Kwanini meli zilizojaa gesi zimetia nanga pwani ya Ulaya?

.

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Meli kama hizo - zina gesi yenye thamani ya makumi ya mamilioni ya dola

Meli za mizigo zilirundikana kwenye mwambao wa Ulaya zikiwa zimejazwa na gesi asilia iliyoyeyuka.

Meli hazisogei popote, na hakuna anayezipakua.

Na hii inatokea wakati Ulaya inakabiliwa na shida ya nishati.

Hili linawezekanaje?

Meli nyingi kubwa za LNG zimewekwa kwenye pwani ya Uhispania, Ureno, Uingereza na nchi zingine za Ulaya.

‘’Hali hii ilichukua takriban wiki tano hadi sita,’’ anasema Augustine Preyt, makamu wa rais wa Kayrros, kampuni ya kimataifa ya uchambuzi wa nishati na mazingira ambayo hufuatilia msongamano wa meli kupitia satelaiti na mfumo maalum wa utambuzi unaotumiwa katika safari za baharini.

Hakika ni hadithi nzuri. ‘’Kwa kifupi, meli za mafuta zinasubiri hali ya hewa baharini. Kihalisi. Huwekwa ikiwa mafuta yanahitajika haraka mwanzo mwa hali ya hewa ya baridi.

Lakini, kwa kweli, kwa nini zisipakuliwe, na walizileta?

Swali linaweza kuonekana rahisi, lakini jibu lake ni gumu zaidi.

Kwanza, dhidi ya hali ya hofu iliyosababishwa na kusitishwa kwa usambazaji kutoka Urusi, Ulaya ilihifadhi gesi kwa kiasi kikubwa tu.

Mpango ulikuwa kujaza hifadhi zao kwa 80% ifikapo Novemba 1, lakini walijaza na kupitiliza mapema zaidi – na yatari hifadhi zimejazwa kwa 95%.

Lakini shehena hizo za thamani zinaendelea kuwasili.

Mchambuzi wa Wood Mackenzie Fraser Carson, ambaye pia anafuatilia jinsi meli za mafuta zinavyoongezeka, alihesabu meli 268 za LNG duniani kote kufikia mwezi Oktoba ikilinganishwa na wastani wa kila mwaka wa 241.

Kulingana na Carson, meli 51 ziko karibu na pwani ya Ulaya.

.

Chanzo cha picha, KAYRROS

Maelezo ya picha, Kulingana na Antoine Halff, hali ya soko ya sasa inasukuma wanunuzi kuweka meli za mizigo baharini
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Gesi iliyo kwenye vyombo hupozwa hadi digrii 160 hasi na kufanywa kuwa ya kimiminika kurahisisha usafirishaji.

Wakati huo huo, hakuna miti ya kutosha ambayo inaweza ‘’kufungua’’ mafuta ya kioevu kurudi kwenye gesi, kwani kwa muda mrefu Ulaya ilitegemea usambazaji wa gesi kupitia mabomba kutoka Urusi.

Kwa hivyo meli za mafuta zinangojea kwenye foleni ili kubadilishwa tena.

Ujerumani na Uholanzi, kwa mfano, tayari imewekeza katika ujenzi wa vituo vipya vya mchakato wa kubadilisha gesi asilia iliyoyeyuka kutoka awamu ya kioevu hadi awamu ya gesi.

Baadhi yao - zilizojengwa kwa kutumia meli za mafuta za LNG zilizowekwa kwenye gati - zinatarajiwa kuanza huduma ndani ya miezi michache ijayo.

Zaidi ya hayo, hali ya hewa wakati wa pukutizi imekuwa isiyo ya kawaida, hivyo mafuta kidogo yanahitajika kwa ajili ya joto kuliko kawaida wakati huu wa mwaka.

Kulingana na Antoine Halff, mwanzilishi mwenza wa Kayrros, shughuli za makampuni ya viwanda zinazotumia gesi barani Ulaya zimepungua.

‘’Tumeona kupungua kwa kasi kwa uzalishaji katika viwanda vya chuma na saruji,’’ Halff anasema.

Inasemekana kunawezekana kuwa na hali bei kupanda siku za usoni ikilinganishwa na hali ya sasa.

