Saratani: Utafiti wabaini kitu cha kushangaza kuhusu bakteria wanaoishi ndani ya uvimbe

Miili yetu ni makazi ya aina tofauti ya vijidudu.

Utumbo, mdomo, pua na ngozi ni nyumbani kwa jumuiya mbalimbali za vijidudu ambavyo vinaweza kuwa vyema au vibaya kwa afya zetu.

Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni wanasayansi wamepata mahali pa kushangaza zaidi wanapoishi: kwenye uvimbe.

Ni jambo la kawaida kufikiria uvimbe kama wingi wa seli za mgonjwa ambazo hazifanyi kazi vizuri na hukua bila kudhibitiwa. Kwa hakika, muungano wa aina tofauti za seli, ambazo zinaashiria kwa kiasi kikubwa ugumu wa kuzishambulia bila kuharibu tishu zenye afya.

Lakini uvimbw pia huhifadhi mkusanyiko wa seli kutoka kwa aina nyingine za viumbe hai: bakteria na fungi. Baadhi hustawi katika mazingira yanayozunguka uvimbe, huku wengine wakiishi ndani ya seli za saratani zenyewe.

Lakini, hadi hivi karibuni haikubainika wazi vijidudu huwa na jukumu gani ndani ya uvimbe.

Sasa wanasayansi wanaanza kubaini ikiwa vijidudu hivi vinahusika katika ukuzaji wa seli za saratani au ni vijidudu tu vilivyonaswa kwenye uvimbe.

Majibu yanaweza kutoa mbinu mpya za kutibu na kuzuia saratani.

Bakteria zinazolinda uvimbe

Katika utafiti wa 2017, Ravid Straussman, mwanabiolojia wa saratani katika Taasisi ya Sayansi ya Weizmann huko Rehovot, Israel, na timu yake walionyesha kuwa baadhi ya bakteria wanaoishi ndani ya saratani ya kongosho wanaweza kulinda uvimbe kwa kuzima dawa ya kawaida ya chemotherapy.

Waligundua kwamba aina fulani ya bakteria, inayojulikana kama Gammaproteobacteria, inaweza kuvunja gemcitabine, dawa inayotumiwa kutibu aina mbalimbali za saratani, ikiwa ni pamoja na zile zinazopatikana kwenye kibofu cha mkojo, matiti na kongosho. Hii husaidia uvimbe kuwa sugu kwa dawa.

Wakati watafiti waliingiza bakteria kwenye panya wenye saratani ya utumbo, uvimbe pia ukawa sugu kwa dawa hiyo. Lakini watafiti walipowapa panya dawa ya antibiotiki pamoja na dawa ya chemotherapy, uusugu huo ulitoweka.

Utafiti huo unatoa kidokezo cha kuvutia kwa kile kinachoendelea ndani ya uvimbe.

Straussman na timu yake sasa wanatarajia kuendeleza utafiti huo kwa kufanya majaribio ya kimatibabu yanayohusisha wagonjwa wa saratani ya kongosho ambao matibabu yao ya kwanza hayakufaulu.

Watawapa wagonjwa kiuavijasumu kinachofanya kazi dhidi ya Gammaproteobacteria, pamoja na gemcitabine, ili kuona kama dawa hiyo inaboresha matokeo yao.

Bakteria zinazofanya saratani kuwa mbaya zaidi

Bakteria pia inweza kuchukua nafasi nyingine katika saratani badala ya kulinda uvimbe dhidi ya dawa ya matibabu .

Mnamo 2020, kundi la Straussman lilichambua zaidi ya vivimbe 1,500 za binadamu katika aina saba tofauti za saratani: matiti, mapafu, ovari, kongosho, melanoma, mfupa na ubongo.

Waligundua kwamba aina zote za uvimbe zilivamiwa na bakteria, ambao waliishi ndani ya seli za saratani na baadhi ya seli za kinga.

Aina tofauti za uvimbe zilikuwa na jamii tofauti za bakteria.

