Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
China yamuonya Spika wa Marekani juu ya kuizuru Taiwan
Uvumi kuhusu mpango wa Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi kufanya ziara Taiwan umeikasirisha China na kuiacha Ikulu ya White House na maumivu makali ya kijiografia.
Hili ni tatizo kubwa kiasi gani?
China imeonya juu ya "madhara makubwa" ikiwa Pelosi ataendelea na ziara yake.
Ni wa pili kwa wadhifa wa urais, baada ya makamu wa rais, Bi Pelosi anakuwa mwanasiasa wa cheo cha juu zaidi wa Marekani kusafiri hadi kisiwani humo tangu 1997.
Hii inaipa nafasi China, ambayo inaiona Taiwan inayojitawala kama jimbo lililojitenga ambalo lazima liwe sehemu ya nchi. China haijatoa uamuzi kuhusu uwezekano wa matumizi ya nguvu kufanikisha hili.
Hata utawala wa Biden umeripotiwa kujaribu kumzuia Pelosi asiende.
Wiki iliyopita, Rais Joe Biden aliwaambia waandishi wa habari "jeshi linadhani si wazo zuri", lakini Ikulu yake ya White House imetaja matamshi ya China dhidi ya safari yoyote kama hiyo "kwa wazi kuwa haina msaada na sio lazima".
Idara ya serikali inasema Pelosi hajatangaza safari yoyote na mtazamo wa Marekani kwa Taiwan haujabadilika.
Wakati Marekani inadumisha kile inachoita "uhusiano thabiti na usio rasmi" na Taiwan, ina uhusiano rasmi wa kidiplomasia na China na sio Taiwan.
Safari ya Pelosi, kama itatokea, pia inakuja huku kukiwa na ongezeko la mvutano kati ya Washington na China na kabla ya mazungumzo ya kati ya Rais wa Marekani Joe Biden na kiongozi wa China Xi Jinping.
Kwa nini Pelosi anataka kutembelea Taiwan?
Kuna uungwaji mkono mkubwa wa pande mbili kwa Taiwan miongoni mwa umma wa Marekani na katika Bunge la Marekani.
Na katika uzoefu wa kazi za bunge kwa miaka 35, Spika Pelosi amekuwa mkosoaji mkubwa wa China.
Ameshutumu rekodi ya haki za binadamu, alikutana na wapinzani wanaounga mkono demokrasia, na pia alitembelea Tiananmen Square kuwakumbuka waathirika wa mauaji ya 1989.
Mpango wa awal iwa Pelosi ulikuwa kutembelea Taiwan mwezi Aprili, lakini uliahirishwa baada ya kupimwa na kukutwa na Covid-19.
Amekataa kuzungumzia maelezo ya safari hiyo, lakini alisema wiki iliyopita kwamba ilikuwa "muhimu kwetu kuunga mkono Taiwan".
Kwa nini China inapinga ziara hiyo?
Beijing inaiona Taiwan kama eneo lake na mara kwa mara imeibua wasiwasi wa kuichukua kwa nguvu ikiwa itawalazimu
Maafisa wa China wameelezea hasira zao kwa kile wanachokiona kama kuongezeka kwa ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Taiwan na Marekani. Hii ni pamoja na ziara ya ghafla katika kisiwa hicho iliyofanywa na wabunge sita wa Marekani mwezi Aprili.
Siku ya Jumatatu, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian alionya kuwa nchi yake itachukua "hatua madhubuti" ikiwa Pelosi ataendelea na ziara yake.
"Na Marekani itawajibika kwa madhara yote makubwa," alisema.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya China anaonekana kupendekeza kuwa kunaweza kuwa na mwitikio wa kijeshi.
"Ikiwa upande wa Marekani utasisitiza kuendelea, jeshi la China halitakaa bila kufanya kazi na litachukua hatua kali kuzuia uingiliaji wowote wa nje na majaribio ya kujitenga kwa 'uhuru wa Taiwan'," Kanali Tan Kefei aliiambia China Daily.