Hili ni neno la ubadilishanaji katika soko la siku zijazo, kumaanisha kwamba bei ya bidhaa ambayo itawasilishwa katika siku zijazo ni ya juu kuliko bei yake kwa sasa.

Hiyo nis awa na kusema: kusubiri kupata mafuta mnamo mwezi Desemba, na sio Novemba, itagharimu mnunuzi makumi ya mamilioni ya dola zaidi.

Mahitaji ya gesi kwa hali na mali sasa hivi inamaanisha kuwa nchi tayari zimelipa pesa nyingi kupata bidhaa hiyo.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nchi za Ulaya zilikimbilia kujaza hifadhi yao ya gesi kwa siku zijazo

Ujerumani, kwa mujibu wa Reuters, ilitumia euro bilioni 49.5 kuagiza bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi kati ya Januari na Agosti - ikilinganishwa na euro bilioni 17.1 katika kipindi kama hicho mwaka wa 2021.

Hizi ni nguvu za soko katika kazi, anasema Michelle Wiese Bockmann, mhariri wa soko na mchambuzi wa orodha ya Lloyd’s Uingereza, gazeti kongwe la masuala ya usafirishaji.

Pamoja na haya yote, anasisitiza, Ulaya iko katika nafasi nzuri zaidi, kwa kuzingatia hali ya kijiografia.

Wakati huo huo, inawezekana kabisa kwamba, kwa mfano, mtu huko Asia atanunua sehemu ya mizigo kutoka kwenye foleni ya Ulaya, na gesi itaenda huko.

Nini kinafuata?

Wakati wa vifaa vya kuhifadhia mafuta vimejaa kwa wiki chache zijazo, bei ya gesi barani Ulaya imeanza kushuka kwa kasi tangu Agosti, ingawa bado imesalia mara mbili ya bei ya mwaka jana.

Majira ya baridi kali na usumbufu unaowezekana kutokea wa usambazaji unaweza kubadilisha picha hiyo kwa kiasi kikubwa.

Kwa kuongezea, ununuzi wa kiwango cha juu wa gesi na nchi za Ulaya ulichochea kuongezeka kwa mapambano ya usambazaji wa mafuta muhimu ulimwenguni kote.

Na, kwa mfano, nchi kama Pakistan na Bangladesh, ambazo zinategemea LNG lakini zina uwezo mdogo wa soko, zimeachwa.

Na hivi karibuni Uchina, Japan na Korea Kusini zitajiunga na mchezo huo, ambao pia hutumia gesi nyingi na bila shaka watataka kuwa na hakikisho la usambazaji msimu wa baridi.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ni faida kwa Ulaya kuwa na meli kubwa za gesi baharini wakati wa msimu wa baridi

Hata hivyo, kulingana na Corey Grindal, mkuu wa biashara ya kimataifa katika mzalishaji wa gesi asilia ya Cheniere, kinachoendelea sasa hivi katika soko la LNG ni kitu cha muda mfupi sana.

Sehemu ya shauku ya kampuni ya LNG katika miaka ijayo inapaswa kuwa Ulaya kuwa na mpango wa usambazaji wa nishati kutoka sehemu tofauti tofauti.

Sehemu kubwa ya gesi inayozalishwa na Cheniere tayari imenunuliwa hadi mwisho wa mwaka, na kufikia 2026 kampuni hiyo inapanga kuongeza kiasi kutoka tani milioni 45 hadi 55 milioni.

Habari za hali hii kuhusu gesi haziwezi ila kukasirisha wafuasi wa mabadiliko ya vyanzo vya nishati mbadala.

‘’Nishati mbadala ni nzuri. Ni kwa ajili ya kufanya jambo sahihi kwenye sayari tunayoishi. Lakini tunahitaji mafuta kwa sasa,’’ anakariri Grindal.

Nini kitatokea baadaye inategemea sana hali katika vita vya Ukraine, hali ya hewa, kuongezeka kwa vyanzo vya nishati mbadala, mahitaji ya kimataifa ya gesi - na kwa mamia ya meli za LNG ambazo zitaenda ama mashariki au magharibi.