Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fahamu lishe unayopaswa kula kutokana na umri wako
Je unakula kuishi au unaishi kula? Uhusiano wetu na chakula kwa asili ni mgumu, kwani unahusisha bei, upatikanaji wake na wale tunaokula nao . Lakini kitu kimoja ambacho huwa ni muhimu wakati wote ni njaa – hamu ya kula.
Wakati hisia ya njaa inapotokea, mwili hufahamu kwamba chakula kinahitajika. Hii ni hisia asilia. Lakini mara nyingi huwa tunakula hata kama hatuhisi njaa au wakati mwingine hatuli hata kama tunahisi njaa
Utafiti wa hivi karibuni umefichua kuwa harufu ya chakula, sauti , ni mambo yanayotufanya tule chakula kupita kiasi.
Kadri umri wetu unavyosonga , ndivyo hamu yetu ya kula inavyoongezeka. Kama mwandishi Shakespeare anavyosema , kuna hatua saba za njaa. Unapoelewa hatua hizi, unaweza kuepuka kula kupindukia au kula chakula kidogo na kuepuka madhara ya kiafya yanayotokana na ulaji wa chakula .
Utoto ni kipindi cha furaha ...
Katika hatua ya kwanza ya utoto, ukuaji wa mwili ni wa haraka. Tabia za kula katika umri huu huendelea kuwa sawa katika umri wa baadaye.
Kwanza mtoto hunenepa na anapokuwa mwanaume au mwanamke hunenepa kulingana na umri wake.
Hali ya mtoto ya kukataa kula chakula au kukiogopa inaweza kumsababishia mtoto kushindwa kuridhika na chakula.
Lakini iwapo mtoto atapewa chakula chenye ladha fulani mara kwa mara na mtoto akaweza kukila kwa kukipenda , mtoto anaweza kula vyakula vipya kama vile mboga za majani na kuzipenda.
Watoto wanapaswa kujifunza ni kiasi gani cha chakula wanachopaswa kula, jinsi ya kudhibiti kiasi cha chakula.
Wazazi wanaosisitiza kuwa ni lazima chauka kiishe kwenye sahani wanaweza kuingilia kati kwa kuwapatia watoto chakula wakati wananjaa.
Watoto hawapaswi kujumuishwa katika matangazo ya vyakula ambavyo havina faida ya lishe mwilini , kwani matangazo hayo hujenga tabia ya watoto kula vyakula hivyo.
Hii hupelekea watoto kuongeza uzito wa mwili na kujipata katika hatari ya magonjwa ya kudumu kama vile kisukari, na magonjwa ya moyo.
Umri wa kubalehe
Mara nyingi homoni huchangia pakubwa na mara kwa mara kwa kijana au msichana mwenye umri wa kubarehe kuhisi njaa. Jinsi vijana wenye umri huu wanavyokula huelezea ni jinsi gani watakavyokula baadaye .
Hii inamaanisha kuwa tabia za kula ambazo zimekuwepo wakati wa umri wa kubarehe huathiri kizazi kijacho, kwani watoto hawa huendelea kuku ana kuwa wazazi. Kwa bahari mbaya huwa kuna ukosefu wa muongozo wa ulaji unaofaa katika umri huu, na athari za ulaji huu mbaya hujitokeza baadaye maishani mwao.
Magonjwa yanayohusiana na utapiamlo ni ya kawaida miongoni mwa wasichana na wavulana walio katika umri wa kubalehe .
Je unakuwa na njaa kiasi gani katika umri wa miaka 20?
Mabadiliko mengi ya mtindo wa maisha hutokea katika hatua hii. Katika umri huu , huwa masomo ya chuo yamekamilika, baadhi huwa wameolewa , au wanaishi na wenza wao.
Baadhi ya watu huwa ni wazazi wanaoishi na wenza wao. Wengine huwa ni wazazi kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza uzito wa mwili.
Wakati unene wa mwili unapoongezeka, ni vigumu sana kupunguza kiwango cha mafuta mwilini.
Tunapokula chakula kidogo, mwili huashiria kuhitaji chakula zaidi. Hatahivyo kiwango cha kujizuia kula chakula kupita kiasi huwa ni cha chini. Hii hupelekea mtu kula chakula kupita kiasi.
Baada ya kula, mtu huhisi hali ya kuridhika na kushiba.
Hali hii pia imewafanya watafiti kuichunguza kwa kina. Hii ni muhimu sana wakati unapopunguza uzito wa mwili.
Kwasababu kikwazo kikuu cha kula chakula kidogo kuliko kile ambacho mwili kinamaanisha kuwa mtu atahisi njaa wakati wote.
Pingamizi tofauti hutuma ishara tofauti kwa mwili wetu.
Miaka 30 na ushee, 40 na ushee na hatari zake
Miongo hii ni tofauti sana inapokuja katika suala la ulaji. Kwasababu kundi hili la miaka lina changamoto zaidi ya ujazaji wa tumbo. Katika umri huu, msogo wa mawazo ni wa hali ya juu. Hii husababisha mabadiliko katika hamu ya kula.
