Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 16.09.2024

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Leroy Sane
Muda wa kusoma: Dakika 3

Newcastle wanamfuatilia winga wa Bayern Munich Mjerumani Leroy Sane, 28, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Football Insider)

Bayern Munich pia wanazidisha mazungumzo na Jamal Musiala, 21, kuhusu kuongeza mkataba, huku mkataba wa sasa wa kiungo huyo wa kati wa Ujerumani ukikamilika 2026. (Sport1 – In Detsch).

AC Milan, Inter Milan na Napoli wote wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Torino mwenye umri wa miaka 23 Samuele Ricci. (Calciomercato – In Italy)

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Max Eberl ametetea kuuzwa kwa mlinzi wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 25, kwa Manchester United, akisema mabeki wa kati wa sasa wa klabu hiyo wana uwezo zaidi wa kuweka ulinzi juu zaidi ya uwanja. (Mirror),

Pia unaweza kusoma
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Matthijs de Light

Mfanyabiashara wa Marekani John Textor anamtaka nyota wa muziki Jay-Z kushirikiana naye katika kuinunua Everton. (Sun}

Kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich, 29, yuko tayari kusaini mkataba mpya na Bayern Munich. (Sky Sports Germany)

Kimmich, hata hivyo, ananyatiwa na Barcelona anapokaribia mwisho wa mkataba wake wa sasa na klabu hiyo ya Bundesliga. (Mundo Deportivo – In Spanish)

Liverpool haiwezi kumnunua beki wa kati wa Sevilla Loic Bade, 24, licha ya kuhusishwa na Mfaransa huyo. (Matteo Moretto, via Yahoo).

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ansu Fati

Mshambuliaji wa kimataifa wa Jamaica Michail Antonio, 34, na mshambuliaji wa Uingereza Danny Ings, 32, wote wanaweza kuondoka West Ham kabla ya kukamilika kwa mikataba yao msimu ujao. (Football Insider)

Barcelona wanasema wanataka kumbakisha fowadi wa Uhispania Ansu Fati licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kutoichezea klabu hiyo mchezo wowote wa ligi tangu Agosti 2023, kabla ya kutolewa kwa mkopo kwa Brighton msimu uliopita . (Fabrizio Romano)

Manchester United walizuiliwa katika mbinu zao za kumsajili beki wa Senegal Mikayil Faye, 20 kabla ya kujiunga na Rennes kutoka Barcelona. (Inkubator podcast, via Teamtalk)

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla