ya maisha, hali inayoilazimisha serikali za Magharibi kufikia makubaliano na Kremlin: Kupunguza msaada wao kwa Ukraine kwa mabadilishano ya nishati ya Urusi.

Chanzo cha picha, EPA
Mpaka sasa, Ulaya inaonekana imejitayarisha vizuri kwa msimu wa baridi kuliko Moscow ilivyotarajiwa.
Mwezi Oktoba haukuwa na baridi sana kama ilivyo kawaida na ongezeko la gesi asilia ya kimiminika ya akiba ambayo hifadhi yake imekamilika na pia bei ya gesi barani Ulaya imepungua.
Lakini kama viwango vya joto vikipungua, shinikizo linaweza pia kuongezeka. Hasa nchini Ukraine, ambapo jeshi la Urusi limekuwa likishambulia miundo mbinu yake.
3. Ukusanyaji wa raslimali kwa operesheni maalum ya kijeshi
Katika siku za hivi karibuni tumemuona Vladimir Putin akichukua hatua za kuhamasisha uchumi wote wa Urusi na viwanda kwa mahitaji ya "operesheni maalum ya kijeshi" yake.
Kwa njia nyingi inahisi kama nchi nzima imekuwa kwenye vita ya muda mrefu. Ishara, labda, kwamba Kremlin sasa inajiandaa kwa ajili ya vita vya kufa kupona nchini Ukraine.
4. Uharibifu wa pande zote mbili
Kanuni ya vita baridi bado ni halali hadi leo. Inafikiriwa kwamba kama upande mmoja ukiwaka moto, upande wa pili utajibu ipasavyo na kila mmoja atakufa. Hakuna washindi katika vita vya nyuklia. Putin anajua hilo.
Haya yote ni kwa msingi wa kuamini kuwa hakutakuwa na nyuklia katika vita vya Ukraine. Lakini bila shaka, kuna tatizo. Mantiki ilitoweka Februari 24, na vita si lazima vita kufuata mwelekeo fulani.
5. Kuchukulia upinzani wa Ukraine kwa uzito mdogo
"Operesheni maalum" ya Putin haijaenda kulingana na mpango. Kile kilichopaswa kuchukua siku au wiki kadhaa tayari imechukua miezi kadhaa. Kremlin inaonekana kabisa haikuchukulia upinzani wa Ukraine kwa uzito mkubwa. Magharibi kuunga mkono Kyiv na wimbi la vikwazo vya kimataifa ambavyo Urusi ingekabiliana nayo.
Pamoja na kuwahakikishia mwanzoni kwamba "wanajeshi mahiri" pekee ndio watapigana, Rais Putin ameishia kutangaza "usajili wa wanajeshi wa ziada". Zaidi ya hapo, wanajeshi wa Urusi wamekuwa wakipoteza maeneo walioyateka katika majuma ya hivi karibuni kutokana na mashambulizi ya Ukraine.
Lakini ni nadra kwa Putin kukiri kufanya makosa. Kwa sasa, inaonekana amedhamiria kuendeleza vita hivi na kuibuka na kitu ambacho anaweza kukiita ushindi.















