Asilimia 70 ya chui ulimwenguni wako India-Utafiti

Kulingana na Sensa ya Chui iliyotolewa hivi karibuni, kwa sasa kuna Chui 3,167 nchini India. Idadi imeongezeka hadi zaidi ya 200 katika miaka minne iliyopita.

Ongezeko la asilimia 6.7 la idadi ya Chui kufikia 2022 ikilinganishwa na 2018. Kulingana na takwimu za 2018, kulikuwa na chumba 2,967 nchini India, huku mwaka jana idadi yao ilifikia 3,167.

Waziri Mkuu Narendra Modi Jumapili alitoa ripoti juu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya kampeni ya Mradi wa Chui. Kulingana na hilo, asilimia 70 ya chui ulimwenguni wanakadiriwa kuwa nchini India.

"Sio tu juu ya kuokoa chui, bali pia tumetoa mfumo mzuri wa ikolojia kwa ajili yao kustawi," Modi alisema.

Mradi wa Chui

Inakadiriwa kwamba chui elfu 80 waliuawa kati ya 1875 na 1925. Katika siku hizo, wafalme na maafisa wakuu walikuwa wakienda kuwinda na kutoa thawabu kwa wale walioua chui. Hali hii iliendelea hadi miaka ya 1960. Matokeo yake, idadi yao ilipungua kwa kasi.

Serikali ya India imechukua hatua za kumlinda chui wa kitaifa.

Mnamo 1972, serikali ya wakati huo ilileta Sheria ya Kulinda Uhai wa Misitu.

Pamoja na kupiga marufuku uwindaji, kambi za uhamasishaji zilipangwa katika vijiji ili kuokoa wanyama hao. Sheria zililetwa kwa ajili ya ulinzi wa wanyama.

Wameleta sheria kali kuwa kunasa na kuua wanyama wa msituni ni marufuku na wasifanye mambo hayo hata wakikabiliwa.

Ka mtika uendelezo wa hayo, Waziri Mkuu wa wakati huo Indira Gandhi alizindua mradi wa chui mwaka 1973.

Kama sehemu ya hayo, mikoa 9 ya kwanza ya nchi ilitangazwa kuwa Hifadhi ya Tiger.

Bandipur Tiger Sanctuary huko Karnataka, Hifadhi ya Kitaifa ya Corbett huko Uttarakhand, maeneo 9 ya hifadhi ya chui yameanzishwa katika eneo la kilomita za mraba elfu 18.

Miaka hamsini baada ya kuanzishwa kwa Mradi wa chui, kuna hifadhi 54 za chui kote nchini. Eneo la msitu lililofunikwa na chui limeongezeka kutoka kilomita za mraba elfu 18 hadi kilomita elfu 75. Ni asilimia 2.4 ya eneo la ardhi ya nchi, kulingana na ripoti iliyotolewa na Waziri Mkuu Modi.

Kuongezeka kwa idadi ya chui

Tangu 2006, idadi ya chui imekuwa ikiongezeka kwa njia yenye afya.

Kulingana na hesabu za 2022, idadi ya chui katika Siwalik (safu za milima na mabonde ya mafuriko yanayoenea kutoka Himalaya magharibi mwa Nepal hadi Uttarakhand) na Gangetic (maeneo ya bonde la mito ya Indus, Ganges, Brahmaputra) Kaskazini na Kati mwa India, imeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Uhamaji wa chui pia umeongezeka katika maeneo mapya ya Madhya Pradesh na Maharashtra.

Tume ya Kitaifa ya Kuhifadhi inakadiria kwamba kulikuwa na chui 1,411 nchini India mwaka wa 2006. Wakati huo watu wanaopenda wanyama-pori walikuwa wakisema kwamba chui wanakaribia kutoweka nchini India.

Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya chui, serikali pia imetangaza misitu ya hifadhi kuwa hifadhi ya chui.

Kulikuwa na chui 1,411 nchini India mwaka 2006 na 1,706 mwaka 2010; 2,226 kufikia 2014; 2,967 kufikia 2018; 3,167 kufikia 2022.

Kuongezeka kwa idadi ya chui ni nzuri. Lakini mwanaharakati wa ulinzi wa wanyama Arun Prasanna alisema kuwa mbinu ya kuhesabu wanyama hao haiwezi kuaminiwa kabisa. Mchakato wa kuhesabu ni wa kiufundi tu.

Alisema kuwa hakuna ushiriki wa binadamu katika tafiti hizo.

Huhesabiwa vipi?

Mbinu zilizotumiwa kukadiria idadi ya chui katika siku za mwanzo za Mpango wa Kuhifadhi ziligeuka kuwa zisizo za kisayansi. Kuhesabu chui mara nyingi husababisha makosa katika idadi yao.

"Siku hizo walihesabiwa kulingana na nyayo zao. Haiwezekani kukadiria kwa usahihi idadi ya chui walio nao," Kalidas aliiambia BBC.

"Idadi ya chui waliotajwa katika Hifadhi za chui za Panna huko Madhya Pradesh na Hifadhi ya Sariksa huko Rajasthan sio sahihi. Hakuna chui halisi katika misitu hiyo," Kalidas alisema.

