Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Rashford kurejea Man United?

Rashford

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Hatua ya Manchester United kumtimua Ruben Amorim huenda ikampa nafasi mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 28, ambaye yuko kwa mkopo Barcelona, ​​​kurejea Old Trafford. (Mirror)

Oliver Glasner huenda analengwa na Manchester United kuchukua nafasi ya Amorim aliyefutwa. Uongozi wa klabu hiyo unavutiwa sana Maustria huyo mwenye umri wa miaka 51, ambaye kandarasi yake Crystal Palace inaisha msimu wa joto. (Telegraph - usajili unahitajika)

Fulham inajiandaa kupokea ofa ya Manchester United ya kumsajili meneja wao Mreno Marco Silva. (Sun)

Wachezaji wa klabu ya Manchester United Kobbie Mainoo, 20, Joshua Zirkzee, 24, na Manuel Ugarte, 24, walikuwa na hamu ya kuhama Old Trafford Januari hii laiti Amorim hangeliondolewa . (Mail - usajili unahitajika)

Juventus imeanza kujadiliana na Liverpool kuhusu mpango wa kumsajili Federico Chiesa kwa mkopo, huku mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 28 akiwa tayari kurejea katika klabu hiyo ya Serie A ambayo aliichezea kwa misimu miwili kati ya 2022-2024. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Bournemouth ilikuwa tayari kulipa euro 40m (£34.7m) kwa winga wa Stuttgart na Ujerumani Jamie Leweling kama mbadala wa winga wao wa Ghana Antoine Semenyo, 25, ambaye anakaribia kuhamia Manchester City, lakini klabu hiyo ya Bundesliga ilikataa ofa ya Cherries. (Sky Sports - kwa Kijerumani)

Chelsea italazimika kuchukua hatua haraka ikiwa wanataka kumsajili Jeremy Jacquet, 20, kutoka Rennes, kwa sababu Liverpool, Arsenal, Real Madrid na Manchester United zikimuwania mlinzi huyo wa Ufaransa. (Team talk)

Federico Chiesa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Juventus imeanza kujadiliana na Liverpool kuhusu mpango wa kumsajili Federico Chiesa kwa mkopo

Barcelona imewasilisha dau la kumsajili mlinzi wa Al-Hilal na Ureno Joao Cancelo, 31, kwa mkopo, huku Inter Milan pia wakihitaji. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Mkuu wa soka wa Nottingham Forest Edu anakabiliwa na shaka kuhusu mustakabali wake wa siku zijazo huku klabu hiyo ikiendelea kustahimili msimu wa misukosuko. (Telegraph - usajili unahitajika)

Crystal Palace iko tayari kuchuana na West Ham kumsajili mshambuliaji wa Norway Jorgen Strand Larsen, 25, kutoka Wolves. (Mail - usajili unahitajika)

Cancelo

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson, 33, yuko mbioni kuvunja mkataba wake na West Ham baada ya kuwa nao kwa miezi mitano pekee. (Athletic - usajili unahitajika)

Kocha wa zamani wa Wolves Gary O'Neil amefanya mazungumzo ya kuwa kocha mkuu mpya wa Strasbourg, huku meneja wa sasa wa klabu hiyo ya Ufaransa Liam Rosenior akikaribia kuchukua nafasi ya Enzo Maresca katika klabu ya Chelsea. (Athletic - usajili unahitajika)

Mshambuliaji wa Crystal Palace mwenye umri wa miaka 20 kutoka England, Romain Esse anatarajiwa kutumia muda uliosalia wa msimu huu kwa mkopo katika klabu ya viongozi wa Championship Coventry City. (Sky Sports)

Pia unaweza kusoma:

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi