Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Putin: Hatari ya nyuklia inaongezeka, lakini sisi sio wazimu
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema tishio la vita vya nyuklia lilikuwa linaongezeka, lakini akasisitiza kuwa Urusi "haina wazimu" na haitatumia silaha zake za nyuklia kwanza.
Maafisa wa nchi za Magharibi wanaamini kuwa awali Putin alipanga kupata ushindi wa haraka.
Uwezo wa Urusi wa kutumia silaha za nyuklia umezidi kuongezeka tangu ilipoivamia Ukraine mwezi Februari.
"Tishio kama hilo linaongezeka, itakuwa mbaya kuficha," Putin alionya wakati akizungumzia matarajio ya vita vya nyuklia kupitia kiunga cha video kutoka Moscow.
Lakini alidai kwamba Urusi haitatumia silaha kwanza "chini ya hali yoyote", na haitamtishia mtu yeyote na silaha zake za nyuklia.
Putin pia alijigamba kuwa Urusi ina silaha za nyuklia za kisasa na za hali ya juu zaidi ulimwenguni, na alitofautisha mkakati wake wa nyuklia na Marekani- ambayo alisema iliendelea zaidi kuliko Urusi kwa kuziweka silaha zake za nyuklia kwenye maeneo mengine.
"Hatuna silaha za nyuklia, zikiwemo za kimkakati, kwenye eneo la nchi nyingine, lakini Wamarekani wanazo - nchini Uturuki, na katika baadhi ya nchi nyingine za Ulaya," alisema.
Putin hapo awali alisisitiza kwamba mafundisho ya nyuklia ya Urusi yanaruhusu tu matumizi ya kujihami ya silaha za nyuklia.
Akionekana kutambua kwamba mpango wake wa kudai ushindi ndani ya siku chache baada ya kuivamia Ukraine haukufaulu, Putin alikiri kwamba vita vinaweza kuwa "mchakato mrefu".
Hata hivyo, alisema matokeo tayari yamekuwa "chanya" - kwa mfano, maeneo mapya ambayo Urusi imedai kinyume cha sheria baada ya kura za maoni za udanganyifu katika mikoa minne ya Ukraine.
Alijigamba kwamba unyakuzi huo umefanya Bahari ya Azov - ambayo inapakana na kusini-mashariki mwa Ukrainia na kusini-magharibi mwa Urusi - "bahari ya ndani" ya Urusi, akiongeza kuwa hayo yalikuwa matarajio ya Tsar Peter Mkuu wa Urusi.
Rais Putin amejilinganisha na mtawala wa Karne ya 17 na 18 hapo awali.
Lakini - licha ya kudai mikoa ya Kherson, Zaporizhzhia, Luhansk na Donetsk kama eneo jipya la Urusi - Moscow haidhibiti kikamilifu mojawapo ya maeneo hayo.
Mwezi uliopita, vikosi vya Urusi vililazimika kuondoka Kherson, mji mkuu pekee wa kikanda ambao walikuwa wameuteka tangu uvamizi wa Februari.
Vikwazo kwenye mstari wa mbele vimefanya Urusi kulenga vituo vya umeme vya Ukraine kwa kuanzisha mashambulizi makubwa ya angani kote nchini.
Mashambulio hayo ya anga yamesababisha uharibifu mkubwa kwa miundombinu ya nishati ya Ukraine, na kuwaacha mamilioni ya watu bila umeme kwa saa, au hata siku, huku halijoto ikishuka chini ya sufuri.
Meya wa Kyiv, Vitali Klitschko, alionya kwamba mji mkuu wa Ukraine - ambao umeathiriwa vibaya na kukatwa kwa umeme.
Ingawa makao yenye joto yamejengwa jijini, Bw Klitschko alikiri kuwa hayatoshi kwa wakazi wote, na watu wanapaswa kuwa tayari kuhama ikiwa hali itazidi kuwa mbaya.
Nchini Urusi, ukosoaji wowote dhidi ya uvamizi wa Putin ulipingwa mbele ya baraza la haki za binadamu.
Katika maandalizi ya mkutano huo wa Jumatano, wajumbe 10 wa baraza hilo ambao walikuwa wameonyesha mashaka kuhusu vita hivyo waliondolewa. Badala yake, wabadilishaji wanaounga mkono vita waliletwa.
Masuala yatakayojadiliwa wakati wa mkutano pia yalipimwa sana kabla, kulingana na chombo huru cha habari cha Urusi Verstka.
Katika wiki za hivi karibuni, mafundisho ya nyuklia ya Urusi yamekuwa yakichunguzwa kwa karibu ni lini silaha za nyuklia zinaweza kutumika, haswa silaha "ya kimbinu" ambayo inaweza kuachiliwa kwenye uwanja wa vita nchini Ukraine.
Silaha ya busara ya nyuklia ni ya kutumika katika mapigano, kinyume na silaha kubwa "za kimkakati" ambazo zimeundwa kusababisha uharibifu mkubwa.