"Nekonomics": Uwezo wa nguvu ya paka katika uchumi wa Japani

Mbali na kuvutia idadi kubwa ya watu, paka walisaidia kuinua uchumi wa Japani wakati wa janga la covid-19.

Kulingana na Katsuhiro Miyamoto, profesa aliyestaafu katika Chuo Kikuu cha Kansai, jambo aliloliita "nekonomics" (athari za kiuchumi za paka) lilisababisha takribani dola bilioni 14.6 (yen trilioni 1.9) katika kipindi cha 2021 pekee.

Ili kufikia takwimu hii ya juu, uchunguzi ulizingatia gharama za chakula, mahitaji ya msingi na huduma ya mifugo, pamoja na miradi inayotokana na shauku ya Japani kwa paka.

Hata wale ambao hawana wanyama nyumbani mara nyingi huenda kwenye migahawa na maeneo ya watalii, kama vile visiwa vinavyojulikana kwa mkusanyiko wa paka, ili tu kupiga picha na kuwagusa paka.

Huko Japan, neno la mlio wa paka ni "nyan nyan nyan", ambalo linasikika kama "ni" (mbili kwa Kijapani).

Kulingana na mchezo huu wa maneno na kwa pendekezo la tasnia ya chakula cha wanyama, mnamo mwaka 1987 ilianzishwa Februari 22 kwamba itakuwa Siku ya Paka, na hivyo kuunda sababu moja zaidi ya kuongeza neno "nekonomics".

Kwa Wajapani wengi, kupuuza kutazama paka ni vigumu kama vile kupinga maelfu ya vitu vya kupendeza ambavyo sekta ya paka hujivunia kipindi hiki cha mwaka.

Kulingana na Shirika la Chakula cha Wanyama Japani, umaarufu wa paka umekuwa ukiongezeka kwa zaidi ya miongo miwili.

Janga hili lilisababisha shauku hii kuongezeka zaidi kwani watu walilazimishwa kujitenga nyumbani.

Idadi ya paka hao iliandikisha rekodi mwaka wa 2021, na kuongeza wengine 489,000 zaidi ikilinganishwa na kipindi cha awali, ambacho kiliandikisha jumla ya paka nchini kufikia milioni 8.94 (ikilinganishwa na mbwa milioni 7.10).

Profesa Miyamoto alizidisha idadi hii kwa wastani wa gharama ya kila mwezi ya Dola za Marekani 63 (kama yen 8,460) ambazo huingia nchini humo kwa ajili ya kulisha na matunzo ya kimsingi ya kila mnyama.

Kiasi hicho kinafikia Dola za Kimarekani milioni 6,758 kwa mwaka (kama yen milioni 911,580)

Kwa kiasi hicho kilijumuishwa kwa kile kilichotolewa na utalii wa ndani wa paka: jumla ilikuwa karibu dola bilioni 14.6 (karibu yen trilioni 2).

Kwa kulinganisha, 'nekonomics' katika mwaka 2021 ni ya juu kidogo kuliko ile iliyotumika kuandaa Michezo ya Olimpiki na Walemavu ya Tokyo 2020 (iliyokadiriwa kuwa $12.528 milioni au yen trilioni 1.69).

Profesa Miyamoto anakumbusha kwamba gharama ya kutunza paka mdogo ni ya chini kwa familia, lakini kwa Japan inamaanisha kitu kikubwa sana.

"Kwa maneno mengine, mrundikano wa kiasi kidogo kwa kila familia huchangia uchumi wa Japani, hii ndio inayowapa msukumo wa kuendelea na hili," anasema katika mahojiano na BBC News Brazil.

Shirika la Chakula cha Wanyama Japani kinakumbuka kwamba watu walipatwa na hali ya wasiwasi na mfadhaiko walipolazimika kuacha kwenda nje na ilibidi wakae nyumbani na kufanya kazi kutoka huko kwa muda mrefu.

Wanapoishi na wanyama wanaowapenda, wao hutafuta amani na utulizu wa akili na kuboresha mawasiliano ndani ya familia zao.

Urahisishaji wa hatua za kukabiliana na virusi vya corona na ongezeko la bei la hivi karibuni kwa bidhaa na ushuru wa nishati nchini unapaswa kuwa na athari kwa 'nekonomics', lakini ni mapema sana kusema itakuwa kiasi gani.

Kile ambacho hakiwezi kupuuzwa ni kwamba daima kutakuwa na ongezeko la idadi ya wapenzi wa wanyama wa nyumbani nchini Japani.

Mbwa au paka, uchaguzi utategemea sana nafasi na wakati unaopatikana kuwahudumia..

Paka waliotelekezwa

Katika utafiti huo, Miyamoto anaorodhesha mfululizo wa mambo kwa nini Wajapani wanapenda paka.

Miongoni mwao, anataja kuwa watu wengi zaidi wanahamia kwenye vyumba vya mijini ambavyo pamoja na kuna watu wengi, mara nyingi wanyama kama mbwa hawaruhusiwi, lakini wanaweza wasijali sana uwepo wa paka, ambao pia ni rahisi kuwatunza na kuhitaji uangalifu mdogo, kama kuwapeleka kwa matembezi.

Hata hivyo, sio paka wote wanatunzwa vizuri. Kulingana na uchunguzi uliofanywa na Wizara ya Mazingira ya Japani, katika mwaka wa fedha wa 2020, idadi ya paka waliochukuliwa kutoka kwa wamiliki wao ili kuasiliwa ilifikia takriban 10,000.

NGO ya TNR Felinos Japón, Shirika lililoanzishwa na Elen Tanaka na Cássio Silva, eneo la Iwata (jimbo la Shizuoka), linafanya kazi kama kipimajoto kutathmini hali hii ya paka kutelekezwa.

Wanandoa hao wa Brazil wameshuhudia ongezeko la paka wengi, ikiwa ni pamoja na wanyama wengine wa kufugwa wanaotelekezwa.

Baada ya shauku ya awali, watu wengi huacha kutunza paka baada ya gundua kuwa kutunza mnyama hata paka mdogo, ni kazi kubwa na inagharimu pesa.

Hivyo, huishia kuwatelekeza wanyama na huishia kuhamishiwa kwa wale waliojitolea kuwapa hifadhi wanyama hao.

Cássio anasema kwamba gharama za shirika hilo zimeongezeka sana. Kwa sasa, yeye na mke wake wanalipa takriban dola za Marekani 963 (yen 130,000) kukodisha sehemu mbili: moja inatumika kama nyumba ya wanandoa na nyumba nyingine ni ya paka 100 waliokolewa, na kutunzwa na wote wawili wakati wakisubiri watu wanaoweza kuwaasili.

Kodi ni sehemu ndogo zaidi ya gharama za kusaidia paka wengi. Mbali na kunyonya mshahara wa Cássio kama mfanyakazi katika kiwanda cha vipuri vya magari, Shirika hilo linatumia muda wake wote kutunza wanyama hao ambao hupokelewa na mke wake Elen, kwa kuwa wanyama wengi hufika wakiwa wamedhoofika kutoka mitaani.