Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Napoli inataka kumsajili De Bruyne

Chanzo cha picha, Getty Images
Napoli wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wake wa Manchester City utakapokamilika msimu huu wa kiangazi. (Times- usajili unahitajika)
De Bruyne ana nia ya kusalia Ulaya, na Aston Villa inasadikiwa kuwa miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyofuatilia hali yake. (i paper)
Napoli pia inamfuatilia kiungo wa kati wa Manchester City Jack Grealish mwenye umri wa miaka 29. (Sun)
Mshambuliji wa Manchester United Muingereza Marcus Rashford, 27, ambaye yuko kwa mkopo Aston Villa, anapania kuhamia Barcelona msimu huu. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
Beki wa Bayer Leverkusen Jeremie Frimpong ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 29.7 katika kandarasi yake, inaipatia furasa kubwa Liverpool ambao wanamtaka nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 24. (Sportsport)
Klabu za Liverpool, Arsenal na Manchester City zimewasiliana na winga wa Brazil Rodrygo, 24, kutoka Real Madrid kwa lengo la kumsajili. (Tbrfootball)
Crystal Palace wana uhakika wa kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Joe Willock mwenye umri wa miaka 25 kutoka Newcastle msimu huu wa kiangazi. (Chronicle Live)

Chanzo cha picha, Getty Images
Borussia Dortmund wamejiunga na mbio za kumnunua kiungo wa kati wa Sunderland Muingereza Jobe Bellingham, 19, ambaye pia amekuwa akiwindwa na Manchester United. (Talksport)
Aston Villa hawataki kumpoteza kiungo wa England anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 90 Morgan Rogers, ambaye ananyatiwa na Chelsea, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 yuko tayari kuhama ikiwa nafasi hiyo itajitokeza. (Teamtalk)
Al Hilal ina nia ya kumnunua mshambuliaji wa Liverpool kiungo wa kimataifa wa Uruguay Darwin Nunez,25, na winga wa Colombia Luis Diaz mwenye umri wa miaka 28. (Caught Offside)
Chelsea inataka kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Emanuel Emegha kutoka Strasbourg, huku Newcastle pia ikiwa na mpango wa kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Football Mercato - kwa Kifaransa)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












