Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ziara ya Kamala Afrika: Je Marekani inaweza 'kupora'' ushawishi wa China Afrika?
Na Anne Soy, BBC
Kwanza alikuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani aliyefanya ziara Afrika, lakini sasa ni makamu wa rais na baadaye mwakani rais mwenyewe wa Mraekani, Joe Biden anatarajiwa kuja Afrika.
Mfulululizo wa ziara hizi kwa viongozi wakubwa katika utawala wa Marekani unaonyesha mwamko unaokua kwamba Marekani inahitaji kuimarisha ushirikiano wake na bara hilo.
Haya yote yanakuja katika namna ya ushindani unaokua kutoka kwa mataifa mengine yenye nguvu duniani, hasa China na Urusi.
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris atakuwa na ziara ya siku tisa Afrika akianzia nchini Ghana kabla ya kuelekea Tanzania na Zambia.
Ghana, inayowekeza kuimarisha uhusiano na watu wanaoishi nje ya Afrika na vile vile ikiwa na rekodi ya kubadilishana madaraka kwa njia kidemokrasia na amani, inatoa fursa bora kwa Bibi Harris kuanza kuitembelea.
Safari yake, kulingana na taarifa rasmi, utagusia kuhusu mkutano ujao wa kilele wa mwezi Disemba wa Marekani na Afrika huko Washington ambapo Rais Joe Biden alisema Marekani "imejikita katika mustakabali wa Afrika".
Lakini unaochochewa pia na idadi ya watu vijana na inayoongezeka pamoja na maliasili nyingi za bara hilo, ambazo zimevutia mataifa mengine mengi yenye nguvu yanayowania kuwa na ushawishi Afrika.
Wakati ziara ya hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken huko Ethiopia na Niger, iliangazia changamoto za usalama katika nchi hizo, ziara ya makamu wa rais itampeleka katika mataifa yanayokabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi.
Uchumi unaostawi wa Ghana unapitia kwenye wakati mgumu zaidi wa kifedha katika miongo kadhaa.
Nchi hiyo inayohaha kulipa deni lake la taifa, inakabiliwa na mfumuko wa bei wa zaidi ya 50%. Waziri wa Fedha Ken Ofori-Atta amekuwa Beijing hivi karibuni akiongoza mazungumzo na serikali ya China.
"Hadi sasa, mikutano chanya na ya kutia moyo sana imefanyika nchini China," waziri wa fedha aliandika kwenye mtandao wake wa twitter huku akionyesha matumaini kwamba nchi hiyo itapata usuluhishi "hivi karibuni".
Haijabainika ni eneo gani kama msaada, Bi Harris anaweza kutoa, lakini ziara yake itakuwa chini ya shinikizo la kufanya kitu kama mshirika aliye tayari kusaidia hasa kufuatia ziara ya Bw Ofori-Atta nchini China.
'Marekani ni marafiki - kama ilivyo kwa China na Urusi'
Mchumi na profesa wa fedha katika Chuo Kikuu cha Ghana, Godfred Alufar Bokpin, hafikirii ziara hiyo itatoa "gawio la haraka" kusaidia kupunguza matatizo ya kifedha ya nchi.
"Kuwa na China ni jambo gumu," alisema, huku akibainisha kuwa ziara ya Bi Harris ilikuwa "muhimu sana" kwa Ghana kwani "inainua uhusiano wetu na Amerika hadi kuwa wa kiwango kingine".
Aliiambia BBC maslahi ambayo Marekani inaonyesha nchini humo na mgogoro wake wa madeni "ni mzuri" lakini ana wasiwasi kuhusu kile alichokitaja kuwa "masharti yasiyofaa ya biashara" na mataifa yanayokopesha fedha.
Zambia na yenyewe inapita inayopitia Ghana.
Taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa madini ya shaba lilikuwa la kwanza barani Afrika kutolipa deni lake kwa wakati pale janga la Covid lilipotokea.
