Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Real Madrid yajiunga na mbio za kumsaka Wharton

Wharton

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Real Madrid itachuana na Chelsea, Liverpool, Manchester City na Manchester United kumsajili kiungo wa Crystal Palace Adam Wharton, 21. (AS - kwa Kihispania)

Crystal Palace ina mapania kufanya sajili kadhaa Januari hii huku beki wa Bayern Munich Mfaransa Sacha Boey, 25, kiungo wa kati wa Wolves wa Brazil Joao Gomes, 24, na kiungo wa kati wa Auxerre Mfaransa Kevin Danois, 21, wakiwa kwenye orodha yao. (Mail+ - usajili unahitajika)

AC Milan inafuatilia hali ya mlinzi wa Uholanzi Nathan Ake, 30, huko Manchester City huku wakitathminii chaguzi kadhaa. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)

Chelsea inaweka pamoja kitita cha pauni milioni 130 katika jaribio la kuishawishi Real Madrid kumuuza winga wa Brazil Vinicius Jr. (Fichajes - kwa Kihispania), mwenye umri wa miaka 25.

Mshambuliaji wa Argentina Taty Castellanos, 27, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya huko West Ham kabla ya kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 27 kutoka Lazio. (Sportsport)

Tottenham ilituma maskauti kumtazama winga Mfaransa Maghnes Akliouche, 23, akiichezea Monaco dhidi ya Lyon Jumamosi. (Team talk)

Winga wa Misri Omar Marmoush

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Winga wa Misri Omar Marmoush

Eintracht Frankfurt wako anajadiliana na Newcastle kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Denmark William Osula, 22. (Florian Plettenberg),

Winga wa Misri Omar Marmoush, 26, anavutiwa na Aston Villa na Tottenham lakini anataka kusalia Manchester City na kupigania nafasi yake. (Football Insider)

Bournemouth inamenyana na Fiorentina, Cagliari na Genoa kumsajili kiungo wa kati wa Atalanta mwenye umri wa miaka 25 Marco Brescianini. (Calciomercato)

Tottenham imeelekeza mawazo yake kwa mlinzi wa Udinese Mfaransa Oumar Solet, 25, lakini inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Chelsea na Crystal Palace. (Caught offside)

Raheem Sterling ameichezea England mechi 82

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Raheem Sterling ameichezea England mechi 82

Sunderland iko tayari kumwachia Luke O'Nien, 31, kuondoka mwezi huu huku Birmingham, Coventry na West Bromwich Albion wakimtaka beki huyo wa Uingereza. (Chronicles)

Beki wa Bournemouth Muargentina Julio Soler, 20, ameonekana kulengwa kwa mkopo na Watford. (Fabrizio Romano),

Barcelona wanafikiria kutoa pauni milioni 70 kutoka kwa Sunderland kwa winga wa Uhispania Fermin Lopez, 22. (Fichajes - kwa Kihispania)

Winga wa England Raheem Sterling, 31, anatazamiwa kupata njia ya kuondoka Chelsea mwezi Januari huku Newcastle ikiwa klabu ya hivi punde zaidi ya Ligi Kuu ya Englanda kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. (Football Insider)

Pia unaweza kusoma:

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi