'Nilifanyiwa upasuaji kuongeza makalio nilichokipata ni maumivu tu'

Yadira Perez ameondoa makalio yake tena.

Alionesha umbo la duara la manjano, dogo wakati daktari alipomwonesha picha ya tishu iliyopigwa miezi minne iliyopita.

"Mipira midogo ni biopolymers," alisema mpiga picha huyo mwenye umri wa miaka 43 kutoka Venezuela. Alisema kuwa tishu zilizokusanywa na damu kavu sio zake.

"Baadhi ya mipira hii midogo iliingia kwenye misuli yangu ya kulia na ilisababisha maumivu makali."

Yadira alidungwa sindano za biopolima kwenye makalio alipokuwa na umri wa miaka 26.

Kwa hakika, Yadira alijiona kuwa mwanamke mwenye sura nzuri na mrembo. Lakini mpenzi wake wakati huo alifikiri Yadira alikuwa na "makalio makubwa".

Yadira pia alitaka kumfurahisha mpenzi wake.

Baada ya kuingiza biopolymers kwenye makalio, makalio yao yakawa mekundu, magumu na ya moto. Hawakuweza hata kuketi au kujikunja.

Baada ya hapo, kila walipopata hedhi, walipata dalili hizo.

Biopolymer ni nyenzo ambayo huongeza ukubwa wa midomo, matiti au makalio.

Mnamo 2021, miaka 14 baada ya upasuaji wa Yadira, serikali ya Venezuela ilipiga marufuku matumizi ya "fillers" katika upasuaji wa urembo. Pia ilipigwa marufuku katika nchi kama Colombia, Brazil na Mexico.

Kwa vile upasuaji kama huo una uwezekano wa kufanywa kwa njia isiyo rasmi au kwa siri, takwimu za kimataifa za wagonjwa waliochomwa sindano za biopolima hazipatikani.

BBC Mundo iliwasiliana na saluni ya Caracas ambapo Yadira alikuwa amepandikizwa biopolymer, lakini haikupata jibu.

Katika muda wa miaka 16 tangu kupandikizwa, Yadira amefanyiwa upasuaji wa kuondoa lipolymer na biopolymer.

Wakati wa upasuaji wa mwisho, aliamua kuweka picha zake ili kuandika matibabu na kupona kwake. Yadira pia alilazimika kuchukua mkopo kupata upasuaji na matibabu huko Miami, Florida, USA. Aliishi Miami kwa miaka miwili.

Kundi la wanawake 44 asili yao kutoka Cuba, Colombia na Venezuela lakini wanaishi katika miji tofauti nchini Marekani. Wanawake hawa wote wanajiandaa kufanyiwa upasuaji wa kuondoa vipandikizi. Orodha pia ziko kwenye kundi hili.

Katika simulizi hii binafsi, ametoa habari juu ya mizunguko ambayo alilazimika kufanya kwenye hospitali, zahanati na wataalamu.

Je, dalili hizi husababishwa na vipandikizi vyake? Hawakuweza kutabiri kwa usahihi. Pia hakuna hata mmoja wao aliyempa matibabu mazuri ya kuondoa maumivu haya.

'Tupandikize makalio'

Mnamo 2007 kulikuwa na upasuaji wa urembo huko Caracas.

Wakati huo nilikuwa nikiishi na Henry, baba wa mtoto wangu.

Henry alileta magazeti kila wakati na kulikuwa na matangazo ya upasuaji huu.

"Angalia, wanafanya upasuaji wa makalio, tutakufanyia pia. Hebu fikiria, utakuwa na makalio makubwa," aliniambia siku moja.

Mwanzoni nilikataa, lakini mwishowe nikasema ndiyo ili kumfurahisha.

Tulikwenda mahali. Haikuwa kliniki rahisi pia. Lakini kulikuwa na chumba cha upasuaji. Vipandikizi vya matiti na liposuction vilifanywa hapo. Mahali hapa palikuwa Belo Monte, Caracas.

