Shamima Begum: Jasusi wa Canada alimuiba msichana wa shule na kumpeleka Syria

Shamima Begum, ambaye alitoroka Uingereza na kujiunga na kikundi cha Islamic State, alitoroshwa na kuingizwa ndani ya Syria na wakala wa ujasusi wa Canada

 Faili zilizoshuhudiwa na BBC zinaonyesha jasusi huyo alidai kushirikisha maelezo ya paspoti ya Bi Begum kwa Canada,na kuwatorosha Waingereza wengine kwa ajili ya kupigana kwa ajili ya IS.

 Mawakili wa Begum wanapinga kumuondolea uraia wa Uingereza, wakidai kuwa alikuwa muathiriwa wa usafirishaji haramu wa binadamu.

 Canada na Uingereza zilikataa kuzungumzia kuhusu masuala ya usalama.

Bi Begum alikuwa na umri wa miaka 15 wakati yeye na wanafunzi wengine wawili wa shule iliyopo mashariki mwa London - Kadiza Sultana, 16, na Amira Abase mwenye umri wa miaka 15 -waliposafiri hadi Syria kujiunga na kikundi cha ugaidi cha IS katka mwaka 2015.

 Katika kituo kikuu cha basi cha Instanbul, wasichana hao walikutana na Mohammed Al Rasheed, ambaye alipanga safari yao ya kuelekea katika eneo la Syria lililodhibitiwa na IS.

Afisa wa ngazi ya juu wa ujasusi, katika shirika ambalo ni sehemu ya muungano wa dunia wa ugaidi dhidi ya IS, aliithibitishia BBC kuwa Rasheed alikuwa akitoa taarifa kwa shirika la ujasusi la Canada wakati akiwatorosha wat una kuwapeleka katika IS.

 BBC imepata waraka kuhusu Rasheed ambao una taarifa zilizokusanywa na maafisa wa usalama na ujasusi, pamoja na taarifa nyingine zilizokusanywa katika kompyuta yake iliyogunduka , ambavyo vinaoa taarifa zisizo za kawaida kuhusu jinsi alivyofanya harakati zake.

 Aliwaambia maafisa kwamba alikuwa amepata taarifa kuhusu watu aliowasaidia kuingia ndani ya Syria kwasbabu alikuwa akiiwasilisha kwa ubalozi wa Canada nchini Jordan.

Rasheed, ambaye alikamatwa nchini Uturuki katika siku za kumtorosha Bi Begum na kumpeleka kwa IS, aliwambia maafisa kwamba alikuwa ameshirikisha picha ya paspoti ya msichana wa shule Muingereza aliyokuwa anatumia.

Polisi wa Uingereza walikuwa wanamsaka msichana huyo, ingawa wakati Canada ilipopokea maelezo ya paspoti yake , Bi Begum alikuwa amekwishafika tayari nchini Syria.

 Waraka unaonyesha kuwa Bi Begum alihamishiwa Syria kupitia mtandao wa watu wa IS wanaofahamika ambao ulikuwa ukidhibitiwa kutoka mji mkuu wa kikundi hicho wa Raqqa.

 Rasheed alikuwa mkuu wa mtandao huo upande wa Uturuki na alisaidia kusafirishwa kwa wanaume Uingereza, wanawake na watoto kwenda IS kwa walau miezi minane kabla ya kumsaidia Bi Begum na rafiki zake wawili.

 Bi Begum alikiambia kipindi cha BBC BBC forthcoming I'm Not A Monster podcast: "Alipanga safari yote kuanzia Uturuki hadi Syria… Sidhani kama mtu yeyote angeweza kufika Syria bila msaada wa walanguzi wa binadamu.

 "Aliwasaidia watu wengi kuingia ndani…tulikuwa tunafanya tu kila kitu alichokuwa akituambia tufanye kwasababu alijua kila kitu , hatukujua chochote ."

 Rasheed alitunza taarifa kuhusu watu aliowasaidia, akipiga nyaraka zai za vitambulisho- ID mara kwa mara au kuchukua video zao kisiri kwa kutumia simu yake.

 Moja ya rekodi za kipindi inaonyesha Bi Begum na rafiki zake wakitoka ndani ya teksi na wakiwa ndani ya gari wakisubiri katika eneo ambalo sio mbali na mpaka wa Syria.

 Rasheed pia alikudanya taarifa kuhusu IS, akichora ramani za maeneo ya nyumba za wapiganaji wa Magharibi wa IS nchini Syria, akitambua makazi ya IP na maeneo yenye Intaneti katike eneo linalodhibitiwa na IS, na kuchukua picha za mazungumzo aliyokuwa nayo na wapiganaji wa IS.

 Katika mojawapo ya mazungumzo, Rasheed alizungumza na mwanaume anayeaminiwa kuwa ni mpiganaji sugu wa IS Muingereza na mtu aliyewaingiza katika IS, Raphael Hostey, ambaye anamwambia: "Ninakutaka ufanye kazi chini yangu. Rasmi… Ninataka wewe usaidie kuleta watu ndani ya IS."

Katika ujumbe uliofuatia, Rasheed anamuuliza Hostey: "Unaweza kufafanua kidogo, tafadhali ?"

