Mzozo wa DRC: Je, kutekwa kwa mji wa Bukavu kunamaanisha nini?

g

Chanzo cha picha, MONUSCO

Maelezo ya picha, Bukavu ni mji muhimu Mashariki mwa DRC
    • Author, Ambia Hirsi
    • Nafasi, BBC Nairobi
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Hatua ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Bukavu ambao ni wa pili kwa ukubwa katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kunaonekana kulemaza juhudi za kikanda na kimataifa za kutafuta ufumbuzi wa mzozo unaoendelea kufuta kati ya nchi hiyo na taifa jirani la Rwanda.

Waasi hao walichukua udhibiti wa mji huo siku ya Jumapili baada ya kuuteka uwanja wa ndege wa Kavumu uliopo kilomita 30 kutoka Bukavu. Wapiganaji wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wanadai kuwa lengo lao kurejesha hali ya utulivu baada ya majeshi ya Congo kuutelekeza.

Kundi hilo limemeendelea kuteka miji ya Congo katika hatua ambayo haujawahi kushuhudiwa tangu lilipoanzisha uasi wake wa 2022, ulioathiri mamlaka ya Kinshasa mashariki.

Jimbo la Kivu Kusini likiangukia mikononi mwa M23, siku moja baada ya Rais wa DR -Congo Félix Tshisekedi kuongoza mkutano wa usalama kujadili hali inayoendelea kuwa mbaya mashariki mwa DRC.

Tshisekedi alisema amepata uungwaji mkono wa kidiplomasia kutoka kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU), ambao wamelaani jukumu la Rwanda katika mzozo wa DRC na kudai kuwa wanafanyia kazi vikwazo dhidi ya Kigali.

Licha ya wito wa kikanda na kimataifa wa kusitisha mapigano ya mara moja, mapigano yanaendelea kati ya wanajeshi wa M23 na FARDC, huku serikali ya Congo ikiituhumu Rwanda kuhusika moja kwa moja.

Soma pia:

Kwanini M23 inaitaka Bukavu

Baadhi ya watu walijitokeza kuwashangilia wapiganaji wa M23 walipoingia Bukavu bila upinzani siku ya Jumapili

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Baadhi ya watu walijitokeza kuwashangilia wapiganaji wa M23 walipoingia Bukavu bila upinzani siku ya Jumapili

Bukavu, ni jiji la mashariki mwa Congo, lililopo kwenye rasi inayoenea hadi Ziwa Kivu. Ni kituo cha kibiashara na kiviwanda, bandari ya ziwa, na jiji la kitalii lililo na barabara inayounganisha eneo la kaskazini-magharibi hadi Kisangani, kusini-magharibi hadi Kasai, kusini hadi Lubumbashi, na eneo zima la Afrika Mashariki.

Kutokana na vita vya muda mrefu vilivyokumba eneo la mashariki mwa Congo mtandao wa barabara umezorota na barabara kuu za Goma, Kisangani na miji mingine imekuwa katika hali mbaya.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Uwanja wa ndege uliotekwa Ijumaa iliyopita ulikuwa kizuizi cha mwisho kikubwa cha kijeshi kwa vikosi vya waasi kabla ya kufika Bukavu, jiji la ambalo lina zaidi ya watu milioni moja.

Serikali ya Congo inasisitiza kwamba inafanya kila linalowezekana "kurejesha utulivu, kurejesha usalama na mamlaka yake".

"Bukavu, Goma na maeneo mengine yote yanayokaliwa kwa mabavu ya Kivu Kaskazini na Kusini ni ishara kwamba tunakabiliana na adui. Tutaendelea kupambana wakati huu mgumu, kusimama na jeshi letu na Mkuu wa Nchi, Mkuu wa Majeshi," alisema Muyaya.

Serikali ya Kinshasa ilitangaza hayo baada ya jeshi la Congo (FARDC) kutangaza Jumatano wiki iliyopita kwamba linadhibiti mji wa Bukavu, lakini picha na ripoti kutoka kwa wakazi wa jiji hilo ziliwaonyesha wapiganaji wa M23 wakiendelea kuingia kwa mji huo kwa wingi.

Kanisa Katoliki la Bukavu na Jumuiya ya Kiraia ya Kivu Kusini linaonya kuwa jiji hilo linaweza kukumbwa na umwagaji damu mwingi.

Picha zilizonaswa na majeshi ya serikali zinawaonyesha wakikimbia Kavumba kuelekea Bukavu, wakisema walisalitiwa, wamechoka kupigana bila vifaa, na bila chakula, hivyo waliamua kuachana na mapambano.

