Jose Eduardo dos Santos: Rais wa zamani wa Angola aaga dunia

Jose Eduardo dos Santos

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jose Eduardo dos Santos

José Eduardo dos Santos, rais wa zamani wa Angola ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 79, alikuwa akitibiwa ugonjwa ambao haujajulikana katika hospitali moja katika jiji la Barcelona nchini Uhispania.

Taarifa ya rais wa Angola kutangaza kifo hicho ilisema amekuwa akiugua ugonjwa wa muda mrefu.

Ilitoa heshima kwa urais wake wa muda mrefu, ikisema ametawala kwa uwazi na ubinadamu.

th

Vita vya wenyewe kwa wenyewe na urithi wake vilitawala sehemu kubwa ya miongo minne ya Dos Santos madarakani.

Alijiuzulu miaka mitano iliyopita, akimkabidhi waziri wake wa zamani wa ulinzi, João Lourenço, ambaye alichukua hatua haraka kufungua uchunguzi wa ufisadi, haswa katika sekta ya mafuta, ukilenga watoto wa kiongozi huyo wa zamani.

th

Chanzo cha picha, Getty Images