Huku mtoto wa bilioni 8 akizaliwa, nani alikuwa wa 5, wa 6 na wa 7

Umoja wa Mataifa unasema idadi ya watu duniani imefikia watu bilioni nane, miaka 11 tu baada ya kupita idadi ya watu bilioni saba.
Baada ya ongezeko kubwa la watu katikati mwa karne ya 20, ukuaji wa ongezeko la watu tayari umeanza kupungua.
Inaweza kuchukua miaka 15 kufikia watu bilioni tisa na Umoja wa Mataifa hautegemei kufikiwa kwa idadi ya watu bilioni 10 hadi mwaka 2080.
Ni vigumu kufanya mahesabu ya idadi ya watu duniani kwa usahihi, na Umoja wa Mtaifa unakiri kwamba makadirio yake yanaweza kuwa nyuma kwa mwaka mmoja au miwili.
Lakini tarehe 15 Novemba ni makadirio yake bora zaidi ya kuvukwa kwa mstari wa idadi ya watu bilioni nane.

Katika miaka iliyopita, Umoja wa Mataifa ulichagua watoto wachanga kuwakilisha watano , sita na saba wanaotimiza idadi ya bilioni sana – kwahiyo hadithi zao zinaweza kutuambia nini kuhusu ukuaji wa idadi ya watu duniani?
Dakika chache baada ya kuzaliwa mwezi Julai 1987, Matej Gaspar alipigwa picha ya kamera ya mwangaza kwenye uso wake mdoogo na wanasiasa walimzunguka mama yake ambaye alikuwa mchovu.
Akiwa amekwama nyuma ya gari nje, afisa wa Umoja wa Mataifa Muingereza Alex Marshall alihisi kidogo kuwajibika na vurugu alizosababisha katika kitengo cha uzazi kidogo kilichopo katika viunga vya mji wa Zagreb.
"Kimsingi tuliangalia makadirio na kuota kuhusu wazo kwamaba idadi ya watu duniani itapita bilioni tano katika mwaka 1987," anasema. "Na tarehe ya takwimu ilikuwa ni tarehe 11 Julai." Waliamua kumbatiza mtoto mchanga wa dunia wa bilioni tano.
Wakati tulipokwenda katika demografia za Umoja wa Mataifa kutoa wazo walikasirika.
"Walitufafanulia sisi watu wajinga kwamba hatujui kile tunachokifanbya. Na kusema kweli tusingepaswa kumchagua mtu mmoja miongoni mwa watu wengi sana ."
Lakini walifanya tu. "Ilikuwa ni kuzipatia sura namba,"anasema. "Tulibaini alipokuwa akienda katibu mkuu siku ile na ilikwenda kutoka pale."


Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Miaka thelathini na mitano baadaye, mtoto wa dunia wa bilioni tano anajaribu kusahau jinsia alivyoingia kwa sherehe duniani. Ukurasa wake wa Facebook unaonyesha anaishi mjini Zagreb, yuko katika ndoa yenye furaha na anafanya kazi kama Mhandisi mkemia. Lakini anaepuka mahojiano na amekataa kuzungumza na BBC.
"Simlamu yeye," anasema Alex, huku akikumbuka jinsi alivyozingirwa na vyombo vya habari katika siku ya kwanza ya Matej.
Tangu wakati ule, watu bilioni tatu zaidi wameongezeka katika kdunia yetu. Lakini miaka 35 ijayo inaweza kushuhudia ongezeko la watu milioni mbili pekee – na idadi ya watu duniani inaweza kuongezeka kwa kiwango kidogo.
Nje kidogo tu ya Dhaka nchini Bangladesh, Sadia Sultana Oisheeanamsaidia mama yake , kumenya viazi kwa ajili ya chakula cha jioni. Ana umri wa miaka 11 na angependa kuwa nje akicheza soka lakini wazazi wake wanaendesha meli ndogo sana.
Familia yake imelazimika kuhamia hapa wakati biashara yao, ya kuuza vitambaa na sari, zilipoathiriwa na janga. Maisha ni rahisi kidogo kijijini , kwahiyo wanaweza kumudu bado kuwalipia ada watoto wao watatu wa kike.
Oishee ni mdogo zaidi na familia haina uchangamfu. Alizaliwa mwaka 2011, na aliitwa mojawapo ya majina ya watoto wachanga wa bilioni saba wa dunia.
Mama yake hakujua ni nini kitakachotokea. Hakuwa hata ametarajia kujifungua siku ile. Baada ya kumtembelea daktari alipeleka kwenye wodi ya kujifungulia kwa ajili ya upasuaji wa dharura -CS.
Oishee aliwasili dakika moja baada ya saa sita usiku , akiwa amezingirwa na waandishi wa habari wa TV na maafisa wa eneo wakisukumana kumtazama. Familia ilishituka lakini ilishukuru.