Uwindaji haramu wa wanyama hao uliletwa kwa serikali kuu mwaka 2005 na wanaharakati wa haki za wanyama kote nchini. Baada ya hapo Tume ya Kitaifa ya Kuhifadhi Chui iliundwa kwa ajili ya uhifadhi wa chui.

Baada ya kuundwa kwa tume, mbinu ya hivi punde ya kuhesabu na kamera, 'Camera Drop', ilipatikana.

Kamera zimewekwa katika maeneo ambayo chui huzurura na idadi yao inahesabiwa kulingana na picha za chui zilizorekodiwa ndani yao.

Programu maalumu hutumiwa kutambua kupigwa kwenye ngozi ya chui inayoonekana kwenye picha hizo.

"Kama alama za vidole vya binadamu, kupigwa kwenye ngozi ya chui ni tofauti. Hakuna chui wawili walio na mistari sawa. Hii itasaidia kuepuka kuwahesabu mara mbili," anasema Kalidas.

Mgogoro wa chui na binadamu

Ingawa idadi ya chui imeongezeka hadi zaidi ya elfu 3, makazi yao yanapungua kwa sababu ya msongamano wa watu na mipango ya maendeleo katika maeneo mengi. Afisa wa zamani wa Idara ya Misitu ya India alifichua kwamba karibu asilimia 30 wako mbali na makazi yao.

Maeneo yaliyopandwa mimea kwa ajili ya kuongeza kijani kibichi katika miji pia yanaunganishwa katika maendeleo ya maeneo ya misitu. Takwimu za serikali zinaonesha kuwa maeneo ya misitu yameongezeka. Lakini kwa kweli eneo la msitu halitoshi kwa chui,” alisema Mwanabiolojia wa Misitu Osai Kalidas.

Kadiri idadi ya chui inavyoongezeka nchini India, kuna kuchelewa kutangaza maeneo ya hifadhi kuwa maeneo ya misitu iliyolindwa.

Matokeo yake, chui wanakuja kwenye makazi. Kwa sababu ya hii, mzozo wa wanyama hao na binadamu unatokea.

Kutokana na matatizo yanayowakabili makabila na wenyeji, misitu ya hifadhi imegeuzwa kuwa hifadhi za katika maeneo mengi. Hata hivyo, wanamazingira wanapendekeza kwamba serikali ifanye kulingana na mbinu.

Mnamo 2021, waziri aliamuru kuua chui wa T23 katika mkoa wa Masinagudi wa Tamil Nadu kwani alikuwa akiua wanadamu. Baada ya hapo, kwa kuingilia kati kwa mahakama, chui aliwekwa dawa na kuwekwa chini ya ulinzi na kuwekwa katika bustani ya wanyama.

"Kwa upande wa T23 Puli kulikuwa na upinzani wa watu pale, watu walidai kuiua, lakini hakuna anayejua kwanini inashambulia hivyo, sijui ni chui anaua na kula watu," alisema. Arun Prasanna.

Wapenzi wa wanyama wanataka serikali kuchukua hatua ili kuondokana na matatizo hayo kati ya binadamu na wanyama pori. Inasemekana kwamba ikiwa hatua za kutumia silaha zitachukuliwa, chui hawataacha makazi yao.

Kuwinda chui

Huko India, chui 127 walikufa mnamo 2021 na chui 121 mnamo 2022 kwa sababu tofauti. Kulingana na Tume ya Kitaifa ya Kuhifadhi chui, idadi ya chui waliouawa na ujangili ni kubwa.

Takribani chui 52 walikufa hadi wiki ya kwanza ya Aprili 2023.

Chui wanakufa kwa sababu ya ujangili. Osai Kalidas alisema kuwa walinzi hao wanapaswa kupewa vifaa na msaada wa kiufundi ili kuwazuia.

"Ili kulinda wanyama pori kama chui na tembo dhidi ya ujangili, wanapaswa kutambuliwa kwa msingi wa satelaiti na kufuatiliwa mara kwa mara," Arun Prasanna alisema.

"Tunachukua hatua zote zinazohitajika kudhibiti ujangili wa chui," SB Yadav, Mkurugenzi wa Ziada wa Idara ya Misitu ya India, aliliambia shirika la habari la PTI.

Katika Ghats Magharibi kando ya pwani ya magharibi ya India, kuna kupungua kwa idadi ya simbamarara.

Ripoti hiyo ilionesha kuwa idadi ya chui imetoweka katika baadhi ya maeneo ya hifadhi na kuna haja ya kuchukua hatua kali za uhifadhi wa wanyama hao katika majimbo kama Andhra Pradesh na Jharkhand.

Ripoti hiyo pia ilionesha changamoto za mipango mikubwa ya maendeleo ya kiuchumi, kusawazisha uhifadhi wa wanyamapori, matatizo yanayosababishwa na binadamu na wanyamapori, athari kwa makazi ya chui kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, na biashara haramu ya wanyamapori.

"Kuongezeka kwa idadi ya chui ni ishara nzuri. Lakini, hatupaswi kuridhika na hilo. Hatua za lazima zichukuliwe kulinda mazingira yetu ya misitu. Juhudi zote muhimu kwa maisha ya chui zinahitaji kudumishwa," ripoti hiyo ilipendekeza.