Uwezo wa kijeshi wa M23

M23

Chanzo cha picha, M23

Kufikia Januari 2025, makadirio yanaonyesha kuwa vikosi vya M23 vina wapiganaji kati ya 3,000 na 4,000. Zaidi ya hayo, ripoti kutoka Umoja wa mataifa zinaonyesha kuwa wanajeshi wa Rwanda wanaunga mkono operesheni za M23, ingawa Rwanda imekuwa ikikanusha vikali madai ya kuhusika kwake.

Aidhaa Rwanda imeendeleza madai kwamba kundi la wapiganaji la FDRL ambalo lilitajwa kuhusika katika vita vya kimbari vya 1994, lilikimbilia DRC na linatumiwa na taifa hilo kuendeleza muaji ya kimbari ndani ya Mashariki mwa DRC, jambo ambalo Kinshasa imekanusha vikali pia.

M23 imeonyesha uwezo mkubwa wa kijeshi, ikiwa ni pamoja na:

Vita vya Kawaida: Kikundi kinatumia mikakati ya kijeshi ya kawaida, kuwawezesha kukamata na kudhibiti miji muhimu kama vile Goma.

Mbinu za mapigano ya miguu: Pia hutumia mbinu za kutembea, kuruhusu operesheni za kupambana zinazonyumbulika na zinazobadilika.

Silaha Nzito Nzito: M23 inamiliki silaha na silaha nzito, ambazo zimetumika katika mashambulizi ya hivi majuzi. Vile vile, wapigaji wake wanavalia sare rasmi za kijeshi na silaha kali , nyinginezo zikiwa za kisasa.

Mchanganyiko wa uwezo huu umewezesha M23 kuleta changamoto kubwa kwa Wanajeshi wa DRC na kudhibiti maeneo ya kimkakati ndani ya eneo hilo.

Udhibiti wa M23 kwa sasa

X

Mashambulizi ya hivi majuzi ya M23 yamebadilisha kwa kiasi kikubwa hali ya usalama mashariki mwa DRC. Tangu mwishoni mwa 2021, kundi hilo limeanzisha mashambulizi mapya, na kukamata maeneo ya kimkakati:

  • Goma (Januari 2025): Januari 27, 2025, wapiganaji wa M23 walitoa taarifa ya kuuteka Jiji la Goma, jiji kubwa zaidi mashariki mwa DRC. Mapigano ya silaha yalizuka karibu na uwanja wa ndege, na kuwalazimu maelfu ya raia kukimbia. Hili linaashiria mafanikio kwa M 23, kwani Goma ni kitovu muhimu cha kiuchumi na kiutawala.
  • Sake, Masisi, Babmbiro na Luberoo, maeneo haya yalitekwa moja baada ya nyingine kuanzia katikati mwa Mwezi Desemba 2024. Wapiganaji waliyateka miji hiyo muhimu, Sake ikiwa kilomita 23 kutoka Goma.
  • Minova: wiki chache zilizopita, M23 iliteka mji wa biashara wa Minova, na kupata njia muhimu za ugavi na maeneo ya kiuchumi.
  • Eneo la Rutshuru (2022): M23 ilichukua udhibiti wa maeneo kadhaa katika eneo la Rutshuru, ikiwa ni pamoja na mji wa mpaka wa Bunagana, na kuwawezesha kutoza ushuru haramu kwenye njia za biashara.
  • Mafanikio haya ya kimaeneo yameimarisha msimamo wa M23 huku yakivuruga uthabiti wa kikanda.

Rwanda inahusika?

Kuibuka tena kwa M23 kunafungamana kwa karibu na ushindani wa kikanda, hasa kati ya DRC, Rwanda na Uganda. Rwanda imeshutumiwa kwa kuunga mkono M23 kwa msaada wa silaha na uendeshaji, madai ambayo imekuwa ikikanusha mara kwa mara.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa mwaka 2022 iliangazia ushahidi wa Vikosi vya Ulinzi vya Rwanda kusaidia M23, na kuzidi kuzorotesha uhusiano kati ya Kigali na Kinshasa.

Kwa mtazamo wa Rwanda, M23 inatumika kama kikosi kinzani dhidi ya Forces Democratiques de Libération du Rwanda (FDLR), wanamgambo wa Kihutu ambao wanajumuisha watu waliohusika na mauaji ya kimbari ya 1994 ya Rwanda.

Rwanda inaona kuvunjwa kwa FDLR kama kipaumbele chake cha usalama.

Wakati huo huo, Uganda imefuata maslahi yake nchini DRC, ikiwa ni pamoja na miradi ya miundombinu na njia za biashara.

Ushindani huu wa ushawishi, pamoja na maslahi ya madini ya kikanda na masuala ya usalama, vimechochea mvutano.

Maelezo zaidi: