Ipi athari ya wasiwasi kati ya Israel na Misri kuhusu mpaka wa Gaza?

Chanzo cha picha, Egyptian Armed Forces Military Spokesman Page - Facebook
- Author, Hisham Al-Mayani
- Nafasi, BBC
- Akiripoti kutoka, Cairo
- Muda wa kusoma: Dakika 6
Mkuu wa Majeshi wa Misri Ahmed Khalifa alifanya ziara isio ya kawaida siku ya Jumatano kukagua hali ya usalama kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza.
Hatua yake ilijiri siku moja baada ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutangaza nia yake ya kuweka majeshi ya Israel katika udhibiti wa mpaka wote wa Gaza na Misri ikiwa ni pamoja na Ukanda wa Philadelphi na kivuko cha Rafah, baada ya kuuteka mwezi Mei, na kuishutumu Misri kwa kutofanya vya kutosha kuzuia silaha kufika Ukanda huo kupitia mahandaki.
Mkuu huyo wa Majeshi wa Misri alisema akiwa umbali wa mita moja kutoka ukuta unaotenganisha wanajeshi wa Misri na wanajeshi wa Israel kwamba dhamira kuu ya jeshi la Misri ni kulinda mipaka ya nchi hiyo.
Alisema: "Vikosi vya jeshi la Misri vina uwezo wa kulinda mipaka ya nchi hiyo kutoka kizazi baada ya kizazi.
Ni ujumbe ambao baadhi walielewa kumaanisha kuwa Misri ilipeleka vikosi vya jeshi lake la ardhini katika eneo la Sinai kando ya mpaka wake na Gaza kujibu uwepo wa jeshi la Israel katika Ukanda wa Philadelphi ambao ilijiondoa mwaka 2005, na kwamba kupuuza masharti ya makubaliano hayo pia kunaweza kuafikiwa na Misri.
Israel inasema kuwa wanajeshi wake wamegundua mahandaki kadhaa katika eneo hilo, huku Misri ikikanusha kuwa hakuna njia zinazounganisha pande hizo mbili, i na kusisitiza kuwa matamshi hayo ya Israel yanalenga kuendeleza kusalia kwa majeshi ya Israel katika mhimili huo na kuharibu makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano mbali na kubadilishana silaha. na wafungwa.
Haya ndio majibu ya wanajeshi wawili wa zamani kutoka israel na Misri.
Ni ujumbe gani ambao Misri inataka kutuma kutoka kwa Mkuu wake wa majeshi ?
Wataalamu hao wawili wa kijeshi walikubaliana kwamba kulikuwa na ujumbe kadhaa uliobebwa na ziara ya Mkuu wa Majeshi wa Misri kwenye mpaka na Gaza, muhimu zaidi ni kwamba "Misri inazingatia sana kile inachosema na kwamba haitakubali Israeli kukiuka ahadi yake.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Samir Farag, jenerali wa zamani na mkurugenzi wa idara ya maadili ya jeshi la Misri, aliambia BBC kwamba Cairo ilitaka kutuma ujumbe kadhaa kupitia ziara ya afisa huyo kwenye mpaka.
Alieleza kuwa ujumbe wa kwanza ni "kwa mwanajeshi wa Misri aliye mpakani, ambapo tunamwambia kuwa Mkuu wa Majeshi mwenyewe alikuja kukujulia hali na kwamba unaelewa na unaijua vyema kazi yako.
Ujumbe wa pili, kwa mujibu wa Farag, ni “kuwahakikishia watu wa Misri kwamba mipaka yao imelindwa vyema na kwamba Mkuu wa Majeshi na viongozi wakuu wameweka mipango mipya ya ulinzi katika mipaka hiyo.
Kuhusu ujumbe wa tatu, Farag alisema ni "kwa yeyote anayehusika, kujua kwamba jeshi la Misri liko tayari kulinda mipaka ya Misri kuelekea kaskazini mashariki.
Lakini kulingana na Kobi Lavi, mshauri wa zamani wa Wizara ya Ulinzi ya Israel, ni kwamba ziara ya Mkuu wa Majeshi wa Misri ilifanyika kwa sababu nne. Ya kwanza ni kwamba, "Misri inaiambia Hamas kwamba inafanya kile inachosema na kwamba ina uzito juu yake, na kwamba haitaki Israeli kukiuka sheria na kuwa na vikosi vyake kwenye kivuko cha Rafah au Ukanda wa Philadelphi.
Sababu ya pili, kulingana na Kobi, ni "kutuma ujumbe kwamba kurejea kwa Ukanda wa Philadelphi kwenye udhibiti wa Hamas haimaanishi kwamba inaruhusiwa kuchimba mahandaki mapya na kwamba Misri haitakubali hilo," akibainisha kuwa uwepo wa Mkuu wa Majeshi mwenyewe katika eneo hilo ina maana kwamba Misri itafanya kila iwezalo kukataa uwepo wa Israel huko, lakini wakati huo huo haitakubali kuingiliwa kwa usalama wa taifa wa Misri na Hamas.
Kobi alieleza kuwa sababu ya tatu ni kwamba Misri inaiambia Marekani na nchi zinazohusika katika faili ya migogoro ya Waarabu na Israel kwamba Cairo haikubali uwepo wa Waisraeli kwenye kivuko cha Rafah au ukanda wa Philadelphi kwa sababu hii inakinzana na makubaliano yaliyofikiwa kuhusu suala hilo.
Amesisitiza kuwa sababu ya nne ni kutuma ujumbe kwa Israel kwamba Misri haitakubali kuwepo kwa majeshi ya Israel huko Rafah au Philadelphi na kwamba jambo hilo linakiuka mikataba iliyohitimishwa, na kama vile Cairo inavyojizatiti katika makubaliano hayo, Israel nayo lazima ijitolee.
Israel inadhibiti Ukanda wa Philadelphi, ambao ni eneo la amani lenye usalama na kwamba linawakilisha ukanda wa njia tatu kati ya Misri, Israel na Ukanda wa Gaza unaoenea kwa umbali wa kilomita 14, na inakataa kuondoka katika eneo hilo.
Kijiografia, ukanda huu wa mpaka kati ya Misri na Ukanda wa Gaza unaenea kutoka Bahari ya Mediterania upande wa kaskazini hadi kivuko cha Kerem Shalom kusini.
Israel inaamini kuwa mhimili huu wa mpaka na Misri ndio lango kuu la Hamas kupata silaha zinazosafirishwa kwa njia ya magendo kupitia mahandaki yanayopitia chini yake, lakini Misri inaamini kwamba mipaka yake iko chini ya udhibiti, na kwamba hakuna mahandaki au magendo katika ardhi yake.
Ni nini kinachosababisha mabishano kuhusu mahandaki licha ya uthibitisho wa Misri kwamba yaliharibiwa?

