Kwa nini Hispania ni moja ya nchi zinazoongoza kwa matumizi ya kokeni duniani?

jk

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Atahualpa Amerise
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Uhispania ni moja ya nchi ulimwengu yenye matumizi makubwa ya kokeni. Tafiti mbalimbali za kimataifa zinaiweka Uhispania kuwa miongoni mwa masoko makuu ya kokeni.

Kulingana na Ripoti ya Dawa ya Ulaya ya 2025, 13.3% ya Wahispania wenye umri wa kati ya miaka 15 na 64 wametumia kokeni angalau mara moja katika maisha yao, hiyo ni idadi kubwa zaidi katika bara Ulaya, juu ya 9.4% nchini Ufaransa na Denmark, na 8% nchini Uholanzi.

Nje ya umoja wa Ulaya, Uingereza, Australia, na Marekani zinajiunga na Uhispania kwa kuwa na viwango vya juu vya watumiaji wa dawa hii.

Polisi wa Uhispania walikamata tani 118 za kokeni 2023, zaidi ya robo ya tani 419 zilizokamatwa kote Ulaya na ndio tani kubwa zaidi baada ya tani 123 zilizokamatwa nchini Ubelgiji.

Nchini Uhispania, kokeni inahusika katika 60% ya vifo vinavyohusiana na dawa za kulevya na nusu ya vifo hivyo ni kutokana na kuzidisha kiasi cha dawa, ni takwimu ambazo ni mara mbili ya wastani wa takwimu za Ulaya.

"Kuna matumizi makubwa ya kokeni katika nchi hii ambayo hayazungumzwi." Onyo hili linatoka kwa mwandishi wa habari David López Canales, katika kitabu chake kilichochapishwa mwaka huu.

Uhispania imekuwaje mojawapo ya watumiaji wakubwa wa kokeni duniani?

Kokeni kufika Uhispania

k

Chanzo cha picha, David López Canales

Maelezo ya picha, Kitabu cha David López Canales kimefungua upya mjadala wa umma kuhusu matumizi ya dawa hii hatari.

"Baada ya kuongezeka kwa dawa hii katika miaka ya 1970 huko Marekani, Miami ukawa ndio mji mkuu wa ulimwengu, kokeni ilienea hadi Uhispania na Ulaya," anaelezea Víctor Méndez, mwandishi wa habari aliyebobea juu ya dawa za kulevya, na mwandishi wa vitabu viwili juu ya ulanguzi wa dawa za kulevya, na mwanzilishi wa tovuti ya Narcodiario.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mapema miaka ya 1980, eneo la kaskazini-mashariki la Galicia likawa lango kuu la kokeni kuingia bara Ulaya, kokeni inayozalishwa Amerika ya Kusini na kusambazwa na magenge yenye nguvu.

Kisha walanguzi mashuhuri wa dawa za kulevya wa Colombia kama vile Gilberto Rodríguez Orejuela na Ochoa brothers waliichagua Uhispania kama kituo cha usambazaji kwa usafirishaji wao kwenda Ulaya.

"Kutoka hapo, walijenga mtandao ambao bado unatumika hadi leo," anasema Méndez.

Baadhi ya kokeni iliyofika Galicia ilibaki Uhispania, ilikuwa rahisi kuisambaza kwa sababu ya ukosefu wa mipaka ya ndani. Mahitaji yalianza kukua wakati wa ustawi wa kiuchumi na uhuru mkubwa zaidi wa kijamii kufuatia demokrasia mpya kuanzishwa baada udikteta wa Francisco Franco (1939-75).

Katika miaka ya awali, kokeni nchini Uhispania haikupatikana kwa watumiaji wa kawaida, na ilitumiwa tu katika mazingira fulani kama ishara ya hadhi na mafanikio.

Taswira yake Ilikuwa ni dawa ya kisasa, ghali, na ya kipekee iliyosambazwa kwa watu wa ngazi ya juu katika jamii – hasa wafanyabiashara, wafanyakazi wa benki, na wasanii.

Lakini kwa miaka, hilo lilibadilika. Poda hiyo nyeupe ilivuka madaraja ya kijamii na vizazi, ikawa sehemu ya maisha ya kila siku ya Wahispania wengi wa kawaida.

Hali ilivyo sasa

k

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maafisa wa usalama hufanya ngumu ya kuzuia usafirishaji wa kokeini kwenye pwani ya Galician.

Wataalamu wanakubali kwamba, kokeni inaonekana ni ya kawaida – huku wengine wakitaka uhuru zaidi wa matumizi ya kokeni nchini Uhispania, pia bei yake imebakia vilevile kwa zaidi ya miongo minne.

Hilo linachangiwa na ukweli kwamba usambazaji wa kokeni umeendelea kukua katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na kuongezeka mara kwa mara kwa uzalishaji, licha ya sera za kupiga marufuku na juhudi za kimataifa za kuizuia.

"Kuongezeka kwa uzalishaji nchini Colombia na Peru kunamaanisha wingi wa upatikanaji wa kokeni zaidi, safi zaidi na ya bei nafuu, kote Ulaya," anasema Joan R. Villalbí, mjumbe wa serikali ya Uhispania katika Mpango wa Kitaifa wa Kupambana na Dawa za Kulevya.

Villalbí anaelezea kuwa kokeni kwa sasa ni "dawa haramu ambayo huagizwa zaidi katika vituo vya matibabu ya uraibu" nchini Uhispania.

"Kimsingi hutumika katika maeneo ya burudani, katika Mkesha wa Mwaka Mpya, siku za kuzaliwa, sherehe za ndani... Haichukiwi sana katika kijamii," anasema Antonio Jesús Molina, profesa wa saikolojia ya jamii katika Chuo Kikuu cha Complutense cha Madrid na mwandishi wa tafiti kadhaa kuhusu dawa za kulevya.

Mwenendo huu unatofautisha Uhispania na nchi zingine za umoja wa Ulaya na Uingereza, ambapo matumizi huwa ya mtu binafsi na ya siri.

Katika kitabu chake, mwandishi anasema moja ya sababu ya kuonekana ni jambo la kawaida, ni kutokana na mtindo wa maisha, ambapo burudani za kijamii huchukua kipaumbele, na kokeni inakuwa sehemu ya karamu hizo, wakati mwingine sambamba na pombe.

Anaonya, matumizi haya ya kokeni kama burudani katika jamii hupunguza kuizingatia hatari yake kwa afya za watumiaji. Kama vile, kuchanganyikiwa, moyo kwenda mbio, hatari ya magonjwa ya akili, mashambulizi ya moyo, na kiharusi kibaya.

Utalii

k

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Matumizi ya madawa ya kulevya ni ya kawaida katika maisha ya usiku ya maeneo ya kitalii kama Ibiza.

Jambo jingine kubwa ni utalii: Wageni milioni 83.7 walitembelea Uhispania mwaka jana pekee, ni nchi ya pili iliyotembelewa zaidi ulimwenguni; maeneo kama vile Costa del Sol, Barcelona, Madrid, na Visiwa vya Balearic na Canary yana utajiri wa maisha ya usiku.

Kulingana na Víctor Méndez, mmiminiko mkubwa wa watalii huwezesha usambazaji na kuongeza matumizi ya kokeni.

"Kwa wafanyabiashara, ni mahali pazuri pa kujificha na kuchanganyika na watalii. Hiyo inazalisha mahitaji, sio tu kwa Wahispania bali pia kwa wageni wengine," anaelezea.

Wakati wa miaka ya 1980 na 1990, heroini ilipokuwa ikileta uharibifu kwa vijana wa Uhispania, kampeni za kupinga dawa za kulevya nchini Uhispania zilikuwa za moja kwa moja.

Ingawa heroini ilisemwa sana na vyombo vya habari na wanasiasa, kutokana na athari zake mbaya, kokeni iliachwa nyuma, bila kupewa uzito sawa katika kampeni hizo na sera za umma.

Kulingana na López Canales, ukosefu huu wa umakini kwa kokeni, uliwezesha kuingizwa kwake katika maisha ya kila siku na kutozungumzwa sana kwa umma, hadi ikawa kitu cha kawaida.