Kwanini mwanamke huyu karibu ajifungue juu ya treni

tt

Chanzo cha picha, KWA HISANI YA ALAN LÓPEZ, MRATIBU WA CASA MIGRANTE DE AGUASCALIENTES.

Maelezo ya picha, Johanndri Pacheco alipata uchungu juu ya paa la treni inayoelekea kaskazini kuelekea Mexico

Johanndri Pacheco alipanda treni akiwa na uchungu wa kujifungua.

Japo alikuwa na ujauzito miezi minane na nusu, hakupitia mlango wa gari la moshi ili kuketi kwenye kiti na kutazama mandhari kati ya Irapuato na Matamoros, katikati mwa mashariki ya mbali ya Mexico, kwenye mpaka na Marekani.

Alipanda ngazi kando ya gari la moshi ili kufikia paa la treni ya mizigo ya mfumo wa reli ya Mexico, mtandao wa zamani wa treni unaojulikana kama La Bestia (Mnyama).

Mhamiaji huyo wa Venezuela mwenye umri wa miaka 23 alikuwa amechoka. Pamoja na mwenzi wake José Gregorio na mwana wao Gael mwenye umri wa miaka minne, walingoja treni lifike kwa siku tano kwenye daraja la Irapuato.

Wahamiaji wengine walisema treni hiyo ilijulikana kwa jina la El Bolichero, kwa sababu ya mipira midogo ya chuma iliyohifadhiwa juu ya paa, ambayo walilazimika kuifunika kwa kadibodi ili kupumzika wakati wa safari.

Johandri na rafiki yake walikusanya masanduku kwa ajili ya safari na kula chakula ambacho wanaharakati na watu waliojitolea walisambaza kwenye daraja.

Wenzi hao na mtoto walisafiri katika nchi kadhaa kwa mwezi mmoja na nusu ili kuhakikisha kwamba Mía, mtoto Johandri aliyekuwa amembeba tumboni mwake, alizaliwa Marekani.

“Rafiki yangu aliniarifu kwamba endapo nitajifungua Mexico, wangenirudisha kwenye mpaka wa Guatemala na kumsajili binti yangu kuwa wa Guatemala,” alisema kutoka katika makao ya wahamiaji huko Aguascalientes, katikati mwa Mexico.

"Hofu yangu ilikuwa kwenda hospitali na kurudishwa na huduma za uhamiaji.

Treni hiyo iliwasili Irapuato usiku wa manane mnamo Ijumaa Agosti 25. Alikuwa amesalia na siku 12 kujifungua, kulingana na makadirio ya daktari ambaye alikuwa amemfanyia uchunguzi wake wa mwisho wa ujauzito.

Wahamiaji hupanda juu ya paa za treni za La Bestia ili kufika Marekani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wahamiaji hupanda juu ya paa za treni za La Bestia ili kufika Marekani.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Johandri alikulia Las Adjuntas, mji wa mabanda kusini-magharibi mwa Caracas.

Alihamia Peru muda mfupi kabla ya janga la Corona, akiwa na umri wa miaka 18, kabla ya kumaliza shule ya upili au kupata uzoefu wa kazi. "Nilitaka kujionea dunia mwenyewe, kujikimu mwenyewe kimaisha."

Mgogoro wa kiuchumi, ukosefu wa huduma za umma na ghasia nchini Venezuela zimesababisha zaidi ya watu milioni saba kuhama makwao tangu mwaka 2015, kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).

Johanndri alipta kazi yake ya kwanza huko Peru kama muuzaji katika duka la viatu. "Rudi katika nchi yako, nyinyi Wavenezuela mnakuja hapa kufanya fujo," baadhi ya wateja walimwambia, anasema. Alijifanya hasikii na kusalia kimya.

"Maoni haya hayaniathiri," alisema, akikumbuka matusi aliyopokea katika duka hilo. “Najipigania mimi na familia yangu.

Huko Peru, alijifungua mtoto wake wa kwanza, Gael.

Lakini, kufikia katikati ya mwaka 2021, mtazamo wake wa siku zijazo umebadilika. Gharama ya maisha ilipanda na mshahara wake hautoshi tena kulipia kodi na chakula.

Akiwa na chini ya dola 100 mfukoni mwake, Johandri alikata tamaa kurudi nyumbani kwa familia yake huko Las Adjuntas na kuhamia Chile, akipanda barabarani.

Alipata kazi kama msafishaji katika zahanati ndogo huko Santiago. Anauza nguo peke yake na hutoa vinywaji kwenye baa. Wakati tu alipofikiri alikuwa amepata utulivu wa kifedha, kodi ya nyumba yake mpya iliongezeka na aliogopa kwamba angelazimika kurudi Las Adjuntas.

“Niliamua kuondoka Chile nilipokuwa na ujauzito wa miezi saba,” anakumbuka.

"Nikiwa na ujauzito wangu nililazimika kushikilia miti na kuvuka mito ya Darien, ambayo ilikuwa moja ya sehemu ngumu zaidi za safari. Lakini sijui hali ingekuwa vipi laiti ningekuwa nimembeba mtoto mikononi mwangu.