Tulipitia tangazo bila kushauriana na mtu yeyote. Katika tangazo hilo, ilisemekana kuwa watatumia vifaa vya kupandikiza vinavyotumiwa na madaktari wa upasuaji huko Amerika na Ulaya.

Mwili wangu ulikuwa mzuri sana. Ndio maana sikuwahi kufikiria kuwa na kipandikizi. Makalio yangu hayakuwa madogo sana wala makubwa sana. Ilikuwa sambamba kwa urefu na umbo la mwili wangu.

Lakini Henry alitaka makalio yangu yawe makubwa zaidi. Uhusiano wetu ulikuwa mwanzo tu. Tulikuwa kwenye uhusiano kwa takribani mwaka mmoja.

Nilikuwa nimepandikizwa hapo awali. Nilifanyiwa upasuaji wa matiti nilipokuwa na umri wa miaka 21. Wakati huo nilikuwa na uvimbe kwenye titi langu. Alipochunguzwa, iligundulika kwamba alikuwa na seli mbaya.

Nilifanyiwa upasuaji sehemu ya matiti yote mawili. Prosthesis (kiungo cha bandia) pia kiliwekwa.

Wakati mimi na Henry tulipokwenda kuchunguza, kulikuwa na safu ya wanawake wakisubiri kudungwa sindano za biopolima.

Aliyetutibu alituambia kuwa yeye ni daktari. Akatuonesha chupa ndogo iliyokuwa na kimiminika. Kimiminiko hicho kilipaswa kudungwa kwenye makalio yangu.

Lakini hawakuiita biopolymer. Alisema kuwa ni seli ndogo za ukuzaji ambazo zitatoa umbo la makalio.

Daktari alipanga miadi na mkewe. Alikuwa pia mwanamke mzee kama daktari. Pia alituambia kuwa amekuwa na dutu hii kwenye makalio yake kwa zaidi ya miaka 15 bila shida yoyote.

Alivaa suruali na fulana inayobana. Walionekana vizuri.

Sikuhitaji kupandikiza, lakini nilijua Henry angesisitiza hadi nitakapokuwa tayari. Kwa hiyo nikasema ndiyo.

Nilikuwa najiamini sana. Sikusoma chochote kuhusu hilo au kujua chochote kuhusu nilichokuwa nikifanya.

Daktari alinisafisha kwanza kwa dawa kisha akanidunga ganzi ya ndani. Nilikuwa nimelala kifudifudi kwenye machela, sikuweza kuona chochote.

Sikuweza hata kuona kile kifaa walichotumia kunipandikiza kilikuwaje au walichonidunga. Sikuhisi hata maumivu yake.

Waliweka bendeji ndogo juu ya kila shimo ambapo walikuwa wamedunga bipolymer na nikaja nyumbani.

Nilishangaa nilipojiona kwenye kioo. Henry aliniambia kuwa ninaonekana mrembo.

Lakini baada ya siku chache maji maji yakaanza kutoka na suruali yangu ilianza kuloa. Niliambiwa na daktari niweke plasta na kioevu kiliacha kutoka.

Madhara yalianza kuonekana

Nilihisi shimo ndogo na lilionekana kama selulosi. Henry aliniambia niende kwa daktari nirekebishe.

Daktari aliijaza kioevu zaidi lakini tundu dogo halikuziba (kujaa).

Wiki moja baada ya sindano hiyo ya pili, makalio yangu yalikuwa yamevimba. yalikuwa mekundu, magumu na yenye kuuma.

Baada ya hapo kiuno na mgongo wangu vilikuwa vimevimba hadi (mpaka mabegani).

Sikuweza kulala. Sikuweza kulala upande kwa sababu ya matiti bandia na kwa sababu ya biopolymer katika nyonga sikuweza kulala chali.

Kuketi ilikuwa kama kazi ngumu kwangu. Kulikuwa na maumivu makubwa.

