Kylian Mbappe: Je mshambuliaji huyu hatari anaelekea Manchester United au Real Madrid?

Kylian Mbappe ameiambia Paris St-Germain kuwa hataongeza mkataba wake zaidi ya 2024, lakini anataka kusalia msimu ujao.

Hilo likitokea, mabingwa hao wa Ufaransa wana hatari ya kumpoteza kwa uhamisho wa bila malipo wa - kiasi cha euro 180m (£165.7m) chini ya walivyomlipa mwaka wa 2017.

Kwa hivyo watajaribu kumlipa pesa msimu huu wa joto?

Wakifanya hivyo, hakutakuwa na upungufu wa mashabiki, lakini ni idadi ndogo tu ya vilabu vinavyoweza kumudu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, amefunga mabao 212 na kuchangia mabao 98 katika michezo 260 tangu ajiunge na PSG kutoka Monaco, awali kwa mkopo miaka sita iliyopita - akishinda mataji matano ya ligi kati ya mataji 13 ya nyumbani akiwa na klabu hiyo.

Pia alichukua jukumu muhimu katika ushindi wa Kombe la Dunia la 2018 kwa Ufaransa na rekodi yake ya kimataifa ya mabao 38 katika mechi 68 inamweka nafasi ya tano kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote nchini mwake - 15 nyuma ya Olivier Giroud anayeshikilia rekodi hiyo.

Mnamo Desemba, Mbappe alifunga hat-trick ya kwanza katika fainali ya Kombe la Dunia tangu 1966 lakini kupoteza kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Argentina kulimnyima ushindi mtawalia wa Kombe la Dunia akiwa na umri wa miaka 23.

Hivyobasi huku akiendelea kuwa mchezaji bora Zaidi duniani, je anaelekea wapi

Real Madrid

Kylian Mbappe na meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti wakipeana mikono baada ya mechi ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa mwaka jana.

Rais wa Real Madrid Florentino Perez alisema Kylian Mbappe "lazima awe amebadilisha ndoto yake" baada ya kukataa kuhamia klabu hapo mwaka jana.

Mbappe alionekana kukaribia kusajiliwa na Real Madrid mwaka jana.

Mchezaji huyo aliyekuwa akivutiwa sana na wababe hao wa Uhispania, alikubali kifurushi cha fedha na Real na PSG huku akifikiria mustakabali wake kabla ya kumalizika kwa mkataba wake Juni.

Real walikuwa tayari kulipa euro 150m (£127m) kama ada ya kumsaini na mshahara wa euro 40m (£34m). Badala yake, Mbappe alichagua kukubali mkataba mpya na kusalia PSG, ingawa alisema ndoto ya kuichezea Real "haijaisha".

Kuondoka kwa Mfaransa mwenzake na mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or Karim Benzema kwenda Saudi Arabia kunamaanisha kuwa Real wako sokoni kutafuta mshambuliaji, huku Harry Kane wa Tottenham akidhaniwa kuwa kinara wa orodha yao ya wachezaji wanaosakwa.

Je, huu ndio mwaka ambao Real watampata mshambuliaji huyu?

Kikosi cha Carlo Ancelotti tayari kimetoa kauli moja ya kusaini msimu huu, kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham kwa euro 103m (£88.5m), na sasa wanaweza kujaribiwa kufadhili uhamisho mwingine.

Manchester United

Manchester United ni klabu nyingine kubwa ya Ulaya inayomwinda mshambuliaji huyu matata msimu huu wa joto - na miongoni mwa vilabu vichache vya Ligi ya Premia vilivyo na uwezo wa kifedha kufadhili uhamisho.

Bado kuna sintofahamu kuhusu umiliki wa baadaye wa klabu, hata hivyo, Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani na mzabuni mpinzani Sir Jim Ratcliffe wakisubiri kuona kama ofa zao za kununua klabu zitakubaliwa na familia ya Glazer.

Meneja Erik Ten Hag ametanguliza kujaza nafasi ya tisa katika dirisha lake la pili la uhamisho wa majira ya kiangazi, huku nahodha wa Uingereza Kane akiwa chaguo ikiwa mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy ataonyesha nia ya kumuuza mchezaji huyo..

