Ni nani wanaohusika na mzozo wa DR Congo?

..

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda limesema linataka kuikomboa DR Congo
Muda wa kusoma: Dakika 7

Uvamizi wa waasi wa M23 katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya demokrasi ya Congo (DRC) lenye utajiri wa madini umesababisha mzozo wa kibinadamu na kidiplomasia, ukihusisha mataifa kadhaa jirani.

Idadi kubwa ya majeshi ya Kiafrika tayari yamepeleka vikosi vyao kwenye eneo la mapigano, ambalo lina historia ndefu ya kuingiliwa kutoka nje.

Jamhuri ya demokrasi Congo ni kubwa kiasi kwamba ni theluthi mbili-za ukubwa wa Ulaya Magharibi, hivyo ni mwanachama wa jumuiya mbili za Kiafrika; Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Makundi haya mawili ya jumuiya yanajiunga ili kufanya mkutano wa dharura Jumamosi kujaribu kumaliza mapigano haya.

Hivyo basi, ni nani wahusika wakuu na wanataka nini?

Jamhuri ya Kidemokrasi a ya Congo - ' Nchi kubwa iliyogubikwa na mzozo'

..

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa Jamhuri ya demokrasi ya Congo, Félix Tshisekedi, anasema kuwa nchi yake imevamiwa.

Rais wa Congo Félix Tshisekedi anataka kurudisha ardhi aliyoipoteza kwa waasi, ikiwemo mji mkubwa wa mashariki wa Goma, na kuzuia waasi hao kuchukua zaidi.

Anamshutumu Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa kuunga mkono waasi wa M23 kwa silaha na wanajeshi, akiishutumu Kigali kwa kuuvamia mpaka wa Congo kwa lengo la kuiba mali ya nchi hiyo na kupanga mageuzi ya utawala.

Mashtaka kwamba Rwanda inaunga mkono mashambulizi ya M23 yanatokana na ushahidi uliowasilishwa katika ripoti ya Umoja wa mataifa na ambao unaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na serikali nyingi za Afrika na za Magharibi, ambazo zimeitaka Kigali kujiondoa na vikosi vyake.

Hata hivyo, kinachomshangaza Tshisekedi, hakuna yeyote aliyejizatiti kwa kauli yao na kuitikia wito wa Kinshasa wa vikwazo na hatua kali nyingine.

Rais wa Congo pia ana wasiwasi kuhusu kuimarisha utawala wake."Nadhani usalama wa kisiasa wa serikali yake uko hatarini," alisema Jason Stearns, aliyewahi kuwa mpelelezi wa Umoja wa mataifa huko DR Congo na kwa sasa ni profesa katika Chuo Kikuu cha Simon Fraser.

Kuna wasiwasi kwamba harakati za M23 zinaweza kuhamasisha upinzani wa ndani au kusababisha mapinduzi kwenye jeshi lake, ambalo lina sifa ya kugawanyika na kudhoofishwa na rushwa.

Unaweza pia kusoma

Rwanda - 'Muhusika mkwepaji'

..

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, "Rais Paul Kagame wa Rwanda anasema anapigana na vikundi vya waasi vinavyohusiana na mauaji ya kimbari."
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Katika mgogoro huu, kiongozi wa muda mrefu wa Rwanda, Kagame, ndiye amekuwa akitajwa, lakini amekuwa mzoefu katika kujiepusha.

Ana historia ndefu ya kuingilia kijeshi ndani ya DR Congo kunakohusishwa na matokeo ya mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994.

Rwanda imekuwa ikikanusha kutoa msaada wa kijeshi kwa M23, lakini mara kwa mara inasisitiza itafanya kinachohitajika kujilinda.

Kagame anasisitiza kuwa kipaumbele cha Rwanda ni kuangamiza kundi linalo miliki silaha lililoundwa na wahusika wa mauaji ya kimbari ya wahutu, ambao waliua Watusi wa Rwanda na kisha kutoroka hadi kunakotajwa sasa kuwa mashariki mwa DR Congo.

Amewashutumu wanajeshi wa DR Congo kwa kuungana nao na wengine kuua Watusi wa Congo - ambao M23 inadai inawalinda - lakini pia kutishia Rwanda.

Katika kiwango cha kidiplomasia, Rwanda inataka uthibitisho wa madai hayo kwamba mgogoro ni tatizo la Congo, na Kigali inajilinda tu dhidi ya vita vya kiraia.

Inadai kwamba Kinshasa ijadiliane moja kwa moja na M23, jambo ambalo inakataa kufanya.

Lakini kile inachotafuta kwa kweli, amesema Bwana Stearns, ni "kuimarisha hali ya ushawishi katika eneo la mashariki mwa DR Congo".

...

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, "Marafiki na ndugu wanatazama miili ya waliofariki wakati M23 ilipoteka Goma katika mashambulizi mapya."

Rwanda ina maslahi ya kiuchumi na usalama.

Kigali inakanusha ushahidi wa UN kwamba inasafirisha dhahabu na madini mengine kutoka mashariki mwa Jamhuri ya demokrasi ya Congo na kuyauza kama yake.

Lakini upatikanaji wa utajiri wa madini nchini DR Congo umekuwa ni chanzo cha mizozo katika eneo hilo kwa miongo kadhaa.

Kuna wengine katika mzozo huu, ikiwemo uhasama binafsi kati ya Kagame na Tshisekedi. "Kagame anataka kumfundisha Tshisekedi somo kuhusu ni nani mwenye nguvu kwenye eneo hilo," alisema Richard Moncrieff, anayefuatilia eneo la Maziwa Makuu kutoka taasisi inayoshughulikia mizozo Afrika (ICG). "Wanyarwanda wataendelea kupigana mpaka atakapofanya makubaliano na... awape uhuru zaidi katika mkoa wa mashariki wa North Kivu," aliongeza.

