'Kila kitu ni kigumu' - Amorim atafuta majibu Man Utd

Muda wa kusoma: Dakika 3

Je, maisha ndani ya Manchester United yanaweza kuwa ya kukatisha tamaa zaidi?

Wametoka tu kufungwa 3-0 nyumbani na klbau ndogo ya Bournemouth kama alivyoeleza mmiliki wa Cherries Bill Foley, kwa msimu wa pili unaoendelea, matokeo ambayo yanamaanisha kuwa watahudumia Krismasi wakiwa nafasi ya 13 kwenye jedwali. Ni mara ya kwanza kuwa katika nusu ya mwisho katika hatua hii tangu ufanisi wa klabu hiyo uanze .

Mashabiki wao - ambao waliizomea timu ya Ruben Amorim kwenye kipenga cha mwisho - wamekasirishwa sana na kupanda kwa bei ya tikiti hadi pauni 66 bila makubaliano hatua ambayo imewafanya kuungana na wafuasi wenzao wa Liverpool kuandamana wakati timu hizo mbili zitapokutana Anfield tarehe 5 Januari.

Wakati Amorim alipokuwa akiambia vyombo vya habari alihisi mashabiki "wamechoka" katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mechi, uvujaji kutoka kwenye dari ulisababisha maji kuwatiririka waandishi wa habari waliokuwa mstari wa mbele, na kumlazimu mmoja wao kusonga mbele.

Lakini kwa Amorim, msimao wa United katika jedwali si jambo la mzaha. Beki Lisandro Martinez aliiambia Mechi Bora ya Siku hali ya uwanjani inamfanya "akasirike". Bosi wake lazima atafute majibu.

"Kwa wakati huu, kila kitu ni kigumu sana," Amorim alisema. "Katika klabu kama Manchester United, kupoteza 3-0 nyumbani, ni ngumu sana kwa kila mtu.

"Kwa kweli mashabiki wamekatishwa tamaa na wamechoka. Unaweza kuhisi katika uwanja.

Ikiwa kuna tofauti kubwa iliyoletwa na Mreno huyo kwa muda mfupi tangu achukue nafasi ya Erik ten Hag mwezi uliopita, ni kwamba United wana udhibiti zaidi wa mpira katika mechi.

Takwimu zao za umiliki ziko juu 60% leo. United walikuwa na mashabulizi mengi na mashuti mengi yaliyolenga lango kuliko Bournemouth. Lakini walipoteza, vibaya

Kwa mara ya pili pekee katika historia yao - nyingine ikiwa dhidi ya Burnley katika miaka ya 1960 - wamepoteza mechi mfululizo za nyumbani dhidi ya wapinzani kwa tofauti ya mabao matatu.

Ingesaidia sana ikiwa hawangeendelea kuruhusu mabao kwenye 'set pieces'.

Ilitokea mara mbili , dhidi ya Arsenal mapema mwezi huu na dhidi ya Nottingham Forest katika mchezo wao wa mwisho wa nyumbani. Wakiwa Tottenham siku ya Alhamisi, Son Heung-min alifunga bao la moja kwa moja kutoka kwa kona.

Wote hawakuwa chini ya uangalizi wa Amorim, lakini United sasa wameruhusu mabao 17 kutoka kwa set piece kwenye Premier League mwaka huu, ikiwa idadi kubwa zaidi katika mwaka mmoja wa kalenda kwenye mashindano.

Makosa ya hivi majuzi yanazua swali, je, kocha Carlos Fernandes, ambaye aliandamana na Amorim kutoka Sporting, anafanya nini hasa?

Sio kwamba Amorim anagawanya lawama.

"Jukumu ni juu yangu, sio Carlos," alisema.

"Sisi ni timu katika wakati mzuri na wakati mbaya. Tuna njia ya kufanya mambo. Tunalifanyia kazi hilo na tunaenda kuboresha hilo. Lakini hatukupoteza kwa sababu ya kuweka vipande. Tumepoteza kwa sababu tumeunda. nafasi zaidi na hatukufunga."

Akizungumza na Mechi ya Siku, Martinez aliiweka kwa uwazi zaidi.

"Tuna hasira sana na hali ya aina hii," alisema beki huyo wa Argentina. "Lazima tufanye kazi zaidi katika 'set pieces' haswa.

"Ninaamini sana katika timu hii na wachezajii. Ikiwa hawatafunga bao lao la kwanza kutoka kwa seti piece basi ni mchezo tofauti kabisa."

Amorim inatatizwa na ukosefu wa ubora.

Mreno huyo alimwamini Tyrell Malacia katika nafasi ya beki wa kushoto, lakini alimtoa Mholanzi huyo wakati wa mapumziko baada ya kumtazama akiutoa mpira kwa rahisi mara nyingi na hakutoa chochote kwenda mbele.

Diogo Dalot alibadilisha safu yake, lakini tishio lake la bao moja lilikosa imani. Noussair Mazraoui alikwenda kwa beki wa kushoto kutoka nafasi yake katika safu ya ulinzi ya watu watatu, lakini alimchezea visivyo Justin Kluivert ambaye alimruhusu fowadi huyo kufunga bao la pili la Bournemouth kutoka kwa mkwaju wa penalti.

Mechi ikiendelea , nahodha Bruno Fernandes pekee ndiye aliyekuwa hatari kwa lango la Bournemouth, huku Marcus Rashford akiwekwa benchi kwa mechi ya tatu mfululizo, ingawa alikuwa Old Trafford kutazama matukio ya huzuni yanayoendelea.

"Inategemea, tutaona," alisema Amorim alipoulizwa kama fowadi huyo wa Uingereza anaweza kugombania nafasi yake siku ya Boxing Day dhidi ya Wolves.

Imetafsiriwa na kichapoishwa na Seif Abdalla