Kiongozi wa waasi na ushiriki wake katika machafuko ya Rwanda na DRC

Sultani Makenga

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,
    • Author, Wedaeli Chibelushi
    • Nafasi, BBC News
  • Muda wa kusoma: Dakika 6

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekwama vitani, wanamgambo wa kundi la M23 limekuwa vitani dhidi ya jeshi la kitaifa na kudhibiti sehemu muhimu zote kwa mkoa wa mashariki.

Katika kipindi cha wiki chache tu, idadi kubwa ya watu wameuawa na vita vilevile vimechangia vita vya maneno kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na jirani yake, Rwanda.

Basi, jinsi gani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, nchi kubwa zaidi kusini mwa jangwa la Sahara imefika hapa?

Asili ya mzozo huu inaweza kueleweka kupitia hadithi ya mtu mmoja, kiongozi wa M23, Sultani Makenga, ambaye amekuwa akihusishwa na mashtaka mashtaka mbalimbali ya uhalifu wa kivita.

Tukirejea maisha ya Makenga hadi sasa ni kutazama miongo kadhaa ya vita, uingiliaji wa kigeni kwa muda mfupi na mvuto wa raslimali za madini za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Maisha yake yalianza katika Siku ya Krismasi mwaka 1973, alipozaliwa katika mji wa kijani wa Masisi, DRC. Alilelewa na wazazi wa kabila la Tutsi, na Makenga aliacha shule akiwa na umri wa miaka 17 ili kujiunga na kikundi cha waasi wa Tutsi kilichozunguka mpaka wa Rwanda.

Kikundi hiki, kilichoitwa Rwandan Patriotic Front (RPF), kilikuwa kinadai uwakilishi bora wa Watutsi katika serikali ya Rwanda, ambayo wakati huo iliongozwa na wanasiasa kutoka kwa kabila la Hutu. Walikuwa pia wanataka wakimbizi wa Tutsi waliofukuzwa nchini Rwanda kwa sababu ya vurugu za kikabila kurudi nyumbani.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa miaka minne, Makenga na RPF walipigana na jeshi la Hutu. Vita vyao vilichanganyika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, ambapo wapiganaji wa Hutu waliwaua Watutsi 800,000 na Wahutu wastani.

Akikumbuka kipindi hiki katika mahojiano nadra ya mwaka 2013, Makenga alisema: "Maisha yangu ni vita, elimu yangu ni vita, na lugha yangu ni vita... lakini mimi ninaheshimu amani."

RPF ilipiga hatua na kuchukua ardhi zaidi na zaidi kabla ya kuingia mji mkuu wa Kigali na kuangusha serikali ya Hutu iliyokuwa na itikadi kali, wengi wao walikimbilia katika kile kinachoitwa sasa DRC.

Baada ya RPF kuchukua madaraka, Makenga alijumuishwa katika jeshi rasmi la Rwanda na kupanda cheo hadi kuwa naibu kamanda wa kikosi na kufikia cheo cha sajenti.

"Alikuwa mzuri sana katika kuanzisha mtego," alisema mmoja wa wapiganaji wenzake wa RPF kwa shirika lisilo la kiserikali la Rift Valley Institute.

Hata hivyo, maendeleo yake katika jeshi la Rwanda yalikwama. Uhalisia kwamba alikuwa na elimu ya chini na alizungumza kifaransa na kingereza kidogo ulileta "kikwazo kwa taaluma yake ya kijeshi," ilisema Rift Valley Institute.

M23

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mnamo 1997, alikuwa sehemu ya vikosi vilivyoungwa mkono na Rwanda ambavyo mwishowe vilikamata madaraka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), na kumng'oa mfalme wa muda mrefu Mobutu Sese Seko.

Kwa niaba yake walimweka madarakani kiongozi wa zamani wa waasi wa Congo, Laurent Kabila.

Hata hivyo, Makenga alianza kusigana na wakuu wake, alikamatwa na mamlaka za Rwanda baada ya kukataa amri ya kurudi Rwanda, ripoti ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ilisema.