Iko katika majadiliano ya muda mrefu na China ili kushughulikia deni lake na pia imeomba msaada wa kifedha kutoka kwa shirika la fedha duniani, IMF.
Shirika la habari la Reuters linamnukuu afisa mkuu wa Marekani akisema Bi Harris "atajadili njia bora za jumuiya ya kimataifa kushughulikia changamoto za madeni zinazokabili nchi za Ghana na Zambia".
Kama Prof Bokpin, mchambuzi wa Zambia Dk Sishuwa Sishuwa anadhani China ina ushawishi zaidi linapokuja suala la kushughulikia madeni. Lakini Marekani na yenyewe inataka kuonekana kama mshirika anayetegemewa zaidi.
Kuna hisia zinazoongezeka barani kwamba Afrika inapaswa kuwa na chaguo huru katika mahusiano yake na taifa lolote duniani.
"Zambia inaiona Marekani kwa namna sawa kama inavyoiona China na Urusi - rafiki," Dk Sishuwa aliiambia BBC.
"Nchi inapoiendea China, au Urusi, au Marekani kwa ajili ya msaada, hii haipaswi kuonekana kama kudharau taifa moja lenye nguvu dhidi ya lingine."
Mashaka yaliyotawala Afrika
China ina sera ya kutoingilia masuala ya kisiasa ya ndani ya nchi - jambo ambalo limepunguza uhusiano wake na viongozi wa kiimla.
Na uwepo wa Urusi katika nchi za Kiafrika ambazo zimekumbwa na mapinduzi hivi karibuni - Burkina Faso na Mali - kumesababisha kudorora kwa uhusiano kati yao na Magharibi, haswa Ufaransa, ambao ulikuwa na uhusiano wa karibu na nchi zote mbili.
Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine bila shaka umeyapa mataifa ya Magharibi hisia ya ziada na ya uharaka katika kushinda mioyo ya nchi nyingi zaidi za Kiafrika.
Kura ya Umoja wa Mataifa kulaani Urusi kuivamia Ukraine iliyagawa mataifa ya Afrika ambayo karibu nusu yalijiweka kando na kutyopiga kura, ikiwa ni pamoja na Tanzania ambayo pia iko kwenye ratiba ya kutembelewa na Bi Harris.
Makamu wa rais wa Marekani - mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo - atakutana na Rais Samia Suluhu Hassan, rais wa kwanza mwanamke wa nchi yake.
Uzoefu huu wa pamoja wa kuwa wanawake wa kwanza kushika nafasi kubwa hizo unazua gumzo nchini Tanzania.
Wengi pia wanapongeza ziara hiyo kama uthibitisho wa maendeleo ambayo nchi inapiga na inavyotegeneza mwonekano wake kwenye ramani ya kimataifa.
Siyo zamani sana Tanzania ilikuwa inaonekana tofauti kimataifa chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, ambaye alionekana kuwa na mienendo ya 'kibabe', iliyopunguza shughuli za upinzani na vyombo huru vya habari.
Bi Harris ndiye kiongozi wa juu wa Marekani katika utawala wa Biden kuzuru Afrika na wa tano tangu mkutano wa kilele wa Marekani na Afrika mwezi Desemba.
Wengine ni Waziri wa fedha Janet Yellen, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield, Mke wa Rais Jill Biden na Bw Blinken.
Lakini pamoja na maslahi mapya yanakuja mahitaji ya bara la Afrika ya kutendewa haki.
Prof Bokpin wa Ghana alisema kuna kiwango cha mashaka kuhusu kukua na kuongezeka kwa nia ya Afrika.
"Kuna imani kwamba kunafanyika ushindani mpya kuigombania Afrika," akirejea kugawanyw kwa bara hilo na mataifa ya Ulaya mwishoni mwa Karne ya 19 ambayo ilisababisha miongo ya ukoloni na unyonyaji.
"Ushirikiano huu unahitaji kusisitiza kuheshimiana," aliongeza.