Huenda Binadamu wakapoteza nafasi zao za kazi kutokana na ukuaji wa akili Bandia

www

Chanzo cha picha, Getty Images

Tangu kuanza kwa mapinduzi ya viwanda, kumekuwa na vitisho kwamba mashine mpya kutoka kwa mitambo kubwa ya kufanya kazi kwenye kompyuta mpaka kwenye kifaa kidogo cha microchip inaweza kupelekea asilimia kubwa ya watu kupoteza ajira zao.

Kwa miaka mingi wanadamu wamekua wakiongoza kwenye sekta ya kazi lakini sasa wataalama wanasema kuna wasiwasi huenda nafasi hizo zikataliwa kabisa na roboti.

Ripoti ya iliotolewa mwezi Machi 2023 kutoka Goldman Sachs inakadiria kwamba akili bandia yenye uwezo wa kutengeneza maudhui inaweza kufanya robo ya kazi zote zinazofanywa na binadamu kwa sasa.

Kote katika Umoja wa Ulaya na Marekani, ripoti hiyo inabainisha kwamba zaidi, kazi milioni 300 zinaweza kupotea kutokana na mfumo wa kiotomatiki. Hali inayoweza kusababisha asilimia kubwa ya watu kukosa kazi kabisa duniani.Anasema Martin Ford, mwandishi wa kitabu cha Rule of the Robots.

www

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa bahati nzuri, sio habari zote ni mbaya. Wataalamu wanatoa tahadhari kwamba bado kuna mambo ambayo akili bandia haiwezi kufanya kabisa na hiyo ni Pamoja na majukumu ambayo yanahusisha sifa dhahiri za kibinadamu, kama vili hisia ,kufikiri na kuja na wazo lingine tofauti anapokua kazini. Na kuhamia katika majukumu ambayo yanazingatia ujuzi huo kunaweza kupunguza nafasi ya kazi za binadamu kuchuliwa na Roboti.

"Nadhani kwa ujumla kuna aina tatu ya kazi ambazo haziwezi kufanywa na roboti ama akili bandia maboksi katika siku zijazo," ameongeza Ford.

"Ya kwanza itakuwa ni kazi ambazo ni za ubunifu wa kweli:eneo hili haufanyi kazi ya kimfumo au kupanga tu vitu, lakini ni kazi inayohitaji maoni mapya na mwisho wake kuja na kitu kipya."

www

Chanzo cha picha, Getty Images

Hiyo haimaanishi kwamba kazi zote zinazochukuliwa kuwa ni zakiubunifu ziko salama. Ukweli ni kwamba mambo kama vile muundo wa picha na majukumu yanayohusiana na sanaa ni miongoni mwa kazi ambazo zinaweza kutawaliwa kabisa na roboti .kanuni za msingi zinaweza kuelekeza roboti kuchambua mamilioni ya picha, na kuruhusu akili bandia kustadi kujua namna ya kuzipachika picha hizo sehemu husika. Lakini kuna usalama fulani katika aina nyingine za ubunifu, anasema Ford: "katika sayansi, na utabibu na sheria ... watu ambao kazi yao inakuja na mkakati mpya wa kisheria au mkakati wa biashara. Nadhani hili ndilo eneo ambao wanadamu watalitawala kwa muda mrefu.

Sehemu ya pili ni kazi zinazohitaji uhusiano wa hali ya juu baina ya watu. Anaelekeza eneo hilo kuwa la wauguzi, washauri wa biashara na waandishi wa habari za uchunguzi. Hizi ni kazi, ambazo zinahitaji ufahamu wa kina wa watu. Nadhani itachukua muda mrefu kabla ya ubongo banadia kuwa na uwezo wa kujenga uhusiano mzuri na wanadamu wa kawaida.

