DR Congo kutekeleza marufuku dhidi ya usafirishaji madini ya kobalti

Muda wa kusoma: Dakika 5

Uzalishaji wa vifaa vya umeme vinavyotumika katika vifaa kama simu, kompyuta mpakato, na hata magari ya umeme huenda vikawa ghali zaidi hivi karibuni.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), mzalishaji mkubwa zaidi wa kobalti duniani –mdau muhimu katika utengenezaji wa baadhi ya bidhaa za elektroniki – imesema itatekeleza marufuku ya miezi minne ya kusafirisha bidhaa hiyo.

Kobalti ni metali ngumu, yenye kung'aa, rangi ya kijivu na fedha ambayo hasa hupatikana katika uchimbaji wa nikeli na shaba.

Hutolewa kwenye madini kama kobaltite na heterogenite, na huzalishwa kuwa cobalt sulfate au cobalt oxide kwa matumizi ya viwandani.

Ni hitaji muhimu katika utengenezaji wa betri za lithiamu-ion zinazoweza kuchajiwa ambazo hutumika katika simu za mkononi, kompyuta mpakato, na magari ya umeme.

Zaidi ya hayo, kobalti ni malighafi muhimu katika utendaji wa injini za ndege, zana za kukatia, na vipandikizi vya kimatibabu kutokana na uwezo wake mkubwa kuzuia joto na kutu.

Inapatikana kwa wingi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ambayo inaongoza kwa usambazaji wa kimataifa kwa zaidi ya 70% ya uzalishaji.

Nchi hiyo inasema uamuzi wake wa kusitisha usafirishaji imelenga kushughulikia ongezeko la usambazaji sokoni, ambalo limefanya bei ya Kobalti kushuka katika miaka ya hivi karibuni.

Mnamo Aprili 2022, bei ya kobalti ilifikia kiwango cha juu cha $82,000 kwa tani ya metik ton, lakini kufikia Februari 2025, bei imeshuka hadi $21,000 kwa tani ya metik ton. Hatua ya DRC inatarajiwa kupandisha gharama zaidi.

"Kitendo chochote cha kuingilia usambazaji wa kobalt kina athari kubwa kwa sekta mbalimbali, hasa katika vifaa vya elektroniki," alisema Anita Mensah, mchambuzi wa bidhaa katika Global Trade Insights, aliliambia BBC. "Watengenezaji watatakiwa ama kuvumilia gharama hizo au kuzilipia."

Athari za mara moja

Unaweza pia kusoma

Tangazo hili tayari linatishia sekta zinazotegemea kobalti kwa kiasi kikubwa, hasa utengenezaji wa vifaa vya elektroniki na magari ya umeme (EV).

Kobalti ni kifaa muhimu katika betri za lithiamu-ion, ambazo zinachaji simu za mkononi, kompyuta mpakato, magari ya umeme, na mifumo ya uhifadhi wa nishati mbadala.

Kwa kuwa DRC inasambaza zaidi ya 70% katika soko la kimataifa, usumbufu huu unatarajiwa kuwagusa watumiaji, na kuathiri bei za vifaa vya elektroniki na magari.

Peter Zhang, meneja wa usambazaji katika kampuni kubwa ya vifaa vya elektroniki, alisema "Tayari tunaona wauzaji wakibadilisha bei. Ikiwa marufuku ya usafirishaji itaendelea zaidi ya miezi mitatu, watumiaji wanapaswa kutarajia ongezeko la bei au mabadiliko katika ubora wa betri."

Kuahirishwa ghafla kwa usafirishaji tayari kumeibua ongezeko la bei katika soko la kobalti.

"Tuliona bei za kobalti zikifikia kikomo cha juu katika biashara siku moja tu. Bei huenda zikaendelea kubadilika," alisema David Okoro, mfanyabiashara wa vyuma mkazi wa London.

Lakini Joshua Cauthen, Mshiriki wa kampuni ya Sofala Partners, alisema hii huenda ikasababisha ongezeko la bei kwa muda mfupi tu, akitaja usumbufu wa awali wa usambazaji kama vile kufungwa kwa mgodi wa Mutanda na Glencore mwaka 2019.

