Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi MI-5 ilivyobadili sera yake kufuatia vita vya Urusi nchini Ukraine
Mkuu wa idara ya ujasusi ya Marekani MI5 Ken McCallum anasema sera yake kuhusu mtandao wa ujasusi wa kigeni imeathiriwa vibaya tangu Urusi ilipoingia vitani na Ukraine. McCallum pia amesema Uingereza inapaswa kujiandaa kwa ajili ya kuendelea kwa vita vya Urusi kwa miaka mingi ijayo.
Katika ripoti yake ya mwaka, mkuu wa ujasusi alisema kuwa wafanyakazi 600 wa balozi za Urusi kote duniani wameondolewa, ambapo walau 400 kati yao wanaweza kuwa ni majasusi.
"Hili ni pigo kubwa zaidi la kimkakati kwa ujasusi wa Urusi katika historia ya Ulaya," alisema.
Mkuu wa MI-5 anasema majasusi 23 wa Urusi waliojificha katika huduma za kibalozi wamefukuzwa kutoka Uingereza pekee.
"Lakini hatuwezi kutegemea hilo tu," aliongeza mkuu wa kupambana na ujasusi wa Uingereza, "lazima tujiandae kwa uchokozi wa wazi na wa moja kwa moja kutoka Urusi katika miaka ijayo."
Kulingana na mkuu huyo wa ujasusi nchini Uingereza, Urusi itaendelea kuitishia Uingereza sio tu kwa majasusi na mashambulizi ya kimtandao, bali pia katika mfumo wa usambazaji wa taarifa za upotoshaji kwa umma kwa kupandisha bei za vyanzo vya za nishati.
"Wataendelea kukiuka maadili ya kazi zao," alitahadharisha.
Tisho la Iran na China
Kulingana na Bw McCallum, Iran na China zimeendelea kuwa juu katika orodha ya nchi zinazotishia usalama wa Uingereza. Mwaka huu MI5 iligundua takriban majaribio kumi ya Iran ya kuwateka nyara na kuwauwa watu wanaoishi Uingereza. Pia iliwezekana kuzuia mashambulio ya ugaidi manane.
Wiki iliyopita, polisi ya Uingereza ilitoa tahadhari kwa waandishi wa habari Wairan wanaoishi nchini humo kwamba maisha yao yamo katika hatari.
.McCallum alisema kuwa MI5 ilikuwa inafanya kazi kwa ushirikiano na wafanyakazi wake nchini humo pamoja na wafanyakazi wenzao wa kigeni kuzuia "vitendo vibaya zaidi".
Alisema iran inaendelea na "vitendo vyake vya kukera" kote Ulaya. Tisho jingine lkubwa na ambalo la muda mrefu kwa mkuu wa MI5, ni China.
Inatumia raslimali nyingi kufanya ujasusi kuhusu tawala za maadui wake na kuwatishia inapohisi ni lazima. Kwa mfano, wafanyakazi wa ubalozi mdogo wa Uchina katika Manchester walimshambulia mshiriki wa maandamano ya vuguvugu la demokrasia.
"Tunaona kujitokeza kwa aina hizi mpya za ukandamizaji," mkuu wa MI5 alisema, na kuongeza kuwa Beijing huanzisha vituo tofauti vya polsi ng’ambo inapona ni muhimu kufanya hivyo.
Ingawa ilisema rasmi kwamba vituo hivi huwasaida Wachina kutatua matatizo ya kiutawala , kulingana na baadhi ya ripoti, huwalazimisha raia wa China kurudi nchini mwao kwa njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na unyang’anyi.
"Hatuta kubali vitendo vya vitisho na unyanyasaji wa rai awa Uingereza au wale wanaochagua kuishi nchini Uingereza ," McCallum alisema.
Mwezi januari, MI5 ilionya juu ya juhudi zisio za kawaida za Wachina kuwa na ushawishi katika siasa za Uingereza.
Kulingana na mkuu wa ujasusi, huduma maalumu ya Uchina haitasita kujaribu kuingilia masiha ya ndani ya nchi kwa kuwalaghai mawakala ambao ndio wanaanza kazi au ambao ni wagombea wa ubunge nchini Uingereza.
Mashambulio ya ugaidi na silaha zilizotengenezwa kwa mashine ya kuchapisha ya 3-D printer
Ugaidi umesalia kuwa tisho kuu, lakini sio tisho baya kama lilivyokuwa katika miaka iliyopita.
Tangu mwaka 2017, MI5 imefanya kzi na polisi kuzuia mashambulio 37 ya ugaidi yaliyopangwa na makundi yenye itikadi kali ya Kiislamu na makundi mengine yenye itikadi kali.
Kulingana na McCallum, MI5 inachunguza kujikusanya tena kwa makundi ya kimataifa ya ugaidi. Huduma maalumu pia zinaangalia kuhusu suluhu ya tatizo gumu la kipekee la ugaidi wa watu binafsi na kuwazuia kutekeleza uhalifu bado ni changamoto.
Bw McCallum pia alitaja kwamba jasusi za kupata silaha zinaendelea kuongezeka , zikiwemo, silaha za 3-D-printed (CS).
Sio tu hizo, mamia ya Warusi waotolewa na serikali ya Urusi kuchukua nafasi za wanadiplomasia waliofurushwa walinyimwa vibali vya kusafiria- visa, jambo lililofanyika kwa ajili ya maslahi ya usalama wa taifa.