Takriban 80% ya watu wenye umri huu huwa wana mabadiliko haya. Kundi hili limegawanyika katika makundi mawili. Wale wanaokula kupindukia na wale wanaojaribu kuzia hamu ya kula .
Mambo haya yote yanahitaji udadisi. Ni chakula cha aina gani ambacho wanauraibu nacho. Wataalamu wengi hawako tayari kukiri kwamba kuna kitu cha aina hii.
Kuangazia majukumu au kutaka kuyatekeleza kikamilifu pia inaweza kuleta uwiano wa mshongo wa mawazo na tabia za ulaji.
Pia ni changamoto kubwa kupunduza kiasi cha vyakula vilivyochakachuliwa au vyakusindikwa katika maeneo ya kazi, makuambuni yanapaswa kujaribu kuzingatia mtindo wa ulaji wa vyakula vyenye kuleta afya ya mwili ili kupunguza msongo.
Hatari ya katika umri wa miaka 50 na ushee
Ukweli ni kwamba kufahamu kwamba kitu ni kizuri kwako haiwezi kukufanya ubadili tabia.
Lazima tule kile tunachokitaka bila kubadili mtindo wa maisha. Hata kama utakula kitu kibaya, mawazoni unahitaji afya ya mwili na akili.
Lakini tufahamu kuwa chakula tunachokila kina athari kwa afya yetu iwe nzuri au mbaya .
Kuvuta sigara, lishe duni, ukosefu wa mazoezi ya mwili, na vilevi vinaaathir moja kwa moja afya yetu na uwezo wa kuzaa.
Kati ya umri wa miaka 40 na 50 , watu wanapaswa kula na kunywa akulingana na hali zao za kiafya .
Matokeo ya Shinikizo la damu, kolestro hayaonekani moja kwa moja , kwahivyo watu huwa hawabadili mtindo wao wa maisha.
Miaka zaidi ya 50
Baada ya umri wa miaka 50 , uzito wa misuli hupungua kwa asilimia 0.5-1 Asilimia moja ya misuli hupotea kila mwaka. Hali hii hujulikana kama sarcopenia kwa lugha ya kitaalamu.
Ukosefu wa mazoezi ya mwili, kiwango kidogo cha protini katika vyakula na vinywaji, ukomo wa hedhi miongoni mwa wanawake huongeza viwango vya kupotea kwa misuli.
Mlo wenye virutubisho na mazoezi ya mara kwa mara ni muhimu miongoni mwa wanawake hupunguza athari za uzee.
Vyakula vyenye bei nafuu vyenye viwango vya juu vya protini ni muhimu.
Miaka sabini na ushee...
Madawa mbali mbali na tiba zilizopo kwa ajili ya magonjwa hatari, vimeongeza umri wa kuishi lakini maisha ya kiafya bado hayajaboreka kwa kiasi hicho.
Iwapo hali itaendelea kuwa kama ilivyo, idadi kubwa ya wazee katika jamii zetu na idadi ya wagonjwa wanaotegemea usaidizi itaongezeka.
Mlo uliosheheni virutubisho vya mwili ni muhimu kwa wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 70.
Kadri umri unavyoongezeka, ndivyo chakula kinavyopungua.
Hii husababisha kushuka ghafla kwa uzito wa mwili, na kuufanya mwili kuwa mwembamba.
Baadhi ya magonjwa mapya yanaweza kupona kutokana na kupungua kwa mlo.
Matibabu kama vile ya athari za augonjwa wa ubongo wa Alzheimer huathiri hamu ya kula.
Hatuwezi kupuuza umuhimu wa chakula kama petroli kwa ajili ya miili yetu katika hatua yoyote ya maisha yetu
Maelezo muhimu:
- Mlo wenye afya husaidia kuulinda mwili dhidi ya rutapiamlo na magonjwa ya kudumu mkiwemo kisukari, magonjwa ya moyo, kiharusi na saratani.
- Chakula kisicho cha afya na ukosefu wa mazoezi ya mwili husababisha hatari za kiafya
- Ulaji wa vyakula vyenye virutubisho unafaa kuanza mapema maishani – unyonyeshaji huharakisha ukuaji wa mtoto na kuboresha ukuaji wa utambuzi , na unaweza kuwa na faida za musa mrefu za kiafya
- Ulaji wa vyakula vyenye kutia nguvu mwilini (karoli) unafaa kuwa wa kiasi na unaowiana na matumizi ya nguvu ya mwili wako kila siku
- Kuwa na ukomo cha kiasi cha sukari wa chini 10% ya jumla ya vyakula vyote vyenye kutia nguvu mwilini (2, 7) ni sehemu ya lishe yenye afya
- Kula chini ya gramu 5 za chumvi kwa siku ili kuzuia kupanda kwa mapigo ya moyo, na kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo nakiharusi miongoni mwa mwa watu wazima (8).
Chanzo: Shirika la afya Duniani -WHO