Burundi - 'Jirani mwangalifu'

..

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, amekuwa na uhusiano mgumu na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwa miaka mingi.

Rwanda inalichukulia jeshi la Burundi kama tishio jingine la usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya demokrasi ya Congo (DRC).

Nchi inayopakana na Rwanda na DRC imekuwa na maelfu ya wanajeshi huko kwa miaka mingi.

Walikwenda kuwafuatilia waasi wa Burundi lakini sasa wanasaidia jeshi la Kinshasa katika vita dhidi ya M23.

Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi ni mbaya.

Nchi hizi mbili zina muundo wa kikabila unaofanana lakini kinyume na Rwanda, Hutu ndiyo wanaoshikilia madaraka nchini Burundi.

Nchi zote mbili zimekashifiana kwa kudai kujaribu kuangusha serikali zao.

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ametoa onyo kali kwenye mitandao ya kijamii.

"Ikizidi, Rwanda itaendelea na mashambulizi," aliandika, "Najua vita vitafika Burundi… Siku moja atataka kuingia Burundi - hatutakubaliana na hilo. Vita vitapanuka."

Tishio hili litakuwa kubwa zaidi ikiwa M23 itaendelea na mashambulizi kutoka Goma kuelekea mkoa wa Kivu kusini karibu na mpaka wa Burundi, ambapo vikosi vyake viko.

"Kile kinachotafutwa na Burundi hapa ni kuokoa utawala wake," alisema Bw. Stearns.

"Burundi inahofia kuwa kama vikosi vya Rwanda vitaimarisha ushawishi wao katika eneo la Kivu kusini, inaweza kuteteresha serikali ya Bujumbura. Kile kilicho hatarini hapa ni kuzima uasi huu kabla haujaingilia karibu zaidi."

Wengine wanahofia kurudi kwa vita mbili zilizoshambulia eneo hilo mwishoni mwa miaka ya 1990, ambazo zilihusisha nchi tisa na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu.

Mara hii, mapigano ya moja kwa moja kati ya majeshi mawili yanaweza kupelekea mgogoro wa DRC kuvuka nje ya mipaka yake.

Uganda-'mcheza pande zote'

..

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameshutumiwa kwa kuwa pande zote mbili

Uganda haihusiki moja kwa moja, lakini pia ina wanajeshi mashariki mwa DR Congo.

Wanasaidia serikali ya Congo kwa tishio tofauti la usalama - kuwawinda wanamgambo wenye asili ya Uganda ambao wanahusishwa na kundi la Islamic State.

Lakini jukumu la Uganda ni la kutatanisha – inafanya kazi na Wacongo, huku pia ikidaiwa kutoa usaidizi kamili kwa M23. Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaripoti kwamba imewaruhusu kutumia eneo la Uganda kama kambi na njia ya safari zao.

Kampala inakanusha vikali hilo. Lakini imejibu mashambulizi ya M23 kwa kuweka wanajeshi wake katika "mkao wa mbele wa kujihami," ili kuzuia makundi mengine yenye silaha kutumia vibaya mgogoro huo, imesema.

Wakaazi wa eneo hilo wameripoti kuona wanajeshi wa Uganda wakielekea eneo la mapigano, na hivyo kuzidisha hofu ya kuongezeka kwa eneo hilo.

Kama ilivyo kwa Rwanda, Uganda imeingia mashariki mwa DR Congo siku za nyuma ikidai kulinda mipaka yake. Lakini pia inashutumiwa kwa kupora maliasili, hasa dhahabu.

Wachambuzi wanasema kuwa italinda maslahi yake ya kiuchumi huku ikiwatupia jicho Wanyarwanda.

"Ni wazi kwamba Uganda inataka kubaki na ushawishi wake katika eneo la mashariki mwa DR Congo na sio kusukumwa na mpinzani wake nchini Rwanda," anasema Bw Moncrieff wa ICG.

Afrika Kusini - 'Mlinda amani anayechagua upande'

..

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Cyril Ramaphosa alijikuta katika mvutano mkali mtandaoni na kiongozi wa Rwanda Paul Kagame kuhusu mzozo wa DR Congo.

Afrika Kusini imechangia wanajeshi wengi katika kikosi cha jumuiya ya Kusini mwa Afrika kinachopigana pamoja na jeshi la Congo na imepata hasara kubwa.

Lakini pia imegonga vichwa vya habari kwa sababu ya majibishano ya kushangaza kati ya Kigali na Johannesburg hivi karibuni.

Raia wa Afrika Kusini walishutumu vifo vya wanajeshi wao 14 kusababishwa na Vikosi vya Rwanda, ambavyo Rais Cyril Ramaphosa alivitaja kwa dharau kuwa "wanamgambo wa RDF."

..

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Raia wa Congo nchini Afrika Kusini wamekuwa wakiandamana kupinga mzozo nchini mwao kwa miongo kadhaa

Waziri wake wa ulinzi alidai kwamba alimuonya Kagame kwamba kuendeleza mashambulizi zaidi ingetafsiriwa kama tangazo la vita.

Hii ilimkasirisha rais wa Rwanda, ambaye alisema kwamba maelezo yao yalikuwa "uongo" na kutoa wito kwa Afrika Kusini akiita "kikosi katili cha kivita" ambacho lazima kiondoke DR Congo.

Hii ni sehemu ya mgawanyiko kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

EAC inaiunga mkono Rwanda katika wito wake wa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Kinshasa na M23.

Wakati SADC inalaani mashambulizi ya RDF dhidi ya wanajeshi wake, wakiwemo wanajeshi wa Tanzania na Malawi, na imesisitiza kuheshimiwa kwa uhuru, mamlaka, na umoja wa DR Congo.