Hata hivyo, habari za hali ya Mbappe huenda zikawashawishi United kumleta Mfaransa huyo Uingereza - na mmiliki yeyote mpya anayetarajiwa kupata fursa ya kuonyesha hisia zake za kwanza.

Saudi Arabia

Karim Benzema na mwenzake wa Ufaransa Kylian Mbappe wakikumbatiana

Karim Benzema alikubali kujiunga na mabingwa wa Saudi Arabia Al-Ittihad baada ya kuondoka Real Madrid

Saudi Pro League ni nyumbani kwa fowadi wa Ureno Cristiano Ronaldo na sasa mchezaji mwenza wa zamani wa Real Benzema. Je, Mbappe anaweza kujaribiwa kujiunga nao?

Vilabu vinne kati ya vinara vya Saudi Arabia vilichukuliwa hivi karibuni na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa nchi hiyo, ambao pia unamiliki Newcastle United na LIV Golf.

Uhamisho wa Ronaldo kwenda Al Nassr ulimfanya mshindi huyo mara tano wa Ballon d'Or kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani, huku Forbes wakiripoti mapato ya kila mwaka ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 kuwa $136m (£108.7m) mwezi Mei.

Baada ya klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia kumkosa mchezaji wa zamani wa Argentina Lionel Messi, ofa nono kama hiyo inatolewa kwa nyota mwingine wa kimataifa na Kylian Mbappe haitamshangaza.

Chelsea

Ulikuwa mwaka wa kwanza kabisa kwa Chelsea chini ya mmiliki mpya Todd Boehly, ambaye alianza kutumia zaidi ya pauni milioni 550 katika madirisha mawili ya uhamisho baada ya kuinunua klabu hiyo.

Huenda klabu hiyo isiwe wasimwage fedha za usajili kwa kiasi hiki msimu huu wa joto kwani wanataka kupunguza kikosi chao kilichojaa na pia kuhakikisha wanafuata kanuni za faida na uendelevu za Ligi Kuu.

Hata hivyo, mikataba mirefu ambayo wametoa - Mchezaji aliyesajiliwa kwa rekodi ya Uingereza ya euro 121m (£107m) Enzo Fernandez na nyongeza ya pauni milioni 89 Mykhailo Mudryk wote walijiunga kwa mikataba ya miaka minane na nusu - inawaruhusu kueneza gharama ya kila mchezaji kwa muda huo.

Ikimaanisha, iwapo watafanikiwa kupunguza ukubwa wa kikosi chao, Kikosi cha Boehly cha Blues kinaweza kuwa sokoni kwa ajili ya usajili mwingine huku wakipania kujinasua kutoka katika msimu mbaya uwanjani ambao uliwafanya kumaliza katika nafasi ya 12 kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Liverpool

Mbappe aliweka wazi jinsi anavyovutiwa na Liverpool mnamo 2020, akimtaja Jurgen Klopp kama "meneja mzuri sana" na timu yake kama "mashine" walipokuwa wakiwinda taji la kwanza la Ligi ya Premia.

The Reds hapo awali walihusishwa na Mbappe lakini Klopp alisema fowadi huyo alikuwa nje ya bei ya klabu yake - na alitoa jibu kama hilo huku kukiwa na mazungumzo ya kumsajili Bellingham mapema mwaka huu, hatua ambayo alilinganisha na mtoto anayeomba Ferrari kwa ajili ya Krismasi.

Ingawa kuna uwezekano kuwa hivyo bado mmiliki John Henry amesema anatarajia uwekezaji fulani katika klabu hiyo kwani wanalenga kushindana tena na washindi wa Ligi Kuu ya Uingereza Manchester City.

Huku PSG ikiwa na nia ya kutompoteza Mbappe bila kurejesha sehemu ya fedha zake za ununuzi je, bado kunaweza kuwa na fursa kwa Liverpool kama wataweza kuepuka kuingizwa kwenye vita vya zabuni?