Je! Ujasusi wa Israel ulishindwa vipi kuzuia mashambulizi makubwa kutoka Gaza?
Na Frank Gardner Mwandishi wa usalama wa BBC

Chanzo cha picha, Reuters
"Hatujui jinsi ambavyo hili limeweza kutokea."
Hayo ndio majibu ambayo maafisa wa Israeli wamekuwa wakitoa leo ninapowauliza ni kwa vipi, pamoja na rasilimali zake nyingi, ujasusi wa Israeli haukuona shambulio hili likija.
Makumi ya wapiganaji wa Kipalestina waliokuwa na silaha waliweza kuvuka mpaka wenye ngome nzito kati ya Israel na Ukanda wa Gaza, huku maelfu ya maroketi yakirushwa kutoka Gaza hadi Israel.
Kwa juhudi za pamoja za Shin Bet, ujasusi wa ndani wa Israeli, Mossad, wakala wake wa kijasusi wa nje na mali zote za Jeshi la Ulinzi la Israeli, inashangaza ukweli kwamba hakuna mtu aliyeona hili likija.
Israel ina huduma za ujasusi pana zaidi na zinazofadhiliwa vyema katika Mashariki ya Kati.

Ina watoa habari na mawakala ndani ya makundi ya wapiganaji wa Palestina, pamoja na Lebanon, Syria na kwingineko.
Katika siku za nyuma, imefanya mauaji ya viongozi wa wanamgambo kwa wakati uliopangwa, ikijua mienendo yao yote kwa karibu.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wakati mwingine mauaji haya yamefanywa kwa kutumia mashambulio ya droni, baada ya mawakala kuweka kilipuzi cha - tracker GPS kwenye gari la mtu binafsi; wakati mwingine huko nyuma imetumia hata simu za mkononi zinazolipuka.
Chini, kando ya uzio wa mpaka kati ya Gaza na Israel kuna kamera, vitambuzi vya mwendo wa ardhini na doria za kawaida za jeshi.
Uzio wa juu wa waya wa mkubwa unafaa kuwa "kizuizi mahiri" ili kuzuia aina haswa ya upenyezaji ambao umefanyika katika shambulio hili.
Hata hivyo wapiganaji wa Hamas walijibanza tu kupitia humo, wakakata mashimo kwenye waya au waliingia Israeli kutoka baharini.
Kujiandaa na kutekeleza shambulio kama hilo lililoratibiwa, ni lazima iwe imechukua viwango vya ajabu vya usalama wa uendeshaji na Hamas.
Haishangazi vyombo vya habari vya Israel vimekuwa vikiuliza maswali ya dharura kwa viongozi wa kijeshi na kisiasa wa nchi yao kuhusu kwa jinsi yote haya yangeweza kutokea, katika kumbukumbu ya miaka 50 ya shambulio lingine la kushtukiza la maadui wa Israeli wakati huo: vita vya Yom Kippur vya Oktoba 1973.
Maafisa wa Israel wananiambia uchunguzi mkubwa umeanza na maswali, wanasema, "itaendelea kwa miaka mingi".
Lakini hivi sasa Israeli ina vipaumbele muhimu zaidi. Inahitaji kuzuia uingiaji wa mipaka yake ya kusini, kuwaondoa wanamgambo hao wa Hamas ambao wamechukua udhibiti wa jamii kadhaa za upande wa Israel wa uzio wa mpaka.
Itahitaji kushughulikia suala la raia wake ambao wamechukuliwa mateka, ama kupitia ujumbe wa uokoaji wa silaha au kwa mazungumzo.
Itajaribu kuondoa maeneo ya kurusha roketi hizo zote zinazorushwa nchini Israel, kazi ambayo ni ngumu sana kwani zinaweza kurushwa kutoka popote bila taarifa.
Na pengine wasiwasi mkubwa zaidi kwa Israel ni hili: inawazuia vipi wengine kuitikia wito wa Hamas wa kutaka silaha na kuepuka mashambulio haya kuenea katika Ukingo wa Magharibi na pengine hata kuwavuta wapiganaji wenye silaha nzito wa Hezbollah kuvuka mpaka wake wa kaskazini na Lebanon?