Wakati baba yake alikuwa na matumaini ya kumpata mtoto mvulana, kwa sasa ana furaha kuwa na watoto watatu , wachapa kazi, wenye akili wa kike. Kaka yake yuko chuo kikuu na Oishee ameazimia kuwa daktari. " hatuko vizuri hivyo na Covid imefanya mambo kuwa magumu zaidi ," anasema. "Lakini nitafanya kila liwezekanalo kuhakikisha ndoto zake zinatimia ."
Tangu Oishee alipozaliwa, watu wengine milioni 17 wameongezeka katika ukuaji wa idadi ya watu kwa Bangladesh.
Ukuaji huu umetokana na mafanikio makubwa ya sekta ya matibabu, lakini kiwango ambacho Bangladesh inapanuka kinaonyesha kuwa sio cha kawaida. Katika mwaka 1980 kulikuwa na wastani wa mwanamke kuwa na watoto zaidi ya sita, lakini sasa kiwango hicho kimeshuka hadi wastani wa chini ya watoto wawili. Na hilo limetokana na nchi hiyo kuangazia elimu. Kadri wanawake wanavyoelimika wanachagua kuwa na familia ndogo.
Hili ni muhimu kwa kuelewa ni wapi inakoweza kuelekea idadi ya watu duniani. Mambo makuu matatu ambayo yanawezesha makadirio ya idadi ya watu – Umoja wa Mataifa, taasisi ya IHME katika Chuo kikuu cha Washington na kituo cha IIASA-Wittgenstein cha Vienna – wana maoni mbali mbali juu ya faida wanazozitarajia katika elimu.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa idadi ya watu duniani itapanda na kuwa ya juu katika mwaka 2080, na kufikia watu bilioni 10.4 , lakini IHME na Wittgenstein wanaamini idadi hiyo itafikiwa karibuni zaidi – baina ya mwaka 2060 na 2070, kwa kiwango cha chini ya wau bilioni 10.
Lakini haya ni makadirio tu. Tangu alipozaliwa Oishee katika mwaka 2011 mambo mengi yamebadilika duniani, kiwango cha watu katika maeneo mbali mbali duniani kinashangaza kila mara.

Mtoto wa bilioni sita Adnan Mevic anaishi katika nchi ambayo idadi yake ya watu inaweza kupungua kwa nusu yake katika miaka 50 ijayo.
Wanaofanya mahesabu ya watu walipigwa na mshangao wakati idadi ya watoto wanaozaliwa kwa mwanamke mmoja nchini Korea Kusini iliposhuka kwa wastani wa 0.81, Samir KC anasema. "Kwa hiyo, idadi yake itakwenda chini sana kwa kiasi gani? Hili ni swali kwetu."
Ni kitu fulani zaidi nan chi zaidi zitahitaji kukabiliana nalo.
Huku nusu ya watu bilioni wajao watatoka katika nchi nane tu - nyingi kati yake zikiwa ni za Afrika -katika nchi nyingi kiwango cha uwezo wa kuzaa kitapungua kwa chini ya zaidi ya watoto 2.1 kwa mwanamke, idadi ambayo ni muhimu kuimarisha idadi.
Katika Bosnia-Herzegovina, moja ya maeneo ambapo idadi ya watu inapungua kwa haraka zaidi duniani, Adnan Mevic, mwenye umri wa miaka 23- anafikiri juu ya hili sana.