Alifungwa kwa miaka kadhaa katika kisiwa cha Iwawa.

Wakati huo, uhusiano kati ya Kabila na viongozi wapya wa Rwanda ulianza kudhoofika. Rwanda ilikuwa inataka kuangamiza wanamgambo wa Hutu waliokuwa na jukumu la mauaji ya kimbari lakini walikimbilia ng'ambo ya mpaka mwaka 1994.

Hofu ya Rwanda ilikuwa ni kwamba wangerejea na kuvuruga utulivu wa nchi ambao ulikuwa umejijengea kwa nguvu.

Lakini Kabila alishindwa kuzuia wanamgambo hao kujiandaa na pia alianza kuwafukuza wanajeshi wa Rwanda.

Matokeo yake, Rwanda ilivamia DRC mwaka 1998. Wakati Makenga alipotolewa jela, aliteuliwa kuwa kamanda kwenye mstari wa mbele akiwa na kikundi cha waasi kilichoungwa mkono na Rwanda.

Vijana wa Goma

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Vurugu za hivi karibuni katika harakati za kuelekea Goma na ndani ya jiji lenyewe inaripotiwa kuwa zimesababisha vifo vya maelfu ya watu ndani ya wiki mbili tu.

Kwa miaka mingi, alijijengea sifa ya kuwa na mikakati ya hali ya juu na mtaalamu katika kuongoza vikundi vikubwa vya wanajeshi vitani.

Baada ya wanajeshi wa Rwanda kuvuka mpaka na kuingia DRC, kulikuwa na ongezeko la ubaguzi dhidi ya jamii ya Tutsi. Kabila alidai kuwa Tutsi walikuwa wakiunga mkono uvamizi huo, huku maafisa wengine wakichochea umma kushambulia wanajamii wa kabila hilo.

Makenga, akiwa bado DRC, alimtuhumu kiongozi wa Congo kwa kumtenga miongoni mwa wapiganaji wa Kitutsi, akisema: "Kabila alikuwa mwanasiasa, lakini mimi siyo. Mimi ni askari, na lugha ninayojua ni ya bunduki."

Nchi kadhaa jirani zilikuwa zimejumuishwa katika mzozo huo na kikosi kikubwa cha jeshi la Umoja wa Mataifa kilitumwa kujaribu kudumisha utulivu.

Zaidi ya watu milioni tano wanadhaniwa kufa katika vita na athari yake, wengi kutokana na njaa au magonjwa.

Vita rasmi vilimalizika mwaka 2003 lakini Makenga aliendelea kutumika katika vikundi vya silaha vinavyopingana na serikali ya Congo.

Katika mchakato wa urejeshaji amani, waasi wa Tutsi kama Makenga mwishowe walijumuishwa katika jeshi la serikali ya Congo, katika mchakato uitwao "mixage".

Lakini upepo wa kisiasa nchini DRC unabadilika kila wakati, Makenga alikimbia hatimaye kutoka jeshi na kujiunga na uasi wa M23 ulioendelea kutokea.

M23 ilizidi kuwa na shughuli nyingi mashariki mwa DRC, wakisema kwamba wanapigana kulinda haki za Watutsi, na kwamba serikali ilikuwa imeshindwa kutekeleza makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka 2009.

Makenga alipewa cheo cha jenerali wa M23, kisha muda si mrefu, nafasi ya juu zaidi.

Mnamo Novemba 2012 aliongoza waasi katika mapinduzi makali, ambapo waliteka mji wa Goma, jiji kubwa la mashariki lenye idadi ya watu zaidi ya milioni moja.

DRC na Umoja wa Mataifa waliilaumu serikali ya Rwanda inayotawaliwa na Tutsi kwa kuunga mkono M23, tuhuma ambazo Kigali imekuwa ikikanusha mara kwa mara.

Lakini hivi karibuni, majibu rasmi yamebadilika, na wasemaji wa serikali wakisema kuwa vita karibu na mpaka wao ni tishio la usalama.

Mwaka 2012, Makenga na wengine katika M23 walikuwa wakikabiliwa na tuhuma kubwa za uhalifu wa kivita.

Marekani iliwekea vikwazo, ikisema kwamba alihusika katika "kuajiri watoto kama wanajeshi, na kampeni za ukatili dhidi ya raia." Makenga alisema tuhuma kwamba M23 ilitumia watoto kama wanajeshi "hazikuwa na msingi".

Umoja wa Mataifa nao ulisema kwamba alifanya, na anahusika katika vitendo kama vile mauaji na kusababisha ulemavu, ukatili wa kijinsia na utekaji.

Sultani Makenga

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Makenga amekuwa akihusika katika uasi kadhaa dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Pamoja na kuzuiwa kwa mali, Makenga alikumbana na mgawanyiko mkali ndani ya M23. Upande mmoja ulimuunga mkono kama kiongozi, wakati mwingine ulimuunga mkono mpinzani wake, Jenerali Bosco Ntaganda.

The Enough Project, shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi nchini DRC, lilisema kwamba pande hizo mbili ziliingia katika "vita kamili" mwaka 2013 na kutokana na hayo, wanajeshi watatu na raia wanane walikufa.

Upande wa Makenga ulishinda na Jenerali Ntaganda alikimbilia Rwanda, ambapo alikabidhiwa kwa ubalozi wa Marekani.

Akitambulika kama "Terminator" kutokana na ukatili wake, Jenerali Ntaganda mwishowe alihukumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa kifungo cha miaka 30 kwa uhalifu wa kivita.

Hata hivyo, miezi michache baada ya ushindi wa Makenga, tishio jingine kubwa lilitokea. Umoja wa Mataifa ulituma kikosi cha wanajeshi 3,000 chenye jukumu la kusaidia jeshi la Congo kurejesha Goma, jambo lililosababisha M23 kujiondoa.

Kikundi cha waasi kilifukuzwa nchini na Makenga alikimbilia Uganda, nchi ambayo pia imekuwa ikituhumiwa kwa kuunga mkono M23, tuhuma ambazo inakanusha.

Uganda ilipokea ombi la kumrudisha Makenga kutoka DRC, lakini haikuchukua hatua.

Miazi minane ilipita. Vikundi vingine vingi vya silaha vilizunguka mashariki mwa DRC yenye raslimali za madini, vikileta uharibifu, lakini mamlaka za Congo zilikuwa huru na magaidi maarufu zaidi.

Hii ilikuwa hadi mwaka 2021.

Makenga na waasi wake walichukua tena silaha, wakiteka maeneo katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Mapatano kadhaa ya kusitisha mapigano kati ya M23 na mamlaka za Congo yalishindwa, na mwaka jana hakimu alimhukumu Makenga kifo bila kuwepo mahakamani.

Wakati wa harakati za hivi karibuni za M23, ambapo inasemekana waasi wanasaidiwa na maelfu ya wanajeshi wa Rwanda, Makenga hajaonekana hadharani.

Badala yake, ameacha hotuba za umma na matamko kwa msemaji wake, na Corneille Nangaa, ambaye anasimamia muungano wa vikundi vya waasi ikiwemo M23.

Lakini Makenga bado ni muhusika muhimu, akiwa anaonekana kuzingatia mikakati nyuma ya pazia.

Amesema vita vyake visivyokoma vimekuwa kwa ajili ya watoto wake watatu, "ili siku moja wawe na maisha bora katika nchi hii."

"Sipaswi kuonekana kama mtu asiyetaka amani. Nina moyo, familia, na watu ninaowajali," alisema.

Lakini mamilioni ya watu wa kawaida wanailipa gharama ya mzozo huu na ikiwa atakamatwa na vikosi vya Congo, Makenga aTakutana na adhabu ya kifo.

Ndio, hajakata tamaa.

"Niko tayari kutoa kila kitu," alisema.