Lakini nilipoanza kuwa na tatizo hili, kila kitu kuhusu Henry kilibadilika. Nilikuwa na uchungu sana hata hatukuweza kujamiiana.

Aliniwajibisha kwa hili. Hakuwa na subira. Alitaka raha ya kimwili katika hali yoyote. Hakuwa na uhusiano wowote na maumivu yangu au faraja na afya yangu.

'Ulisema ni salama'

Daktari alianza kunipa dawa kwa sindano ili kupunguza maumivu na uvimbe.

Kila mwezi nilipopata hedhi, nilikuwa na tatizo lilelile. Kiuno na mgongo viLIvimba. Yalikuwa mekundu, magumu na yenye maumivu sana.

Walinipa dawa kila mwezi lakini maumivu yalipungua kufikia mwezi uliofuata.

Henry alikuja nami kwa daktari. "Ulituambia kuwa ni salama. Hakutakuwa na majibu," alimwambia daktari.

Daktari alimwambia, "Usijali. Inatokea wakati mwingine. Lakini tutaitibu na kuiondoa."

Madaktari walitoa sindano kila mwezi kwa karibu mwaka.

Hatimaye, siku moja daktari aliniambia kwamba sindano za mara kwa mara zinamgharimu. Kwa sababu daktari hakuwa akinilipia.

'Usipandikize'

Henry na mimi tulirudi kuonana na daktari aliyenidunga sindano ya Bipolymer. Kwa sababu nilitaka kuwaambia kile kilichokuwa kikiendelea. Hata wakati huo kulikuwa na foleni ya wanawake kwa ajili ya vipandikizi pale.

Siku moja nilishusha suruali yangu ili kuwaonesha wale wanawake kwenye chumba cha kusubiri makalio mekundu na magumu na yenye maumivu.

"Hupati vipandikizi au hili litakutokea," nilianza kuwaambia kila mtu.

Kisha mmoja wao akasema, hii ni bahati nasibu. Hii haifanyiki kwa kila mtu.

Hatimaye daktari aliniambia kwamba hakuna kitu ambacho angeweza kufanya ili kunisaidia. "Moja unanitibu na kuniponya. La sivyo nitakuja hapa kila siku na kuwafukuza wengine kwa kuwaambia kilichotokea," nilimwambia daktari.

Kisha akalipa liposuction ya kwanza. Daktari mwingine wa utafiti alifanya upasuaji huo mwaka wa 2011. Baada ya MRI niligundua ni nyenzo ngapi zilikuwa kwenye chuchu zangu.

Daktari aliniletea chupa ya mayonnaise iliyojaa mipira ya biopolymer.

Nilijisikia vizuri kwa mwaka mmoja. Lakini tena mnamo 2012 nilianza kupata dalili sawa wakati wa hedhi.

Sikuwa na uvimbe mwingi mgongoni lakini makalio yalikuwa magumu kama mwamba. Daktari aliniambia nifanye MRI tena. Niliambiwa kuwa bado kulikuwa na takriban 15% bipolymer iliyobaki kwenye nyonga.

Nilifanya liposuction mara ya pili kwa gharama zangu mwenyewe. Baada ya hapo nililazimika kutumia mshipi kwa miezi mitatu.

Baada ya muda fulani nikapata mimba tena.

Nilipata binti yangu wa kwanza nilipokuwa na umri wa miaka 17. Sikuwa na shida na ujauzito wakati huo. Lakini wakati huu nikiwa na miaka 32, mimba yangu ilifeli.

Maumivu yalianza tena

Baada ya upasuaji wa pili, maisha yangu yalibadilika. Nimekuwa bila maumivu kwa karibu miaka 10. Lakini mwaka jana katika mwezi wa Oktoba kila kitu kilibadilika tena.

Lakini wakati huu dalili zilionekana sio tu kwenye nyonga au nyuma lakini pia kwenye uso na mikono. Kwa mara ya kwanza nilipata maumivu kwenye viungo vyangu.

Nilihisi homa. Mwili ulikuwa unawasha. Nilidhani kichwa changu kitalipuka.

Nilipokwenda hospitali nilikuwa nikitetemeka sana kwenye chumba cha dharura hadi namba yangu ilipopigiwa simu.

Nilimwambia daktari kwamba inaweza kuwa majibu kwa biopolymer. Lakini daktari hakujua nilichokuwa nikisema kweli.

Walifanya electrocardiogram na haikuonesha chochote. Madaktari walipima covid na mafua, hakuna walichobaini.

Nilikwenda kwa daktari kuelewa ni nini hasa kilikuwa kinatokea. Waliniambia chaguzi mbili. Walisema kwamba lazima iwe biopolymer iliyoachwa katika mwili wangu au bandia kwenye matiti yangu.

Pia alinishauri kuondoa bandia ya matiti.

Nilikuwa tayari nimekaa Miami kwa karibu mwaka mmoja na nusu. Kutokana na hili, wasiwasi na woga wangu ulikuwa unaongezeka. Nilitaka kurudi Venezuela kuona familia yangu.

Sikupata usaidizi kutoka kwa mama na kaka zangu nilipokuwa hospitalini. Kwa hivyo ilikuwa na athari kubwa kwangu. Kwa sababu tulikuwa karibu sana.

Daktari alinipa dawa za kupunguza mfadhaiko. Alisema kuwa mwili wangu unakuwa hivi kwa sababu ya unyongovu. "Kunywa kidonge kimoja kidogo na utajisikia vizuri," aliniambia.

Nilimwona daktari wa magonjwa ya akili. Alinionya kuwa vidonge hivyo vitaniletea madhara makubwa, alisema daktari. Alisema kuwa mwingiliano wako na mtoto utaisha, unaamua nini cha kufanya.

Kwa hiyo niliamua kutokunywa vidonge hivyo. Baada ya hapo, nilianza kutafuta wataalamu wa biopolymer ili kujua ni nini hasa kinachoendelea.

Nilipata daktari huko Colombia. Sikuweza kuondoka Marekani wakati huo kutokana na sababu zangu za uhamiaji. Lakini nilikuwa nikifikiria kupata ruhusa kwa sababu za kiafya. Kwa hivyo ningeweza kwenda na kufanyiwa upasuaji.

Nilikuwa na maumivu makali sana kiasi kwamba nilikuwa tayari kufanya lolote ili kuyapunguza. Nilikuwa tayari kuhatarisha hata mchakato wa uhamiaji wenyewe. Lakini polepole nilianza kujisikia vizuri na niliamua kufikiria zaidi kuhusu hali yangu.

Mchakato wa kurejesha baada ya yote haya ulikuwa mrefu sana na uchungu. Sikuweza hata kuketi kwa wiki tatu za kwanza baada ya upasuaji. Kwenda haja ndogo pia ilibidi kufanywa wakati umesimama.

Pia nilikuwa nikipata shida sana kulala. Nilikuwa najaribu kulala na mto chini ya tumbo langu. Kwa sababu mirija iliondolewa. Kwa hivyo sikuweza kulala kwenye mto.

Mtoto Leo alinisaidia sana wakati wa matibabu. Alisaidia katika kila kazi. Sikuweza kuendesha gari kwa miezi miwili, kwa hiyo sikuweza kumpeleka popote.

Nilifanya kazi kutoka nyumbani. Nilifanya kazi nikiwa nimesimama mbele ya kompyuta.

Nina vidonda vikubwa mwilini mwangu. Lakini alama hizo hazisababishi maumivu, zinanikumbusha yale niliyopitia.

Sasa nataka kueneza ufahamu kuhusu madhara ya biopolymers.

Ningewaambia watu wanaotaka kuifanya, msifanye. Usijisumbue kiasi hiki.

Pia nataka kuwakumbusha wale ambao wanaishi na maumivu haya kwamba kuna njia mbadala. Usikate tamaa.

Imetafsiriwa na Lizzy Masinga na kuhaririwa na Seif Abdallah.