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wahamiaji wanaovuka msitu hatari wa Darién huvuka mito huku wakitishiwa maisha na makundi yenye silaha.

Baada ya safari ya mwezi mmoja na nusu, kupanda El Bolichero huko Irapuato na kufika Matamoros hatua ya mwisho ilikuwa ya kuvuka mpaka kuingia Marekani.

Johandri na José Gregorio waliweka masanduku hayo juu ya paa la treni na kumweka Gael katikati yao ili alale.

Saa mbili asubuhi, Johanndri aliamka akiwa ameshika tumbo lake ili kupunguza maumivu.

Alikuwa bado ana siku 12 kabla ya kujifungua.

Johanndri alipopata mtoto wake wa kwanza, uvhungu wa uzazi iliambatana na maumivu ya mgongo. Wakati huu, tumbo pekee lilimuuma, kwa hivyo alidhani kuwa maumivu hayo yalitokana na uchovu na ugumu wa safari ya treni.

Hata hivyo, maumivu yaliongezeka kwa kasi, kuwa chungu wa mara kwa mara. Johanndri alimwambia mwenzi wake apige simu ili apate msaada mara moja. Mtoto Mia alikuwa njiani.

Saa 5 asubuhi, José Gregorio alichukua moja ya masanduku waliyokuwa wamelalia na kuandika: "Mtoto anazaliwa. Dereva wa treni anahitaji kujua. Ni ombi la dharura." Aliwataka wahamiaji wengine kupitisha ujumbe alioandika kwenye kadibodi kwenye mabehewa ya kwanza, kwa matumaini kwamba ingemfikia dereva.

tt

Chanzo cha picha, SOCIAL MEDIA

Maelezo ya picha, Mpenzi wa Johanndri alijaribu kumuomba dereva wa treni asitishe safari kuna mwanamke amepata uchungu wa uzazi.

Wengine walipokuwa wakiuliza ikiwa kuna yeyote angeweza kumsaidia mwanamke kujifungua, Johandri na José Gregorio walimwona mwanamume akikaribia paa la mabehewa ya kwanza ya treni.

Alikuwa ni mwokozi wa Venezuela ambaye pia alikuwa akijaribu kufika Marekani. Mwanamume huyo alichukua simu yake ya mkononi na kumpigia mke wake, nesi ambaye angemwambia jinsi ya kumsaidia Johanndri wakati wa kujifungua.

“Jiandae mpenzi, kunywa pombe, hivi ndivyo utakavyofanya...” Johandri alikumbuka huku akimsikiliza nesi kwenye kipaza sauti.

Mhudumu wa afya alikadiria kuwa uchungu ulikuwa ikitokea kila baada ya dakika tatu. Kisha kila dakika mbili. Johanndri alianza kutapika na kulia bila kujizuia. Hakutaka Mia azaliwe juu ya paa lile chafu, kwenye zile tufe za chuma ambazo zilikuwa zikipigwa na jua hadi kulazimu wasafiri kufunika kwa kadibodi ili kupumzika.

Wanapata pombe, mkasi na blanketi ili mwili wa mtoto usiguse kadibodi. Johanndri aliachana na wazo la binti yake kuzaliwa huko Mexico, juu ya paa la treni.

Mhudumu wa afya alimwambia José Gregorio amshikilie mgongo Johanndri na kusukuma kwa upole juu ya tumbo lake la juu ili kusaidia mtoto kushuka.

Saa 7 asubuhi, wakili Paola Nadine Cortés, mwanaharakati wa chama cha Agenda Migrante, alipokea picha ya ishara ambayo José Gregorio alikuwa ameandika akiomba usaidizi.

Mwanasheria huyo alitoa wito wa ulinzi wa raia kwenda kwenye maeneo ya ujenzi ya kampuni ya Ferromex, katika manispaa ya San Francisco de Los Romo, kilomita 222 kaskazini mwa kituo cha Irapuato.

"Wazo lilikuwa kuanzisha huduma ya dharura na kumwokoa kwa sababu walikuwa wakinitumia video na alionekana katika hali ya kusikitisha," anaeleza mwanaharakati huyo.

Kampuni ya treni hiyo ilimjulisha Bw. Cortés na dereva wa gari-moshi ambalo Johandri alipaswa kusafiria.

"Nilimtumia picha ili aweze kuona nambari ya treni. Kisha kondakta akaniambia: 'Hayuko kwenye treni hii. Ni ile iliyo nyuma zaidi.'

Dereva aliwasiliana na mwenzake na wakakubali kusimamisha treni kwa dakika kumi katika mji wa Aguascalientes.

"Kondakta aliniambia ni dakika kumi tu. Ikiwa hawakuweza kumtoa nje kwa wakati huo, treni ingeendelea na safari," Bw. Cortés alisema.

Treni ilisimama katika eneo la Los Arellanos, baadhi ya kilomita 108 kutoka mji wa Aguascalientes.

"Kwa sababu ya umbali na huduma kuu, timu ya dharura haikuweza kufika ndani ya dakika kumi walizotupatia."

Nusu saa baadaye, Johanndri alipohisi kwamba hawezi tena kuvumilia maumivu, treni ililisimama.