"Kila bakteria hizi imezoea mazingira ya kipekee ambayo inaishi ndani," anasema Straussman.

"Katika saratani ya mapafu, tulionyesha jinsi watu wanaovuta sigara wana bakteria nyingi ambazo zinaweza kuvunja nikotini, ambayo ni metabolite inayohusiana na moshi.

Katika uvimbe wa mifupa, tunaona bakteria ambao hubadilisha hydroxyproline, ambayo ni metabolite iliyoboreshwa katika uvimbe wa mfupa."

Hata hivyo bado haijabainika ikiwa bakteria humsaidia mgonjwa kudhibiti seli za saratani.

Bakteria zinazopatikana katika aina fulani za saratani ya matiti, kwa mfano, zinaweza kuondoa sumu ya arsenate, aina ya uvimbe inayojulikana kuongeza hatari ya saratani ya matiti.

Kuna ushahidi wamba, katika hali zingine, bakteria wanaoishi kwenye uvimbe wanaweza kufanya saratani kuwa mbaya zaidi.

"Kuna tafiti zaidi zinazoonyesha jinsi bakteria zinaweza kuwa sehemu ya saratani," anasema Straussman.

Bakteria pia wanaweza kubadilisha uwezo wa mfumo wa kinga kushambulia na kuharibu seli za saratani, anaongeza. "Kwa kweli tunafanya uchunguzi zaidi."

Straussman anasema mengi zaidi yanahitajika kufanywa ili kufahamu athari za bakteria ndani ya uvimbe wakati wa ugonjwa.

Baadhi ya vidokezo

Utafiti wa 2020 uliofanywa na wanasayansi nchini China unaonyesha kuwa baadhi ya bakteria kwenye uvimbe wa matiti wanaweza kurahisisha seli za saratani kuenea katika sehemu nyingine za mwili.

Watafiti waligundua bakteria wanaoishi ndani ya seli za uvimbe wa matiti zinazozunguka kwenye damu ya panya. Seli hizi hutengana na uvimbe wa msingi na zinaweza kusafiri hadi sehemu nyingine za mwilina kukua.

Hata hivyo, chembe chembe za uvimbe zinapozunguka kwenye mkondo wa damu zinakabiliwa na halingumu ambayo hufanya baadhi hupasuka.

Wakati wanasayansi walipoondoa bakteria hizi kutoka kwa uvimbe kwenye mwili wa panya, vidonda vilionekana kupoteza uwezo wa kukua, ingawa saratani ya matiti ya msingi iliendelea kukua.

"Kuna ushahidi kwamba vijidudu maalum kwenye utumbo, ngozi na viungo vingine vya utando wa mucous vinaweza kukuza ukuaji na kuendelea kwa uvimbi au kwa njia nyingine kuupinga," anasema Douglas Hanahan, M.D. kutoka Taasisi ya Uswizi ya Utafiti wa Saratani ya Majaribio nchini. Lausanne, Uswisi.

"Picha ni ngumu sana. Ingawa kuna dalili, hakuna ufafanuzi wa uhakika juu ya nani anafanya nini."

bakteria wanaohama

Tafiti zingine zilichunguza bakteria ya mdomo inayoitwa Fusobacterium nucleatum, ambayo inahusishwa na ugonjwa wa fizi lakini pia inaweza kuhusishwa na aina mbalimbali za saratani.

Kuna uwezekano wa bakteria hizi kuhama kutoka kinywa na kugeuka seli za saratani ya colorectal kupitia mkondo wa damu.

Kila bakteria hubeba chembe maalum ambazo zinaweza kugeuka na kuwa seli za saratani na kujikuza ndani ya uvimbe.

Baada ya kuanzishwa, bakteria wanaweza kuongeza kasi ya ukuaji na kuenea kwa uvimbe kwa kudhoofisha uwezo wa mfumo wa kinga kuua seli za saratani.

Bakteria pia hutumia silaha ya molekuli ambayo hufanya seli za saratani kuwa sugu zaidi kwa tibu ya chemotherapy.