Eneo la tatu salama, anasema Ford, "ni kazi ambazo zinahitaji sana kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, ustadi na uwezo wa kutatua matatizo katika mazingira yasiyotabirika". Kazi nyingi za biashara fikiria mafundi umeme, mabomba, wahunzi wote wapo katika Eneo hili ,"Hizi ni aina za kazi ambapo unashughulika na hali mpya kila wakati," anaongeza. "Labda ndio ngumu zaidi ya kitu chochote kufanya otomatiki. Ili kufanya kazi kama hii kiotomatiki, utahitaji roboti ya hadithi za kisayansi. Utahitaji C-3PO ya Star Wars.

www

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ingawa wanadamu watabaki katika kazi ambazo ziko ndani ya maeneo hayo matatu hiyo haimaanishi kuwa taaluma hizo zimetengwa kabisa .

Joanne Song McLaughlin, profesa mshiriki wa uchumi wa kazi katika Chuo Kikuu cha Buffalo,nchini Marekani, anasema kazi nyingi, bila kujali tasnia, zina vipengele ambavyo vina uwezekano wa kuendeshwa kiotomatiki na teknolojia.

"Katika hali nyingi, hakuna tishio la haraka kwa kazi,"lakini kazi zitabadilika." Ajira za kibinadamu zitazingatia zaidi ujuzi wa watu wengine, anaendelea Song McLaughlin. "Ni rahisi kufikiria kuwa, kwa mfano, akili bandia itagundua saratani bora kuliko wanadamu. Katika siku zijazo, nadhani madaktari watatumia teknolojia hiyo mpya. Lakini sidhani kama jukumu zima la daktari litabadilishwa."

Ingawa roboti inaweza kufanya kazi nzuri zaidi ya kutafuta saratani, anasema, watu wengi bado watataka kuonana ana kwa ana na daktari na kupewa majibu ya yale yanawasibu na sio Roboti. Hiyo ni kweli kwa karibu kazi zote, anaongeza, na kwa hivyo kukuza ustadi huo wa kibinadamu kunaweza kusaidia watu kujifunza kufanya kazi zao kando kazi itakayofanywa na akili bandia.

"Nadhani ni busara kufikiria kweli, 'ni aina gani ya kazi ndani ya kazi yangu itabadilishwa, au itafanywa vyema na kompyuta au akili bandia ? Na ustadi wangu wa ziada ni upi?’” Anaelekeza kwa wafanyabiashara wa benki, ambao wakati fulani walilazimika kuwa kaunta sahihi sana za pesa. Sasa, kazi hiyo imejiendesha kiotomatiki - lakini bado kuna mahali pa mtangazaji. "Kazi ya kuhesabu pesa ilipitwa na wakati kwa sababu ya mashine," anasema. "Lakini sasa, wasemaji wamelenga zaidi kuungana na wateja na kutambulisha bidhaa mpya. Ustadi wa kijamii umekuwa muhimu zaidi."

Ni muhimu kutambua, anasema Ford, kwamba elimu ya juu au nafasi ya kulipa sana sio ulinzi dhidi ya nafasi hizo kuchukuliwa na akili Bandia. "Tunaweza kufikiri kwamba mtu anaefanya kazi ofisini anamaisha ya juu zaidi na ana Maisha mazuri ikilinganishwa na Maisha ya dereva texi anayeendesha gari ili kujipatia riziki," anasema. "Lakini mustakabali wa mfanyakazi wa ofisini upo hatarini zaidi kuliko hata Dereva Texi, kwa sababu bado hatuna magari ya kujiendesha, lakini akili bandia bila shaka inaweza kuandika ripoti

www

Chanzo cha picha, Getty Images

Mara nyingi, wafanyikazi walio na uwezo mkubwa wa kufanya kazi na wenye eleimu ya juu watatishiwa zaidi kuliko hata wafanyikazi waliosoma kwa kiwango kidogo.

Hebu fikiria mtu ambaye anafanya kazi ya kusafisha vyumba vya hoteli ni ngumu sana kazi hiyo kufanywa na akili bandia au hata kiotomatiki."

Kwa kifupi, kutafuta majukumu katika mazingira yenye nguvu, yanayobadilika ambayo yanajumuisha kazi zisizotabirika ni njia nzuri ya kuzuia upotezaji wa aijra . Angalau, kwa muda.