"Ukubwa wa ongezeko la bei huenda ukadhibitiwa na ongezeko la sasa la usambazaji sokoni," alisema. "Baadhi ya wahusika wa soko wamekuwa wakijiandaa kwa usumbufu kwa kuhifadhi au kutafuta vyanzo vingine vya kobalti kwa mataifa kama vile Australia au Indonesia."

Nani atakayeathirika zaidi?

China inatarajiwa kuathirika zaidi kutokana na utegemezi wake mkubwa kwa kobalti ya Congo.

Marekani, Japani, Korea Kusini, Taiwan, na nchi za Ulaya zimejikita zaidi katika kutafuta njia mbadala za usambazaji na kufanya utafiti wa vifaa mbadala ili kupunguza utegemezi wa kobalti.

Ikiwa marufuku hii itaendelea, watumiaji wanaweza kushuhudia bei za simu za mkononi na kompyuta mpakato zikiongezeka bei,na kutafutwa kwa mbinu mbadala ya kukidhi uhitaji.

Cauthen pia alisisitiza kuwa sababu za kisiasa zinaweza kuathiri muda na ufanisi wa marufuku hii.

"Mzozo wa M23 umeongeza kwa kiasi kikubwa hitaji la Kinshasa kuwa na washirika na marafiki, jambo linaloweza kufanya serikali kuwa wazi kwa mazungumzo kuliko ilivyokuwa awali."

Alipendekeza kuwa nchi kama China au Zambia huenda zikatumia shinikizo la kiuchumi au kidiplomasia kupata msamaha au mbinu mbadala za biashara.

DRC itatekelezaje marufuku hiyo?

Mamlaka ya DRC zimeweka mikakati madhubuti kuhakikisha kampuni za uchimbaji zinazingatia sitisho la usambazaji.

Mashirika ya serikali, ikiwa ni pamoja na Direction Générale des Douanes et Accises (DGDA) na Direction Générale des Migrations (DGM), yamepewa jukumu la kufuatilia na kudhibiti usafirishaji katika maeneo muhimu ya mipakani.

"Hatua hii ni ya kudhibiti usambazaji kwenye soko la kimataifa, ambalo linakutana na ongezeko la uzalishaji," alisema Patrick Luabeya, Rais wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Masoko ya Madini (ARECOMS).

Hata hivyo, utekelezaji wa marufuku hiyo inaweza kuwa changamoto. "Sehemu kubwa ya migodi ya kobalti iko Lualaba na Haut-Katanga, ambazo hazikumbwi na migogoro mikubwa," alisema Cauthen.

"Lakini majimbo hayo yanayopakana na Zambia na Angola yana umbali unakaribia zaidi ya kilomita 1,000, mengi ikiwa maeneo ya mbali na yenye idadi ndogo ya watu.

Aliongeza kuwa miundombinu ya usafiri iliyokutengenezwa na Zambia yenye usimamizi dhaifu wa mipaka huenda ikafanya njia hiyo kuwa kivutio kwa ujangili wa kobalti.

Ili kuhakikisha utekelezaji wa sheria, serikali inaimarisha usimamizi wa uchimbaji wa kobalti katika sekta za viwanda na za kiufundi.

Sheria sasa zinakataza kuchanganya kobalti inayochimbwa viwandani, na ile ya wachimbaji wadogo wanapaswa kupeleka bidhaa zao kupitia linalodhibitiwa na serikali, Enterprise Générale du Cobalt (EGC).

Zaidi ya uangalizi wa kisheria, msako huu unajumuisha hali bora ya kazi. Mamlaka zimepiga marufuku waziwazi kuajiri watoto, mazingira hatarishi ya kazi, na uwepo wa watu dhaifu kwenye maeneo ya uchimbaji.

"Uchimbaji wa kobalti umekuwa ukihusishwa na masuala ya haki za binadamu," alisema Elizabeth Nkosi, mtetezi wa Haki za Wafanyakazi katika Jukwaa la Haki za Madini la Afrika. "shinikizo hili la utekelezaji linaweza kuwa hatua muhimu, lakini tu ikiwa serikali itaendelea kuwa thabiti na wazi."