Rasheed alisema kwamba katika mwaka 2013 alikuwa amekwenda katika ubalozi wa Canada -Jordan kujaribu kuomba ukimbizi. Alisema : "Waliniambia kuwa watanipatia uraia wa Canada iwapo ningewapatia taarifa kuhusu shughuli za ISIS."

 BBC imeweza kuthibitisha kwamba Rasheed aliingia na kutoka Jordan mara nyingi kati ya mwaka 2013 na mwaka alipo kamatwa wa 2015.

 Tasnime Akunjee, ambaye ni wakili wa familia ya Begum, alisema kuwa kutakuwa na kesi mwezi Novemba ya kupinga kuondolewa kwa uraia wa Uingereza wa Bigum "moja ya hoja kuu" itakuwa ile ya aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani wakati huo Sajid Javid ambayo haikuzingatia kwamba alikuwa muathiriwa biashara haramu ya binadamu.

 "Uingereza ina wajibu wa kimataifa wa jinsi tunavyoangaliwa usafirishaji wa watu na jinsi tunavyowapaswa kuchukuliwa kwa vitendo vyao," alisema.

 Bw Akunjee alisema "inashitua" kwamba mtu aliyetumiwa na ujasusi wa Canada alikuwa sehemu muhimu ya operesheni ya usafirishaji haramu - "mtu ambaye alifaa kuwa mshirika, ambaye angefaa kuwalinda watu wetu, badala ya kuwasafirisha watoto wa Ungereza katika eneo la vita ".

 "Ujasusi uliokusanywa unaonekana kupewa kipaumbele zaidi ya maisha ya watoto," alisema.

 Shamima Begum kwa sasa anashikiliwa katika kambi ya mahabusu kaskazini- mashariki mwa Syria, uraia wake uliondolewa mwaka 2019 baada ya kuibuka kutoka katika kile kinachoitwa Khalifa ya IS.

 Msemaji wa Huduma za ujasusi za Canada alisema kuwa hawezi "kuzungumza wazi sula hilo au kuthibitisha au kukanusha mambo yaliyozungumziwa katika uchunguzi wa CSIS ,maslahi ya kikazi, mbinu ziizotumiwa au harakati ".

 Msemaji wa serikali ya uingereza alisema kuwa : "Ni sera yetu ya muda mrefu kwamba hatuzungumzii kuhusu operesheni za ujasusi au masuala ya kiusalama."

Hostey anasema: "Kitu sawa na unachofanya sasa, lakini utufanyie kazi ukileta vifaa, kuwaleta makaka na madada ". Mohammed Al Rasheed anajibu: "Niko tayari kaka ." Rasheed alikamatwa katika mji wa Uturuki wa Sanliurfasio mda mrefu baada ya kusaidia katika safari ya msichana Begum na wenzake.

Katika taarifa yake kwa maafisa wa usalama, alisema kuwa sababu alikuwa ankusanya taarifa kumuhusu kila mtu aliyemsaidia, akiwemo Shamima, ilikuw ani kwasbabu "Nilikuwa nawasilisha taarifa hii kwa ubalozi wa Canada katika Jordan".

Rasheed alisema kwamba katika mwaka 2013 alikuwa amekwenda katika ubalozi wa Canada -Jordan kujaribu kuomba ukimbizi. Alisema : "Waliniambia kuwa watanipatia uraia wa Canada iwapo ningewapatia taarifa kuhusu shughuli za ISIS."

BBC imeweza kuthibitisha kwamba Rasheed aliingia na kutoka Jordan mara nyingi kati ya mwaka 2013 na mwaka alipo kamatwa wa 2015.

Tasnime Akunjee, ambaye ni wakili wa familia ya Begum, alisema kuwa kutakuwa na kesi mwezi Novemba ya kupinga kuondolewa kwa uraia wa Uingereza wa Bigum "moja ya hoja kuu" itakuwa ile ya aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani wakati huo Sajid Javid ambayo haikuzingatia kwamba alikuwa muathiriwa biashara haramu ya binadamu.

 "Uingereza ina wajibu wa kimataifa wa jinsi tunavyoangaliwa usafirishaji wa watu na jinsi tunavyowapaswa kuchukuliwa kwa vitendo vyao," alisema.

 Bw Akunjee alisema "inashitua" kwamba mtu aliyetumiwa na ujasusi wa Canada alikuwa sehemu muhimu ya operesheni ya usafirishaji haramu - "mtu ambaye alifaa kuwa mshirika, ambaye angefaa kuwalinda watu wetu, badala ya kuwasafirisha watoto wa Ungereza katika eneo la vita ".

 "Ujasusi uliokusanywa unaonekana kupewa kipaumbele zaidi ya maisha ya watoto," alisema.

 Shamima Begum kwa sasa anashikiliwa katika kambi ya mahabusu kaskazini- mashariki mwa Syria, uraia wake uliondolewa mwaka 2019 baada ya kuibuka kutoka katika kile kinachoitwa Khalifa ya IS.

 Msemaji wa Huduma za ujasusi za Canada alisema kuwa hawezi "kuzungumza wazi sula hilo au kuthibitisha au kukanusha mambo yaliyozungumziwa katika uchunguzi wa CSIS ,maslahi ya kikazi, mbinu ziizotumiwa au harakati ".

 Msemaji wa serikali ya Uingereza alisema kuwa : "Ni sera yetu ya muda mrefu kwamba hatuzungumzii kuhusu operesheni za ujasusi au masuala ya kiusalama."