Chanzo cha picha, Egyptian Armed Forces Military Spokesman Page - Facebook
Samir Farag alithibitisha kwa kina kwamba "hakutakuwa na makabiliano ya kijeshi kati ya Misri na Israel, na juhudi za kidiplomasia zinafanywa kutekeleza makubaliano ya amani na kuyazingatia kikamilifu."
Mnamo Machi 25, 1979, Misri ilitia saini mkataba na Israeli ambapo nchi hizo mbili zilithibitisha kujitolea kwao kwa "Mpango wa Amani katika Mashariki ya Kati Uliokubaliwa Camp David" wa Septemba 17, 1979.
Mkataba huo unakataza tishio au matumizi ya nguvu kati ya wahusika wake na kuwalazimu kutatua migogoro yote inayotokea "kwa njia za amani."
Makubaliano hayo ya kihistoria pia yalidhibiti namna ya kuwepo kijeshi kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili na kamati ya pamoja ya uratibu wa kijeshi iliundwa.
Je, mazungumzo ya mapatano yataathiriwa na msisitizo wa Misri na Hamas wa kukataa uwepo wowote wa Israel katika Ukanda wa Philadelphi na kivuko cha Rafah?

Chanzo cha picha, Egyptian Armed Forces Military Spokesman Page - Facebook
Amir Farag anasema kuwa Hamas inasisitiza juu ya kuondoka kwa Israel kutoka Gaza yote, ikiwa ni pamoja na Philadelphi, kama kanuni ambayo mazungumzo ya kusitisha mapigano yameegemezwa, "na hii ni haki yake kwa sababu hii ni ardhi yake," akibainisha kuwa Israel, kwa upande wake, haitaki kujitoa kabla ya kuwaachilia mateka wake wote wanaoshikiliwa na Hamas, na yote haya, bila shaka, yanatishia kuzuia mazungumzo ya mapatano kukamilika.
Kwa upande wake, Lavi anasema, "Hii kwa hakika inazuia juhudi za kufikia mapatano kwa sababu Hamas haitaki amani au utulivu kwa sababu hiyo inakinzana na maslahi ya Iran."
Amesisitiza kuwa "Israel inahofia kwamba ikiwa itauacha Ukanda wa Philadelphi, Hamas itaanzisha upya mahandaki hayo na kuwasafirisha mateka wa Israel hadi Iran, na hilo litakuwa ni kosa kubwa la kijasusi la Israel na kushindwa kijeshi.
Je, ni kwa kiasi gani Misri na Israeli ziko wazi kwa maelewano yoyote ili kupunguza mvutano kati yao?
Samir Farag anasema kuwa Misri ndiyo nchi ya kwanza kuathiriwa na yale yanayotokea Gaza kwa upande wa Israel, na usalama wa taifa la Misri hivi sasa upo hatarini, na hivyo basi Misri inaunga mkono suluhu yoyote ya kweli itakayopelekea kutuliza hali katika mipaka yake.
Kwa upande wake, Kobi Lavi anasisitiza kuwa iwapo kutakuwa na pendekezo au maelewano yatakayofanikisha matakwa ya usalama ya Israel, haitayakataa ili kutuliza mivutano na Misri, kwa sababu Israel haioni Misri kuwa ni adui. Kinyume chake, imeishi pamoja na Misri bega kwa bega tangu kusainiwa kwa makubaliano ya amani miaka 40 iliyopita .
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