Ishara mchanganyiko
Ikiwa ni kisiwa kidogo chenye washirika wachache, hautambuliki na Umoja wa Mataifa na unatishiwa kuvamiwa na jirani mkubwa mwenye nguvu Zaidi kisha ukatembelewa na mwanasiasa wa tatu mwenye nguvu zaidi nchini Marekani kunapaswa kuwa kitu ambacho unakikaribisha.
Ndio maana serikali ya Taiwan haitamwambia Spika wa Bunge la Merika Nancy Pelosi akae mbali.
Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen kwa muda mrefu ametoa wito wa ushirikiano wa ngazi ya juu na Marekani. Lakini pia kuna wasiwasi kuhusu kwanini Pelosi anakuja sasa na ikiwa safari yake inaweza kuleta madhara zaidi kuliko mema.
Mara tatu kwa mwaka jana Rais Joe Biden alisema Marekani itaingilia kati kuiunga mkono Taiwan katika tukio la uvamizi wa China ili tu kurudisha nyuma matamshi ya wafanyakazi akisisitiza hakuna mabadiliko katika sera ya Marekani.
Wakati taarifa za safari ya Pelosi nchini Taiwan zilipovuja, jibu la Rais Biden halikuwa kuunga mkono lakini badala yake alisema, "idara ya ulinzi inadhani si wazo zuri".
Huko China hii inaonekana kama udhaifu. Huko Taiwan inaonekana kama kuchanganyikiwa. Je, ni nini hasa sera ya serikali ya Marekani katika kisiwa hicho?
Pelosi sasa ana umri wa miaka 82 na anatarajiwa kustaafu msimu wa vuli. Je, anakuja hapa kwa nia ya wazi ya kutoa uungwaji mkono wa kweli au ni umaarufu wa kisiasa? Yote hayako wazi sana.
Je, ziara inaweza kuongeza mivutano?
Katika kongamano la chama chake baadaye mwaka huu, Chama cha Kikomunisti cha China kinatazamiwa kumchagua tena Xi kwa muhula wa tatu ambao haujawahi kushuhudiwa katika Urais.
Rais Biden ambaye alizungumza na Rais Xi mara ya mwisho mwezi Machi amesema watazungumza kwa njia ya simu tena katika siku chache zijazo, kuhusu mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na Taiwan na "masuala mengine ya mvutano".
Wito huo unakuja huku maafisa wa Marekani wakionya kuhusu kuongezeka kwa jeshi la China katika eneo la Asia-Pasifiki na "tabia ya uchokozi na kutowajibika" katika Bahari ya China Kusini.
Vitisho vya kulipiza kisasi kwa ziara ya Pelosi vimeibua wasiwasi juu ya mwitikio wa China.
Wakati Katibu wa Afya wa Marekani wakati huo Alex Azar alipoelekea Taiwan mwaka 2020, ndege za jeshi la anga za China zilivuka mstari wa kati wa Mlango-Bahari wa Taiwan - njia nyembamba ya maji kati ya kisiwa hicho na jirani yake mkubwa ndani ya safu ya makombora ya Taiwan.
Wiki iliyopita, mhariri wa zamani wa gazeti la serikali ya China la Global Times alipendekeza "jibu la kushtua la kijeshi" likae tayari kwa ajili ya Pelosi.
"Ikiwa Pelosi atazuru Taiwan, ndege ya kijeshi ya [People's Liberation Army] itaaongozana na ndege ya Pelosi kuingia kisiwani na kuweka kihistoria ya kisiwa hicho kwa ndege za kijeshi kutoka bara kuvuka kwa mara ya kwanza," Hu Xijin aliandika.
Hadi sasa, sera ya Marekani ya "utata wa kimkakati" ina maana kwamba Marekani makusudi haijulikani kama ingeilinda au jinsi gani itailinda Taiwan katika tukio la shambulio kubwa katika kisiwa hicho.